Обновить до Про

Escobares, mji uliyo masikini nchini Marekani.
Mji wa Escobares katika mpaka Mexico na Marekani haujawahi kuorodheshwa kama moja ya miji masikini zaidi nchini Marekani lakini wakaazi wake wanaishi chini ya dola moja kwa siku.

Kwa mujibu wa shirika la kukadiria idadi ya watu, 62.4% ya wakaazi 2,512 wa mji huo wanaishi chini ya dola moja kwa siku.

"Wakati mwingine nakosa chakula hadi nasaidiwa na jamaa zangu," anasema Debora Hernández, raia wa Marekani aliyezaliwa na kulelewa katika mji huo wa mpakani.

Mji wa Escobares uko mbali na miji iliyo na shughuli nyingi za kiuchumi na wakaazi hawana njia nyingine ya kujikimu kimaisha.
Watu wanaoishi maeneo ya kusini mwa Marekani wanakabiliwa na viwango vya juu vya umasikini,"Rakesh Kochhar, mtafiti katika kituo cha utafiti cha Pew mjini Washington, aliiambia BBC.

Kituo hicho kinasema kiwango cha umasikini nchini Marekani kimefikia 12.3%, na takriban watu milioni 40 wameathiriwa.

Watu masikini zaidi nchini Marekani wanaishi miji ya Mississippi, Louisiana na New Mexico, wengi wao ni watu wa asili ya "Uhispania na Waafrika ambao katika historia ya nchi hiyo wamekabiliwa na umasikini kwa muda mrefu,"anasema mtafiti, Rakesh Kochhar.
watu wa Escobares wanaishi ndani ya mabogi ya treni au trela ambayo yameguzwa kuwa nyumba ambayo yanawezwa kuhamishwa kutoka sehemu moja hadi nyingine.
Wapo watu wengi wanafikiria marekani maisha ni mazuri je ungependa kuishi marekani katika mji huu!?nakaribisha maoni.
®jbgw.
Escobares, mji uliyo masikini nchini Marekani. Mji wa Escobares katika mpaka Mexico na Marekani haujawahi kuorodheshwa kama moja ya miji masikini zaidi nchini Marekani lakini wakaazi wake wanaishi chini ya dola moja kwa siku. Kwa mujibu wa shirika la kukadiria idadi ya watu, 62.4% ya wakaazi 2,512 wa mji huo wanaishi chini ya dola moja kwa siku. "Wakati mwingine nakosa chakula hadi nasaidiwa na jamaa zangu," anasema Debora Hernández, raia wa Marekani aliyezaliwa na kulelewa katika mji huo wa mpakani. Mji wa Escobares uko mbali na miji iliyo na shughuli nyingi za kiuchumi na wakaazi hawana njia nyingine ya kujikimu kimaisha. Watu wanaoishi maeneo ya kusini mwa Marekani wanakabiliwa na viwango vya juu vya umasikini,"Rakesh Kochhar, mtafiti katika kituo cha utafiti cha Pew mjini Washington, aliiambia BBC. Kituo hicho kinasema kiwango cha umasikini nchini Marekani kimefikia 12.3%, na takriban watu milioni 40 wameathiriwa. Watu masikini zaidi nchini Marekani wanaishi miji ya Mississippi, Louisiana na New Mexico, wengi wao ni watu wa asili ya "Uhispania na Waafrika ambao katika historia ya nchi hiyo wamekabiliwa na umasikini kwa muda mrefu,"anasema mtafiti, Rakesh Kochhar. watu wa Escobares wanaishi ndani ya mabogi ya treni au trela ambayo yameguzwa kuwa nyumba ambayo yanawezwa kuhamishwa kutoka sehemu moja hadi nyingine. Wapo watu wengi wanafikiria marekani maisha ni mazuri je ungependa kuishi marekani katika mji huu!?nakaribisha maoni. ®jbgw.
·40 Просмотры