Mise à niveau vers Pro

MBWA ALIYEZIKWA NACHINGWEA 1950

Na Victor Richard..

Judy ni mbwa jike aliyeishi kati ya mwaka 1936 hadi Februari 17, 1950. Mbwa huyu alikuwa
akiishi melini katika meli za HMS Gnat na HMS Grasshopper ambazo zilitia nanga huko Yangtze kabla na wakati wa vita kuu ya pili ya Dunia.

Alidhihirisha uwezo wake wa kusikia ndege za maadui zilizokuwa zikiwajia na kutoa ishara kwa wanamaji waliokuwapo.
Baada ya baadhi ya wanamaji kuhamishwa kutoka meli ya Gnat na kupelekwa katika meli ya Grasshopper mwaka 1939,meli ilipelekwa Singapore na hii ni baada ya Uingereza kuamua kuingia vitani dhidi ya Ujerumani.

Judy alikuwa melini wakati wa mapambano ya Singapore ambapo alikuwapo pia wakati Grasshopper ikiwahamisha wanamaji wake kuelekea Dutch East Indies lakini ikiwa njiani meli hiyo ilizama na Judy alikaribia kupoteza maisha kutokana na kunaswa na mlolongo wa makabati yaliyoanguka, hata hivyo aliokolewa na wanamaji waliorudi melini wakitafuta masalia.

Katika kisiwa hicho kikame akiwa na wanamaji waliosalimika,Judy aliweza kutafuta vyanzo
vya maji safi vilivyowasaidia wote. Baadae walifanya safari kuelekea Singkep,Dutch East India na kisha Sumatra kwa lengo la kutengeneza namna ya kuyaokoa majeshi ya Uingereza.

Baada ya safari ngumu iliyokatisha maili 200 za pori kwa wiki tano wakati ambapo pia Judy alinusurika kuuawa na mamba, wanamaji waliwasili siku moja baada ya meli ya mwisho kuondoka na hivyo kuangukia kwenye mikono ya wajapani na kufanywa wafungwa wa kivita, Judy akiwa miongoni mwa wafungwa hao.

Judy alihamishwa kinyemela na kupelekwa kambi ya Medan ambako alikutana kwa mara ya kwanza na kiongozi mwandamizi wa Jeshi la anga anayeitwa Frank Williams ambaye aliishi naye kwa kipindi chote kilichosalia cha maisha yake.

Williams alimshawishi Kamanda wa kikosi kumsajili Judy kama mfungwa wa kivita akipatiwa namba ‘81A Gloergoer Medan’.Judy alikuwa ni mbwa pekee aliyesajiliwa kama mfungwa wa kivita katika Vita kuu ya pili ya Dunia.

Judy alizunguuka katika kambi kadhaa,akisalimika/nusulika kifo baada ya meli ya mizigo ya SS Van Warwyck kuzama ambapo kipindi kifupi baadae aliweza kuwaokoa abiria katika meli iliyokuwa ikizama.

Les Searly kutoka katika meli ya Grasshopper ilimuiba tena Judy na kumpeleka katika kambi nyingine ambako aliungana tena na Frank Williams.

Baada ya Vita ya pili ya Dunia kuisha,maisha ya Judy yalikuwa hatarini kwa mara nyingine..........

MBWA ALIYEZIKWA NACHINGWEA 1950 Na Victor Richard.. Judy ni mbwa jike aliyeishi kati ya mwaka 1936 hadi Februari 17, 1950. Mbwa huyu alikuwa akiishi melini katika meli za HMS Gnat na HMS Grasshopper ambazo zilitia nanga huko Yangtze kabla na wakati wa vita kuu ya pili ya Dunia. Alidhihirisha uwezo wake wa kusikia ndege za maadui zilizokuwa zikiwajia na kutoa ishara kwa wanamaji waliokuwapo. Baada ya baadhi ya wanamaji kuhamishwa kutoka meli ya Gnat na kupelekwa katika meli ya Grasshopper mwaka 1939,meli ilipelekwa Singapore na hii ni baada ya Uingereza kuamua kuingia vitani dhidi ya Ujerumani. Judy alikuwa melini wakati wa mapambano ya Singapore ambapo alikuwapo pia wakati Grasshopper ikiwahamisha wanamaji wake kuelekea Dutch East Indies lakini ikiwa njiani meli hiyo ilizama na Judy alikaribia kupoteza maisha kutokana na kunaswa na mlolongo wa makabati yaliyoanguka, hata hivyo aliokolewa na wanamaji waliorudi melini wakitafuta masalia. Katika kisiwa hicho kikame akiwa na wanamaji waliosalimika,Judy aliweza kutafuta vyanzo vya maji safi vilivyowasaidia wote. Baadae walifanya safari kuelekea Singkep,Dutch East India na kisha Sumatra kwa lengo la kutengeneza namna ya kuyaokoa majeshi ya Uingereza. Baada ya safari ngumu iliyokatisha maili 200 za pori kwa wiki tano wakati ambapo pia Judy alinusurika kuuawa na mamba, wanamaji waliwasili siku moja baada ya meli ya mwisho kuondoka na hivyo kuangukia kwenye mikono ya wajapani na kufanywa wafungwa wa kivita, Judy akiwa miongoni mwa wafungwa hao. Judy alihamishwa kinyemela na kupelekwa kambi ya Medan ambako alikutana kwa mara ya kwanza na kiongozi mwandamizi wa Jeshi la anga anayeitwa Frank Williams ambaye aliishi naye kwa kipindi chote kilichosalia cha maisha yake. Williams alimshawishi Kamanda wa kikosi kumsajili Judy kama mfungwa wa kivita akipatiwa namba ‘81A Gloergoer Medan’.Judy alikuwa ni mbwa pekee aliyesajiliwa kama mfungwa wa kivita katika Vita kuu ya pili ya Dunia. Judy alizunguuka katika kambi kadhaa,akisalimika/nusulika kifo baada ya meli ya mizigo ya SS Van Warwyck kuzama ambapo kipindi kifupi baadae aliweza kuwaokoa abiria katika meli iliyokuwa ikizama. Les Searly kutoka katika meli ya Grasshopper ilimuiba tena Judy na kumpeleka katika kambi nyingine ambako aliungana tena na Frank Williams. Baada ya Vita ya pili ya Dunia kuisha,maisha ya Judy yalikuwa hatarini kwa mara nyingine..........
Like
Wow
2
·27 Vue