Upgrade to Pro

MANSA MUSA
.
Mansa Musa alizaliwa 1280 katika familia ya watawala. Nduguye , Mansa Abu-Bakr, alitawala ufamle huo hadi 1312, wakati alipoamua kwenda safari. Kulingana na mwanahistoria wa karne ya 14 Shibab al-Umari, Abu-Bakr alipendelea sana kuiona bahari ya Atlantic na kile ilichokuwa nacho. Aliripotiwa kuanza safari na msafara wa meli 2000 na maelfu ya wanaume na wanawake pamoja na watumwa. Walienda na hawakurudi tena. Wengine kama vile mwanahistoria wa Marekani Ivan Van Sertima anadai kwamba waliwasili Marekani Kusini. Lakini hakuna ushahidi. Ukweli ni kwamba Mansa Musa alirithi ufalme ulioachwa nyuma na nduguye. Chini ya uongozi wake ufalme wa Mali uliimarika kwa kiwango kikubwa.
Watag marafk zako waje wapate kufahamu mengi wasiyo yajua kuhusu Mansa Musa pia isisahau ku follow hawa watu.
.
.
.
Mfalme huyo aliripotiwa kuondoka Mali na msafara wa watu 60,000. Alibeba ufalme wake wote na maafisa wake , wanajeshi, watumbuizaji , madereva wa ngamia na watumwa 12,000 mbali na idadi kubwa ya mbuzi , kondoo na chakula. Ulikuwa mji uliokuwa ukipitia katika jangwa. Mji ambao wakaazi wake hadi watumwa wake walikuwa wamevalia dhahabu na nguo za hariri. Kulikuwa na ngamia 100 ambao kila mmojawao alikuwa akibeba mamia ya pauni za dhahabu. Utajiri huo ulionekana zaidi wakati msafara huo ulipowasili mjini Cairo ambapo ulionekana.
.
.
Kampuni ya kiteknolojia ya Marekani SmartAsset.com inakadiria kwamba kutokana na kuanguka kwa bei ya dhahabu, Hija ya Mansa Musa ilisababisha hasara ya $1.5bn (£1.1bn) katika uchumi wa eneo la mashariki ya kati. Alipokuwa akirudi nyumbani, Mansa Musa alpitia tena Misri na kulingana wachache akajaribu kusaidia uchumi wa taifa hilo kwa kuondoa dhahabu iliokuwepo kupitia kuiomba kwa kiwango cha juu kutoka kwa wafanyibiashara wa Misri. Wengine wanasema kuwa aligharamika sana hadi dhahabu alizokuwa nazo zikaisha. Lucy Duran wa Shule ya African and Oriental Studies mjini London anasema kwamba wanahistoria wa Mali walikasirishwa naye. ''Alitoa dhahabu nyingi ya Mali hali ambayo iliwafanya wanahistoria hao kutomsifu katika nyimbo zao na hadithi kwa kuwa wanaona kwamba alipoteza mali nyingi ya taifa hilo nje ya ufalme wake'', alisema.


.
SHUKRANI
MANSA MUSA . Mansa Musa alizaliwa 1280 katika familia ya watawala. Nduguye , Mansa Abu-Bakr, alitawala ufamle huo hadi 1312, wakati alipoamua kwenda safari. Kulingana na mwanahistoria wa karne ya 14 Shibab al-Umari, Abu-Bakr alipendelea sana kuiona bahari ya Atlantic na kile ilichokuwa nacho. Aliripotiwa kuanza safari na msafara wa meli 2000 na maelfu ya wanaume na wanawake pamoja na watumwa. Walienda na hawakurudi tena. Wengine kama vile mwanahistoria wa Marekani Ivan Van Sertima anadai kwamba waliwasili Marekani Kusini. Lakini hakuna ushahidi. Ukweli ni kwamba Mansa Musa alirithi ufalme ulioachwa nyuma na nduguye. Chini ya uongozi wake ufalme wa Mali uliimarika kwa kiwango kikubwa. Watag marafk zako waje wapate kufahamu mengi wasiyo yajua kuhusu Mansa Musa pia isisahau ku follow hawa watu. . . . Mfalme huyo aliripotiwa kuondoka Mali na msafara wa watu 60,000. Alibeba ufalme wake wote na maafisa wake , wanajeshi, watumbuizaji , madereva wa ngamia na watumwa 12,000 mbali na idadi kubwa ya mbuzi , kondoo na chakula. Ulikuwa mji uliokuwa ukipitia katika jangwa. Mji ambao wakaazi wake hadi watumwa wake walikuwa wamevalia dhahabu na nguo za hariri. Kulikuwa na ngamia 100 ambao kila mmojawao alikuwa akibeba mamia ya pauni za dhahabu. Utajiri huo ulionekana zaidi wakati msafara huo ulipowasili mjini Cairo ambapo ulionekana. . . Kampuni ya kiteknolojia ya Marekani SmartAsset.com inakadiria kwamba kutokana na kuanguka kwa bei ya dhahabu, Hija ya Mansa Musa ilisababisha hasara ya $1.5bn (£1.1bn) katika uchumi wa eneo la mashariki ya kati. Alipokuwa akirudi nyumbani, Mansa Musa alpitia tena Misri na kulingana wachache akajaribu kusaidia uchumi wa taifa hilo kwa kuondoa dhahabu iliokuwepo kupitia kuiomba kwa kiwango cha juu kutoka kwa wafanyibiashara wa Misri. Wengine wanasema kuwa aligharamika sana hadi dhahabu alizokuwa nazo zikaisha. Lucy Duran wa Shule ya African and Oriental Studies mjini London anasema kwamba wanahistoria wa Mali walikasirishwa naye. ''Alitoa dhahabu nyingi ya Mali hali ambayo iliwafanya wanahistoria hao kutomsifu katika nyimbo zao na hadithi kwa kuwa wanaona kwamba alipoteza mali nyingi ya taifa hilo nje ya ufalme wake'', alisema. . SHUKRANI 🙏🙏🙏🙏🙏
Like
1
·31 Ansichten