Atualize para o Pro

MUONEKANO WA NABII ISSA MIAKA HIYO ULIKUWAJE ?

Karibu kila mtu ana dhana fulani kuhusu muonekano wa Yesu Kristo.
Ndiye mtu aliyechorwa zaidi katika sanaa ya Magharibi. Picha zake hutambuliwa kwa urahisi, ambapo huoneshwa akiwa na nywele na ndevu, akiwa amevalia vazi lefu lenye mikono mirefu linalofanana na kanzu ( la rangi nyeupe), na pia akiwa amejifunga joho (la rangi ya samawati). Muonekano wa Yesu umefahamika sana na wengi kiasi kwamba unaweza kutambuliwa ukiwa hata kwenye mikate au biskuti.

Picha za sasa za Yesu zinatokana na enzi ya Byzantine, himaya iliyokuwa na mji mkuu wake Constantinople. Ni picha iliyoanza kutumika karne ya nne hivi. Michoro ya Yesu ya wakati wa utawala wa Byzantine ilikuwa ya ishara, na si muonekano wake. Wasanii waliangazia zaidi maana na si kumfananisha na Yesu mwenyewe.
Picha zao ziliongozwa na dhana ya Yesu kama mtawala, kwenye kiti cha enzi, kama anavyoonyeshwa kwenye mchoro ulio kwenye altari ya kanisa la Santa Pudenziana jijini Roma.

Yesu anaoneshwa akiwa amevalia mgolole wa rangi ya dhahabu.
Ndiye mtawala wa dunia yote aliyetoka mbinguni, mfanano wa picha yake ni ule wa sanamu ya Zeus wa Olympus anayeonyeshwa akiwa na nywele ndefu za ndevu kwenye kiti cha enzi. Ni sanamu iliyokuwa maarufu sana wakati huo kiasi kwamba Mfalme Augustus wa Roma alishurutisha naye atengenezewe sanamu kama hiyo, lakini yake ikiwa bila nywele ndefu na ndevu, Wasanii wa Byzantine, walitaka kumuonyesha Kristo kama mtawala kutoka mbinguni, mfalme wa aina yake, na hivyo wakachora wakimuonyesha kama Zeus, lakini akiwa mdogo kidogo wa umri.

Kilichotokea kadiri miaka ilivyosonga ni kwamba kuonyeshwa huku kwa Kristo kama mtawala kutoka mbinguni - ambapo wakati mwingine ameonyeshwa hata akiwa kama 'hippie' au 'superstar' (kama ilivyo kwenye mchoro huu hapa chini) - ndiko kumekuwa kama kigezo chetu cha Yesu alivyokuwa. Hebu tuchanganue kutoka kichwani hadi vidole vya miguuni. Wakristo wa nyakati za kwanza wakati walipokuwa wanamwonyesha Kristo si kama mtawala kutoka mbinguni, walimuonyesha kama binadamu wa kawaida tu - akiwa hana ndevu na hana nywele ndefu.

Lakini pengine, kama msomi wa aina yake aliyekuwa akisafiri kutoka eneo moja hadi jingine, Yesu pengine alikuwa na ndevu, kwa sababu hakuwa akienda kwa vinyozi. Kwa kawaida, kuwa mchafu kiasi na kuwa na ndevu ndefu ni sifa ambazo zilihusishwa na wanafalsafa, wasomi wa ngazi ya juu, na kuwatenganisha na watu wa kawaida.
Mwanafalsafa maarufu wa kundi la Stoic (Wanafalsafa wa Kigiriki waliofuata mafundisho ya mwanzilishi wao Zeno wa Citium mjini Athens mapema karne ya 3 kabla ya kuzaliwa kwa Yesu) Epictetus aliamini "ilifaa hivyo kwa mujibu wa maumbile." Mambo yalibadilika katika karne ya 1 baada ya kuzaliwa kwa Yesu, wakati wa enzi za Warumi na Wagiriki, ambapo kuwa na nywele fupi na kunyoa ndefu ndiyo mambo yaliyochukuliwa kuwa yafaayo na ya kistaarabu.

Kuwa na nywele ndefu na ndevu ni mambo ambayo yaliachiwa miungu pekee, si ya watu wa kawaida. Hata wanafalsafa enzi hizo walikuwa na nywele fupi. Ndevu pia hazikuwa sifa za kuwatambulisha Wayahudi enzi hizo. Ukweli ni kwamba moja ya changamoto ambazo waliotaka kuwatesa Wayahudi vipindi mbalimbali katika historia walihangaika sana kuwatofautisha na watu wengine. Hii ni kwa sababu wote walifanana (jambo ambalo limegusiwa katika kitabu cha Wamakabayo). Hata hivyo, picha za wanaume wa Kiyahudi zilizokuwa kwenye sarafu za Judea Capta ambazo zilitolewa na utawala wa Roma baada ya kutekwa kwa mji wa Yerusalemu mwaka 70 baada ya kuzaliwa kwa Yesu zinawaonesha wanaume wakiwa na ndevu, lakini nywele zao si ndefu.

Kwa hivyo, Yesu, kama mwanafalsafa wa muonekano wa kawaida, kuna uwezekano alikuwa na ndevu lakini si ndefu sana, sawa na wanaume hao walioonyeshwa kwenye sarafu za Judaea Capta, lakini nywele zake basi hazikuwa ndefu sana pia.
Kama ingetokea kwamba awe na nywele ndefu hata kidogo tu kuliko kawaida, basi angezua mtafaruku Wanaume wa Kiyahudi waliokuwa na ndevu ambazo hazikuwa zimetunzwa vyema na nywele ambazo zilikuwa ndefu kidogo kuliko kawaida walitambulika mara moja kama watu waliokuwa wamekula kiapo cha kuwa Wanazari (Nazarite).

Hii ilikuwa na maana kwamba wangejitoa wakfu kwa Mungu kwa kipindi fulani, ambapo hawangekunywa vileo wala kuzikata nywele zao. Mwisho wa kipindi hicho, wangenyolewa nywele zao katika sherehe maalum hekaluni Jerusalem (kama inavyoelezwa katika kitabu cha Matendo ya Mitume, Sura ya 21, aya ya 24).
Lakini Yesu hakuwa amekula kiapo cha kuwa Mnazari, kwa sababu mara nyingi tunamsikia kwenye Biblia akinywa divai - wakosoaji wake hata wakati mwingine wanamshutumu kwa kunywa divai sana, kupita kiasi (Matayo Sura ya 11, aya ya 19). Kama angekuwepo na nywele ndefu, na kuonekana kama Mnazari, tungelitarajia basi kuwepo na tamko pahala fulani kuhusu tofauti ya muonekano wake na matendo aliyokuwa akiyafanya ambayo hayakuendana na Unazari. Hali kwamba alikuwa akinywa divai yenyewe ingekuwa tatizo kubwa.

Wakati Yesu alipoishi, matajiri walizoea kuvalia kanzu na majoyo ya vitambaa vya thamani, kuonyesha hadhi yao katika jamii. Katika moja ya mahubiri yake, Yesu anasema : "Jihadharini na walimu wa sheria (waandishi). Wao hupenda kutembea wakiwa wamevaa mavazi marefu (stolai), na kusalimiwa kwa heshima masokoni. Pia wao hupenda kukaa kwenye viti vya mbele katika masinagogi, na kupewa nafasi za heshima katika karamu." Mafundisho haya ya Yesu kwa kawaida huchukuliwa kama yenye maelezo ya kuaminika zaidi kwenye Injili, hivyo tunaweza kuwa na msingi kuamini kwamba Yesu hakuvalia mavazi kama hayo marefu. Kwa jumla, mwanamume wakati huo wa Yesu angevalia gwanda au kanzu fupi hivi, na mwanamke angevalia vazi lililomfika kwenye kifundo cha mguu.

Kwa hivyo, katika karne ya 2 kwenye kitabu cha Matendo ya Mitume, Paul na Thecla, inapotokea kwamba Thecla ambaye ni mwanamke anavalia kanzu fupi kama mwanamume, hilo ni jambo linaloshangaza sana. Kanzu hizi kwa kawaida zingekuwa na ukanda au mstari wa rangi tofauti kutoka kwenye bega hadi kwenye pindo sehemu ya chini. Ni vazi ambalo lingeshonwa au kufumwa kama kipande kimoja cha vazi. Juu ya kanzu hiyo, ungejifunga joho au vazi jingine la nje, na tunajua kwamba Yesu alivalia vazi kama hilo kwa sababu ndilo lililoguswa na mwanamke aliyetaka kuponywa naye. (Marko 5:27): Alikuwa amesikia habari za Yesu, naye akaja kwa nyuma yake kwenye umati wa watu, akaligusa vazi lake, kwa maana alisema moyoni mwake, 'Kama nikiweza kuligusa vazi lake tu, nitaponywa.') Vazi hilo la nje lilifumwa kwa manyoya, lakini halikuwa zito sana na ndipo ili uhisi joto ingemlazimu mtu kuvalia mavazi mawili kama hayo.

Vazi hilo lingevaliwa kwa njia nyingi, na wakati mwingine lingening'inia hadi chini ya magoti na kulifunika lile kanzu fupi la ndani. (Baadhi ya wanafalsafa walizoea kuvalia vazi hilo la nje pekee bila kuvalia ile kanzu ya ndani na kuacha sehemu ya bega au kifua ikiwa wazi). Mamlaka na hadhi ya mtu ni vitu ambavyo vilidhihirishwa kupitia ubora, ukubwa na rangi ya mavazi hayo ya nje. Rangi ya zambarau na baadhi ya aina za rangi ya buluu (samawati) ni rangi zilizoashiria utajiri, hadhi na kujionea fahari. Zilikuwa ni rangi za kifahari kwa sababu viungo vya kutengeneza rangi hizo vilikuwa adimu na ghali sana.

Lakini rangi pia huashiria kitu kingine tofauti. Mwanahistoria Josephus, anawaeleza walokole waliofahamika kama Zealots (kundi la Wayahudi wa itikadi kali waliotaka kuwafurusha Warumi kutoka Judea) kama kundi la wahalifu wauaji waliovalia mavazi ya nje yaliyopakwa rangi kwa jina - mavazi anayoyaita chlanidia - kuashiria kwamba yalikuwa ni kama mavazi yaliyovaliwa na wanawake. Hii inaashiria kwamba wanaume kamili, kama hawakuwa na cheo cha juu zaidi katika jamii, walifaa kuvalia mavazi yasiyopakwa rangi.
Yesu hakuvalia mavazi meupe hata hivyo. Haya yalikuwa mavazi ya kipekee na yalihitaji kupaushwa mara kwa mara (kufanywa meupe tena) au kupakwa chokaa. Judea, mavazi kama hayo meupe yalihusishwa na kundi lililofahamika kama Essenes - ambao ni watu waliofuata ufasiri mkali wa sheria za Kiyahudi. Tofauti kati ya mavazi ya Yesu na mavazi mengine ya rangi nyeupe ya kung'aa inaelezwa kwenye sura ya 9 ya Marko ambapo anaandamana na mitume watatu mlimani.

Yesu aliwachukua "Petro, Yakobo na Yohana, akawapeleka juu ya mlima mrefu, mahali walipokuwa faraghani. Huko, Yesu akageuka sura mbele yao. Mavazi yake yakawa na weupe wa kuzima macho, meupe kuliko ambavyo mtu yeyote duniani angaliweza kuyangʼarisha. Mose na Eliya wakawatokea, wakawa wanazungumza na Yesu." Marko anaeleza kwamba mavazi ya Yesu yaligeuka rangi yakawa meupe sana, hapa anarejelea vazi la ndani na si la nje. Kabla ya kugeuka sura huku kwa Yesu, anaoneshwa na Marko kama mwanamume wa kawaida, aliyevalia mavazi ya kawaida, ambayo ni ya rangi ambayo haijapaushwa. Katika hali ambayo ndipo yang'ae na kuangaza unahitaji kumpelekea fundi.

Tunaelezwa zaidi kuhusu mavazi ya Yesu wakati wa kusulubiwa kwake, pale wanajeshi wa Kirumi wanapoyakata mavazi yake ya nje vipande vinne (Yohana19:23: Askari walipokwisha kumsulubisha Yesu, walichukua nguo zake wakazigawa mafungu manne, kila askari fungu lake. Ila walikubaliana wasilichane lile vazi lake kwa maana lilikuwa halina mshono bali limefumwa tangu juu hadi chini.) Kuna uwezekano mavazi hayo ya nje yalikuwa mavazi mawili.

Moja ya vazi hili huenda lilikuwa ni tallith, ambalo ni vazi la kujifunga Kiyahudi wakati wa maombi. Vazi hili lenye shada (tzitzith) limetajwa moja kwa moja na Yesu katika kitabu cha Mathayo 23:5 anapozungumza kuhusu walimu wa sheria na Mafarisayo (Wao hutenda mambo yao yote ili waonekane na watu. Hupanua vikasha vyao vyenye maandiko ya sheria na kurefusha matamvua ya mavazi yao). Lilikuwa ni vazi la nje lisilo zito, ambalo kawaida lilitengenezwa kwa kitambaa cha manyoya na lilikuwa la rangi ya malai hivi (krimu), na pengine lilikuwa na ukanda au mstari wa rangi ya nili (bluu iliyoiva).

Miguuni, Yesu angevalia ndara (kandambili au malapa). Kila mtu wakati huo alivalia ndara. Katika mapango yaliyo jangwani karibu na Bahari ya Chumvi (Bahari Mfu) na Masada, ndara za wakati alipoishi Yesu zimegunduliwa, na tunaweza kutazama ndara ambazo huenda alivaa zilivyoonekana. Zilikuwa hazijafanyiwa kazi nyingi sana ya kiufundi. Soli (nyayo au kikanyagio) zake zilikuwa vipande vigumu vya ngozi vilivyoshonwa pamoja, na juu kulikuwa ni kanda za ngozi ambazo mbele zingeingizwa katikati ya vidole, kama malapa tu ya siku hizi.

Yesu (Nabii Issa) Alikuwa Myahudi, na uso wake pia bila shaka ungefanana na Wayahudi wa wakati huo. Hali kwamba Yesu alikuwa Myahudi (au Mjudea) ni jambo linalorejelewa katika vitabu vingi, zikiwemo barua za Mtume Paulo. Na katika barua yake kwa Waebrania, anaandika: "Kwa maana ni dhahiri kwamba Bwana wetu alitoka katika uzao wa Yuda" (Sura ya 7:14) Kwa hivyo, Myahudi wa wakati huo, mwanamume wa miaka 30 hivi alipoanza kueneza Injili kwa mujibu wa Luka 3, pia akiwa ni mwenye ngozi nyeusi kama ilivyokuwa kwa wayahudi wengi zama zile waliokuwa wakitembeleana na ndugu zao wa Misri (Kushi) kemet.

Mwaka 2001 mwanaantholopojia (mtaalamu wa elimu ya binadamu hasa elimu ihusuyo habari zinazohusu asili na maendeleo yake ya awali) Richard Neave alitengeneza mfano wa mwanamume wa Galilaya wa zama za Yesu ambao ulitumiwa kwa jina Son of God (Mwana wa Mungu). Alitumia fuvu lililopatikana katika eneo hilo. Hakusema kwamba huo ulikuwa muonekano wa uso wa Yesu. Mfano ulikuwa tu wa kuchochea hisia na kuwafanya watu kumfikiria Yesu kama mwanamume wa zama hizo na eneo hilo, kwa sababu hakuna mchoro wala maelezo yaliyopo ya kina kuhusu muonekano wake halisi.

Ingawa tunaweza kupata viashiria kutoka kwa teknolojia na kutumia mifupa ya watu wa kale, kiashiria cha karibu sana kuhusu pengine Yesu alionekana vipi labda kinaweza kutokana na mchoro wa Musa kwenye ukuta wa sinagogi ya karne ya 3 ya Dura-Europos, kwani mchoro huo unaonesha jinsi Myahudi wa hekima alidhaniwa kuwa wakati wa utawala wa Wagiriki na Warumi. Musa anaoneshwa akiwa na mavazi ambayo hayajapaushwa, na moja ya vazi lake la nje ni tallith.

Katika mchoro huo wa Dura wa Musa akitenganisha maji kwenye Bahari ya Sham ili Waisraeli wapite, unaweza kuziona shada (tzitzith) kwenye kona za vazi hilo. Kwa kiwango kikubwa, picha hiyo pengine inatoa msingi bora zaidi wa kumfikiria Yesu alivyokuwa badala ya picha za sasa zinazoongozwa na busara na mawazo ya enzi ya Byzantine - alikuwa na nywele fupi, ndevu fupi, na alikuwa amevalia kanzu fupi lenye mikono mifupi, na alikuwa na joho au vazi la nje.

Makala hii chimbuko lake ni makala ya Kiingereza ya Joan Taylor ambaye ni profesa wa kitivo cha Asili ya Ukristo na Hekalu la Pili la Wayahudi katika Chuo Kikuu cha King's College London na ndiye mwandishi wa kitabu kwa jina The Essenes, the Scrolls and the Dead Sea.
MUONEKANO WA NABII ISSA MIAKA HIYO ULIKUWAJE ? Karibu kila mtu ana dhana fulani kuhusu muonekano wa Yesu Kristo. Ndiye mtu aliyechorwa zaidi katika sanaa ya Magharibi. Picha zake hutambuliwa kwa urahisi, ambapo huoneshwa akiwa na nywele na ndevu, akiwa amevalia vazi lefu lenye mikono mirefu linalofanana na kanzu ( la rangi nyeupe), na pia akiwa amejifunga joho (la rangi ya samawati). Muonekano wa Yesu umefahamika sana na wengi kiasi kwamba unaweza kutambuliwa ukiwa hata kwenye mikate au biskuti. Picha za sasa za Yesu zinatokana na enzi ya Byzantine, himaya iliyokuwa na mji mkuu wake Constantinople. Ni picha iliyoanza kutumika karne ya nne hivi. Michoro ya Yesu ya wakati wa utawala wa Byzantine ilikuwa ya ishara, na si muonekano wake. Wasanii waliangazia zaidi maana na si kumfananisha na Yesu mwenyewe. Picha zao ziliongozwa na dhana ya Yesu kama mtawala, kwenye kiti cha enzi, kama anavyoonyeshwa kwenye mchoro ulio kwenye altari ya kanisa la Santa Pudenziana jijini Roma. Yesu anaoneshwa akiwa amevalia mgolole wa rangi ya dhahabu. Ndiye mtawala wa dunia yote aliyetoka mbinguni, mfanano wa picha yake ni ule wa sanamu ya Zeus wa Olympus anayeonyeshwa akiwa na nywele ndefu za ndevu kwenye kiti cha enzi. Ni sanamu iliyokuwa maarufu sana wakati huo kiasi kwamba Mfalme Augustus wa Roma alishurutisha naye atengenezewe sanamu kama hiyo, lakini yake ikiwa bila nywele ndefu na ndevu, Wasanii wa Byzantine, walitaka kumuonyesha Kristo kama mtawala kutoka mbinguni, mfalme wa aina yake, na hivyo wakachora wakimuonyesha kama Zeus, lakini akiwa mdogo kidogo wa umri. Kilichotokea kadiri miaka ilivyosonga ni kwamba kuonyeshwa huku kwa Kristo kama mtawala kutoka mbinguni - ambapo wakati mwingine ameonyeshwa hata akiwa kama 'hippie' au 'superstar' (kama ilivyo kwenye mchoro huu hapa chini) - ndiko kumekuwa kama kigezo chetu cha Yesu alivyokuwa. Hebu tuchanganue kutoka kichwani hadi vidole vya miguuni. Wakristo wa nyakati za kwanza wakati walipokuwa wanamwonyesha Kristo si kama mtawala kutoka mbinguni, walimuonyesha kama binadamu wa kawaida tu - akiwa hana ndevu na hana nywele ndefu. Lakini pengine, kama msomi wa aina yake aliyekuwa akisafiri kutoka eneo moja hadi jingine, Yesu pengine alikuwa na ndevu, kwa sababu hakuwa akienda kwa vinyozi. Kwa kawaida, kuwa mchafu kiasi na kuwa na ndevu ndefu ni sifa ambazo zilihusishwa na wanafalsafa, wasomi wa ngazi ya juu, na kuwatenganisha na watu wa kawaida. Mwanafalsafa maarufu wa kundi la Stoic (Wanafalsafa wa Kigiriki waliofuata mafundisho ya mwanzilishi wao Zeno wa Citium mjini Athens mapema karne ya 3 kabla ya kuzaliwa kwa Yesu) Epictetus aliamini "ilifaa hivyo kwa mujibu wa maumbile." Mambo yalibadilika katika karne ya 1 baada ya kuzaliwa kwa Yesu, wakati wa enzi za Warumi na Wagiriki, ambapo kuwa na nywele fupi na kunyoa ndefu ndiyo mambo yaliyochukuliwa kuwa yafaayo na ya kistaarabu. Kuwa na nywele ndefu na ndevu ni mambo ambayo yaliachiwa miungu pekee, si ya watu wa kawaida. Hata wanafalsafa enzi hizo walikuwa na nywele fupi. Ndevu pia hazikuwa sifa za kuwatambulisha Wayahudi enzi hizo. Ukweli ni kwamba moja ya changamoto ambazo waliotaka kuwatesa Wayahudi vipindi mbalimbali katika historia walihangaika sana kuwatofautisha na watu wengine. Hii ni kwa sababu wote walifanana (jambo ambalo limegusiwa katika kitabu cha Wamakabayo). Hata hivyo, picha za wanaume wa Kiyahudi zilizokuwa kwenye sarafu za Judea Capta ambazo zilitolewa na utawala wa Roma baada ya kutekwa kwa mji wa Yerusalemu mwaka 70 baada ya kuzaliwa kwa Yesu zinawaonesha wanaume wakiwa na ndevu, lakini nywele zao si ndefu. Kwa hivyo, Yesu, kama mwanafalsafa wa muonekano wa kawaida, kuna uwezekano alikuwa na ndevu lakini si ndefu sana, sawa na wanaume hao walioonyeshwa kwenye sarafu za Judaea Capta, lakini nywele zake basi hazikuwa ndefu sana pia. Kama ingetokea kwamba awe na nywele ndefu hata kidogo tu kuliko kawaida, basi angezua mtafaruku Wanaume wa Kiyahudi waliokuwa na ndevu ambazo hazikuwa zimetunzwa vyema na nywele ambazo zilikuwa ndefu kidogo kuliko kawaida walitambulika mara moja kama watu waliokuwa wamekula kiapo cha kuwa Wanazari (Nazarite). Hii ilikuwa na maana kwamba wangejitoa wakfu kwa Mungu kwa kipindi fulani, ambapo hawangekunywa vileo wala kuzikata nywele zao. Mwisho wa kipindi hicho, wangenyolewa nywele zao katika sherehe maalum hekaluni Jerusalem (kama inavyoelezwa katika kitabu cha Matendo ya Mitume, Sura ya 21, aya ya 24). Lakini Yesu hakuwa amekula kiapo cha kuwa Mnazari, kwa sababu mara nyingi tunamsikia kwenye Biblia akinywa divai - wakosoaji wake hata wakati mwingine wanamshutumu kwa kunywa divai sana, kupita kiasi (Matayo Sura ya 11, aya ya 19). Kama angekuwepo na nywele ndefu, na kuonekana kama Mnazari, tungelitarajia basi kuwepo na tamko pahala fulani kuhusu tofauti ya muonekano wake na matendo aliyokuwa akiyafanya ambayo hayakuendana na Unazari. Hali kwamba alikuwa akinywa divai yenyewe ingekuwa tatizo kubwa. Wakati Yesu alipoishi, matajiri walizoea kuvalia kanzu na majoyo ya vitambaa vya thamani, kuonyesha hadhi yao katika jamii. Katika moja ya mahubiri yake, Yesu anasema : "Jihadharini na walimu wa sheria (waandishi). Wao hupenda kutembea wakiwa wamevaa mavazi marefu (stolai), na kusalimiwa kwa heshima masokoni. Pia wao hupenda kukaa kwenye viti vya mbele katika masinagogi, na kupewa nafasi za heshima katika karamu." Mafundisho haya ya Yesu kwa kawaida huchukuliwa kama yenye maelezo ya kuaminika zaidi kwenye Injili, hivyo tunaweza kuwa na msingi kuamini kwamba Yesu hakuvalia mavazi kama hayo marefu. Kwa jumla, mwanamume wakati huo wa Yesu angevalia gwanda au kanzu fupi hivi, na mwanamke angevalia vazi lililomfika kwenye kifundo cha mguu. Kwa hivyo, katika karne ya 2 kwenye kitabu cha Matendo ya Mitume, Paul na Thecla, inapotokea kwamba Thecla ambaye ni mwanamke anavalia kanzu fupi kama mwanamume, hilo ni jambo linaloshangaza sana. Kanzu hizi kwa kawaida zingekuwa na ukanda au mstari wa rangi tofauti kutoka kwenye bega hadi kwenye pindo sehemu ya chini. Ni vazi ambalo lingeshonwa au kufumwa kama kipande kimoja cha vazi. Juu ya kanzu hiyo, ungejifunga joho au vazi jingine la nje, na tunajua kwamba Yesu alivalia vazi kama hilo kwa sababu ndilo lililoguswa na mwanamke aliyetaka kuponywa naye. (Marko 5:27): Alikuwa amesikia habari za Yesu, naye akaja kwa nyuma yake kwenye umati wa watu, akaligusa vazi lake, kwa maana alisema moyoni mwake, 'Kama nikiweza kuligusa vazi lake tu, nitaponywa.') Vazi hilo la nje lilifumwa kwa manyoya, lakini halikuwa zito sana na ndipo ili uhisi joto ingemlazimu mtu kuvalia mavazi mawili kama hayo. Vazi hilo lingevaliwa kwa njia nyingi, na wakati mwingine lingening'inia hadi chini ya magoti na kulifunika lile kanzu fupi la ndani. (Baadhi ya wanafalsafa walizoea kuvalia vazi hilo la nje pekee bila kuvalia ile kanzu ya ndani na kuacha sehemu ya bega au kifua ikiwa wazi). Mamlaka na hadhi ya mtu ni vitu ambavyo vilidhihirishwa kupitia ubora, ukubwa na rangi ya mavazi hayo ya nje. Rangi ya zambarau na baadhi ya aina za rangi ya buluu (samawati) ni rangi zilizoashiria utajiri, hadhi na kujionea fahari. Zilikuwa ni rangi za kifahari kwa sababu viungo vya kutengeneza rangi hizo vilikuwa adimu na ghali sana. Lakini rangi pia huashiria kitu kingine tofauti. Mwanahistoria Josephus, anawaeleza walokole waliofahamika kama Zealots (kundi la Wayahudi wa itikadi kali waliotaka kuwafurusha Warumi kutoka Judea) kama kundi la wahalifu wauaji waliovalia mavazi ya nje yaliyopakwa rangi kwa jina - mavazi anayoyaita chlanidia - kuashiria kwamba yalikuwa ni kama mavazi yaliyovaliwa na wanawake. Hii inaashiria kwamba wanaume kamili, kama hawakuwa na cheo cha juu zaidi katika jamii, walifaa kuvalia mavazi yasiyopakwa rangi. Yesu hakuvalia mavazi meupe hata hivyo. Haya yalikuwa mavazi ya kipekee na yalihitaji kupaushwa mara kwa mara (kufanywa meupe tena) au kupakwa chokaa. Judea, mavazi kama hayo meupe yalihusishwa na kundi lililofahamika kama Essenes - ambao ni watu waliofuata ufasiri mkali wa sheria za Kiyahudi. Tofauti kati ya mavazi ya Yesu na mavazi mengine ya rangi nyeupe ya kung'aa inaelezwa kwenye sura ya 9 ya Marko ambapo anaandamana na mitume watatu mlimani. Yesu aliwachukua "Petro, Yakobo na Yohana, akawapeleka juu ya mlima mrefu, mahali walipokuwa faraghani. Huko, Yesu akageuka sura mbele yao. Mavazi yake yakawa na weupe wa kuzima macho, meupe kuliko ambavyo mtu yeyote duniani angaliweza kuyangʼarisha. Mose na Eliya wakawatokea, wakawa wanazungumza na Yesu." Marko anaeleza kwamba mavazi ya Yesu yaligeuka rangi yakawa meupe sana, hapa anarejelea vazi la ndani na si la nje. Kabla ya kugeuka sura huku kwa Yesu, anaoneshwa na Marko kama mwanamume wa kawaida, aliyevalia mavazi ya kawaida, ambayo ni ya rangi ambayo haijapaushwa. Katika hali ambayo ndipo yang'ae na kuangaza unahitaji kumpelekea fundi. Tunaelezwa zaidi kuhusu mavazi ya Yesu wakati wa kusulubiwa kwake, pale wanajeshi wa Kirumi wanapoyakata mavazi yake ya nje vipande vinne (Yohana19:23: Askari walipokwisha kumsulubisha Yesu, walichukua nguo zake wakazigawa mafungu manne, kila askari fungu lake. Ila walikubaliana wasilichane lile vazi lake kwa maana lilikuwa halina mshono bali limefumwa tangu juu hadi chini.) Kuna uwezekano mavazi hayo ya nje yalikuwa mavazi mawili. Moja ya vazi hili huenda lilikuwa ni tallith, ambalo ni vazi la kujifunga Kiyahudi wakati wa maombi. Vazi hili lenye shada (tzitzith) limetajwa moja kwa moja na Yesu katika kitabu cha Mathayo 23:5 anapozungumza kuhusu walimu wa sheria na Mafarisayo (Wao hutenda mambo yao yote ili waonekane na watu. Hupanua vikasha vyao vyenye maandiko ya sheria na kurefusha matamvua ya mavazi yao). Lilikuwa ni vazi la nje lisilo zito, ambalo kawaida lilitengenezwa kwa kitambaa cha manyoya na lilikuwa la rangi ya malai hivi (krimu), na pengine lilikuwa na ukanda au mstari wa rangi ya nili (bluu iliyoiva). Miguuni, Yesu angevalia ndara (kandambili au malapa). Kila mtu wakati huo alivalia ndara. Katika mapango yaliyo jangwani karibu na Bahari ya Chumvi (Bahari Mfu) na Masada, ndara za wakati alipoishi Yesu zimegunduliwa, na tunaweza kutazama ndara ambazo huenda alivaa zilivyoonekana. Zilikuwa hazijafanyiwa kazi nyingi sana ya kiufundi. Soli (nyayo au kikanyagio) zake zilikuwa vipande vigumu vya ngozi vilivyoshonwa pamoja, na juu kulikuwa ni kanda za ngozi ambazo mbele zingeingizwa katikati ya vidole, kama malapa tu ya siku hizi. Yesu (Nabii Issa) Alikuwa Myahudi, na uso wake pia bila shaka ungefanana na Wayahudi wa wakati huo. Hali kwamba Yesu alikuwa Myahudi (au Mjudea) ni jambo linalorejelewa katika vitabu vingi, zikiwemo barua za Mtume Paulo. Na katika barua yake kwa Waebrania, anaandika: "Kwa maana ni dhahiri kwamba Bwana wetu alitoka katika uzao wa Yuda" (Sura ya 7:14) Kwa hivyo, Myahudi wa wakati huo, mwanamume wa miaka 30 hivi alipoanza kueneza Injili kwa mujibu wa Luka 3, pia akiwa ni mwenye ngozi nyeusi kama ilivyokuwa kwa wayahudi wengi zama zile waliokuwa wakitembeleana na ndugu zao wa Misri (Kushi) kemet. Mwaka 2001 mwanaantholopojia (mtaalamu wa elimu ya binadamu hasa elimu ihusuyo habari zinazohusu asili na maendeleo yake ya awali) Richard Neave alitengeneza mfano wa mwanamume wa Galilaya wa zama za Yesu ambao ulitumiwa kwa jina Son of God (Mwana wa Mungu). Alitumia fuvu lililopatikana katika eneo hilo. Hakusema kwamba huo ulikuwa muonekano wa uso wa Yesu. Mfano ulikuwa tu wa kuchochea hisia na kuwafanya watu kumfikiria Yesu kama mwanamume wa zama hizo na eneo hilo, kwa sababu hakuna mchoro wala maelezo yaliyopo ya kina kuhusu muonekano wake halisi. Ingawa tunaweza kupata viashiria kutoka kwa teknolojia na kutumia mifupa ya watu wa kale, kiashiria cha karibu sana kuhusu pengine Yesu alionekana vipi labda kinaweza kutokana na mchoro wa Musa kwenye ukuta wa sinagogi ya karne ya 3 ya Dura-Europos, kwani mchoro huo unaonesha jinsi Myahudi wa hekima alidhaniwa kuwa wakati wa utawala wa Wagiriki na Warumi. Musa anaoneshwa akiwa na mavazi ambayo hayajapaushwa, na moja ya vazi lake la nje ni tallith. Katika mchoro huo wa Dura wa Musa akitenganisha maji kwenye Bahari ya Sham ili Waisraeli wapite, unaweza kuziona shada (tzitzith) kwenye kona za vazi hilo. Kwa kiwango kikubwa, picha hiyo pengine inatoa msingi bora zaidi wa kumfikiria Yesu alivyokuwa badala ya picha za sasa zinazoongozwa na busara na mawazo ya enzi ya Byzantine - alikuwa na nywele fupi, ndevu fupi, na alikuwa amevalia kanzu fupi lenye mikono mifupi, na alikuwa na joho au vazi la nje. Makala hii chimbuko lake ni makala ya Kiingereza ya Joan Taylor ambaye ni profesa wa kitivo cha Asili ya Ukristo na Hekalu la Pili la Wayahudi katika Chuo Kikuu cha King's College London na ndiye mwandishi wa kitabu kwa jina The Essenes, the Scrolls and the Dead Sea.
·47 Visualizações