TARABUSHI - KOFIA ZA KIHISTORIA.
Leo hii ni aghalabu sana kukutana na mtu aliyevaa tarabushi kutokana na kutoweka kwa kofia hizi. Ni watu wachache sana wenye nazo, hususani wazee au wenye umri wa makamo, kwa kutaja wachache ni mbunge wa Musoma vijijini, Mh. Nimrod Mkono, na msanii wa maigizo, marehemu 'mzee small.
Hizi ni kofia zenye rangi hasa nyekundu zikiwa na shada ya nyuzi nyeusi. Kwa kingereza zikijulikana kama 'Fez', kwa kiarabu 'Tarboosh' huku waswahili tukiita Tarabushi. Katika kuelezea historia ya Tarabushi, yanipasa kurudi miaka mia mbili iliyopita, pale ambapo Sultan Mahmud II wa dola ya Ottoman alipotangaza kofia za Fez/tarabushi kutumika kama vazi rasmi la dola hiyo. Sultani alifanya hivyo kufuatia kampeni yake ya kuboresha 'empire' ambapo alitamani watu wa Ottoman kuwa na utambulisho wao utakaowatofautisha na watu wengine.
Kufuatia kampeni hiyo, tarabushi zilipata umaarufu mkubwa ndani na nje ya Ottoman ambapo watu wengi walianza kuvaa. Mwaka 1829, Mfalme Mahmud II alipitisha sheria kwamba tarabushi zianze kutumika katika jeshi lake, hivyo kwanzia siku hiyo tuliona wanajeshi wa Ottoman Empire wakienda kwenye uwanja wa vita wakiwa wamevaa tarabushi.
Kabla ya wazo la kutumia Tarabushi, Sultani Mahmud II alichagua aina fulani ya kofia zenye asili ya Uingereza ambazo zina umbo la pembe tatu. Lakini watu wake wa karibu walimshauri kutotumia kofia hizo, kwasababu waliona hiyo pembe tatu humaanisha 'utatu mtakatifu' hivyo isingeleta tafsiri nzuri kwa watu wa Ottoman ambao asilimia kubwa ni waislamu. Wakristo huamini katika "utatu mtakatifu" yaani Mungu, Mwana na Roho mtakatifu.
Wakati Sultani anaendelea kuwaza mbadala wa kofia, ikatokea siku mabaharia wa Ottoman walikuwa wanarudi kutoka Morroco. Kichwani wakiwa wamevaa kofia nyekundu zenye shada ya nyuzi nyeusi. Sultani akavutiwa na kofia hizo na hapo ndio chanzo cha kuzichagua kutumika kama utamaduni wa Ottoman Empire. Morroco ndipo zilipokuwa zinatengenezwa kwa wingi kwasababu rangi ya kutengeneza kofia hizo ilikuwa inatokana na matunda fulani ambayo yalistawi kwa wingi hapo Morroco katika mji wa Fez. Ndio maana hata jina la kofia hizo 'Fez', limetokana na mji huo ambao hadi mwaka 1912 ndio ulikuwa mji mkuu wa Morroco.
Umaarufu wa kofia hizi uliendelea kutapakaa kote ulimwenguni, ukizingatia kwamba dola ya Ottoman ilikuwa ni dola kubwa iliyoenea sehemu nyingi. Hivyo baadhi ya nchi zikaanza kutumia kofia hizi hususani katika majeshi yao-mfano Cyprus, Ugiriki, Albania. Pia India, Misri, Ufaransa n.k.
Kwa huku kwetu Afrika Mashariki, umaarufu wa kofia hizi ulikuja baada ya ujio wa ukoloni. Hiyo ni kutokana na ukweli kwamba katika kipindi cha Uingereza, waAfrika walijumuishwa katika jeshi la kikoloni ambalo lilikuja kuitwa 'King's African Rifles KAR' wakivaa sare za rangi ya khaki na kichwani walivaa Fez/ tarabushi. Jeshi hili lilianzishwa mwaka 1902 huko Kenya na baadae kuenea katika nchi zingine za Afrika Mashariki na hata kujumuishwa kwenye vita ya kwanza ya Dunia mwaka 1914.
Pia katika makoloni ya Ujerumani, Tanganyika ikiwemo, kuliundwa jeshi la kikoloni 'Schutztruppe' ambapo waAfrika wengi walijumuishwa humo na kuwa Askari wa kikoloni 'Polizei-Askari', ambao sare zao zilikuwa za rangi ya khaki pamoja na kofia za tarabushi.
Umaarufu wa kofia hizi za ulikuja kupungua mara baada kuanguka kwa dola ya Ottoman na kuzaliwa kwa nchi ya Uturuki ambapo mwaka 1925 Rais wa kwanza wa Uturuki bwana *Mustapha Kemal Artatuk,* alipiga marufuku kofia hizo. Hiyo ni katika hatua ya kuanzisha Uturuki mpya isiyo na mabaki ya kisultani. Pia huko Misri, mwaka 1956 Mara baada ya Gamer Abdel Nasser kumpindua mfalme, alipiga marufuku kofia za Tarboosh.
Pia hata huku kwetu Afrika Mashariki, muda mfupi kidogo baada ya kupata uhuru, serikali ziliamua kubadilisha sare za majeshi yetu ambapo kofia zingine zilianza kutumika badala ya Tarabushi ambazo zilionekana ni kama za kikoloni. Na huo ndio ukawa mwanzo wa kupotea kwa kofia za Tarabushi japokuwa kuna baadhi ya watu waliendelea kubaki nazo.

·18 Views