ترقية الحساب

Kadiri siku ya mwisho ya amri ya kupiga marufuku au kuuzwa kwa TikTok inavyokaribia Januari 19, 2025, Watumiaji wengi wa TikTok kutoka Marekani wamehamia kwenye Xiaohongshu, jukwaa maarufu la miandao wa kijamii la Kichina.

Hii inakuja baada ya amri inayotaka kampuni mama ya TikTok, ByteDance, kuuza biashara yake ya Marekani au kukabiliwa na kupigwa marufuku kutokana na wasiwasi wa usalama wa kitaifa.

Watumiaji wengi wa TikTok wanapigania marufuku hiyo kwa kuhamia Xiaohongshu, na kuitwa wakimbizi wa TikTok. Hali iliyopeleka pelekea Xiaohongshu kupanda kwenye orodha ya programu zinazopakuliwa zaidi.

Hata hivyo, baadhi ya Wanaharakati wa Kichina wanakosoa hatua hii, wakisema inapuuzia mbali mateso halisi ya Watu chini ya utawala wa China. Kwa upande mwingine, mamlaka za China zinaona hili kama fursa ya kupanua ushawishi wao duniani, na Xiaohongshu inaboresha zana za tafsiri ili kuwezesha mawasiliano na Watumiaji wa kimataifa.

Kadiri siku ya mwisho ya amri ya kupiga marufuku au kuuzwa kwa TikTok inavyokaribia Januari 19, 2025, Watumiaji wengi wa TikTok kutoka Marekani wamehamia kwenye Xiaohongshu, jukwaa maarufu la miandao wa kijamii la Kichina. Hii inakuja baada ya amri inayotaka kampuni mama ya TikTok, ByteDance, kuuza biashara yake ya Marekani au kukabiliwa na kupigwa marufuku kutokana na wasiwasi wa usalama wa kitaifa. Watumiaji wengi wa TikTok wanapigania marufuku hiyo kwa kuhamia Xiaohongshu, na kuitwa wakimbizi wa TikTok. Hali iliyopeleka pelekea Xiaohongshu kupanda kwenye orodha ya programu zinazopakuliwa zaidi. Hata hivyo, baadhi ya Wanaharakati wa Kichina wanakosoa hatua hii, wakisema inapuuzia mbali mateso halisi ya Watu chini ya utawala wa China. Kwa upande mwingine, mamlaka za China zinaona hili kama fursa ya kupanua ushawishi wao duniani, na Xiaohongshu inaboresha zana za tafsiri ili kuwezesha mawasiliano na Watumiaji wa kimataifa.
·36 مشاهدة