Watu 20 wauawa katika shambulio dhidi ya ikulu ya Chad
Watu 20 wameuawa na wengine 11 kujeruhiwa katika shambulio dhidi ya ikulu ya Chad lililotokea jumatano jioni.
Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Mwendesha Mashtaka nchini humo imesema, shambulio hilo lilitokea majira ya saa 1:45 jioni kwa saa za huko ambapo kundi la watu 24 waliokuwa na silaha walidai kuharibikiwa na gari na kuwashambulia walinzi katika mlango mkuu wa Ikulu.
Wakati wa shambulio hilo, washambulizi hao waliwaua askari wawili na kujeruhi vibaya askari wengine watano huku wakijaribu kuingia kwa nguvu ndani ya Ikulu. Hata hivyo vikosi vya usalama vilijibu shambulio hilo haraka na kuwaua washambuliaji 18, huku washambuliaji wengine 6 waliojeruhiwa walikamatwa na kupelekwa hospitali kwa ajili ya kupatiwa matibabu.

·37 Visualizações