Upgrade to Pro

"Habari za Asubuhi wana Simba

Baada ya jana kupokea hukumu ya CAF kuhusu kufungiwa Mashabiki katika mchezo wetu dhidi Costantine kumekua na mawazo na maoni mengi.

Wapo wanaosema tiketi ziendelee kuuzwa ili Wana Simba tuchangie faini iliyotozwa klabu yetu

Wapo wanaosema klabu iandae utaratibu maalumu watu wachangie kuipunguzia klabu mzigo wa adhabu ya faini hiyo

Na wengi wamesisitiza iandaliwe sehemu maalumu Wana Simba tukutane tuangalie kwa pamoja mechi

Kwanza niseme nimefurahishwa na fikra za Wana Simba kulichukua hili kuwa tatizo letu sote na tuko tayari kulitatua kwa pamoja

Pili niwaombe Wana Simba tutulie wakati huu ambao Viongozi wetu wakiangalia namna sahihi ya kuliendea jambo hili

Tatu niwatoe hofu Wana Simba kuwa adhabu yetu inahusu mechi moja tuu ya Jumapili, Robo Fainali tutaendelea na utaratibu wetu kama kawaida wa kwenda Uwanjani

Nichukue nafasi hii kuwapa pole Wana Simba wote ambao tumeumizwa na kadhia hii iliyotokea kwa mara ya kwanza katika maisha yetu

Mwisho kabisa ili kuepuka kupata maumivu kama haya ya kukosa kuiona Live timu yetu ikicheza mchezo muhimu kama huu hatuna budi sisi Mashabiki kujifunza kupitia sakata ili lisijirudie tena

Nguvu Moja - Ubaya Ubwela" - Ahmed Ally, Msemaji wa klabu ya Simba SC.

"Habari za Asubuhi wana Simba Baada ya jana kupokea hukumu ya CAF kuhusu kufungiwa Mashabiki katika mchezo wetu dhidi Costantine kumekua na mawazo na maoni mengi. Wapo wanaosema tiketi ziendelee kuuzwa ili Wana Simba tuchangie faini iliyotozwa klabu yetu Wapo wanaosema klabu iandae utaratibu maalumu watu wachangie kuipunguzia klabu mzigo wa adhabu ya faini hiyo Na wengi wamesisitiza iandaliwe sehemu maalumu Wana Simba tukutane tuangalie kwa pamoja mechi Kwanza niseme nimefurahishwa na fikra za Wana Simba kulichukua hili kuwa tatizo letu sote na tuko tayari kulitatua kwa pamoja Pili niwaombe Wana Simba tutulie wakati huu ambao Viongozi wetu wakiangalia namna sahihi ya kuliendea jambo hili Tatu niwatoe hofu Wana Simba kuwa adhabu yetu inahusu mechi moja tuu ya Jumapili, Robo Fainali tutaendelea na utaratibu wetu kama kawaida wa kwenda Uwanjani Nichukue nafasi hii kuwapa pole Wana Simba wote ambao tumeumizwa na kadhia hii iliyotokea kwa mara ya kwanza katika maisha yetu Mwisho kabisa ili kuepuka kupata maumivu kama haya ya kukosa kuiona Live timu yetu ikicheza mchezo muhimu kama huu hatuna budi sisi Mashabiki kujifunza kupitia sakata ili lisijirudie tena Nguvu Moja - Ubaya Ubwela" - Ahmed Ally, Msemaji wa klabu ya Simba SC.
Like
1
·70 Ansichten