Upgrade to Pro

Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu amesema Israel ina haki ya kuanza tena mapigano na Hamas kwa njia mpya na kwa nguvu mpya kama ikihitajika, iwapo mazungumzo zaidi ya kusitisha mapigano yatavunjika.

Makubaliano ya kusitisha mapigano na Hamas, yanatarajiwa kuanza kutekelezwa Jumapili asubuhi kwa saa za huko.

Netanyahu amebainisha kuwa marais wawili wa Marekani, Joe Biden anayemaliza muda wake na anayetarajiwa kuingia madarakani, Donald Trump, wanaiunga mkono Israel kurejea kupigana, iwapo mazungumzo ya awamu ya pili ya makubaliano yatashindikana.
Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu amesema Israel ina haki ya kuanza tena mapigano na Hamas kwa njia mpya na kwa nguvu mpya kama ikihitajika, iwapo mazungumzo zaidi ya kusitisha mapigano yatavunjika. Makubaliano ya kusitisha mapigano na Hamas, yanatarajiwa kuanza kutekelezwa Jumapili asubuhi kwa saa za huko. Netanyahu amebainisha kuwa marais wawili wa Marekani, Joe Biden anayemaliza muda wake na anayetarajiwa kuingia madarakani, Donald Trump, wanaiunga mkono Israel kurejea kupigana, iwapo mazungumzo ya awamu ya pili ya makubaliano yatashindikana.
·22 Views