NELIUD  COSIAH
NELIUD  COSIAH

@nelly2020

251 Posts
209 Photos
13 Videos
Lives in Dar es salaam
From Dar es salaam
Male
Single
26/05/2000
Pinned Post
#PART1

Kuna gereza, na kuna Guantanamo Bay.

Hili si gereza la kawaida. Ni shimo la mateso, mahali ambapo sheria za haki za binadamu zinaonekana kama hadithi za kufikirika.

Lipo Cuba, lakini linamilikiwa na Marekani.

Wanasema gereza ni sehemu ya kutumikia adhabu, lakini Guantanamo ni sehemu ambapo unatakiwa kusahau kama ulikuwa binadamu.

Kama umewekwa hapa, ni ishara kwamba dunia imeshakusahau.
Na hata kama hauna hatia, hutaweza kuthibitisha chochote.

Marekani ni taifa la haki, Ndio! angalau kwenye makaratasi.
Lakini hata Wamarekani wenyewe walikuwa hawapendi Guantanamo.

Kila mwaka, wanaharakati wa haki za binadamu walikuwa wakiandamana, wakitaka gereza hilo lifungwe.

Ilipofika mwaka 2008, Barack Obama alipoingia kwenye kinyang'anyiro cha urais, akaahidi jambo moja kubwa.

"Nikichaguliwa kuwa Rais, gereza la Guantanamo litafungwa mara moja!"

Ilionekana kama ahadi ya kweli.

Wamarekani wakashangilia, wakaamini kwamba hatimaye heshima ya taifa lao itarudi.
#PART1 Kuna gereza, na kuna Guantanamo Bay. Hili si gereza la kawaida. Ni shimo la mateso, mahali ambapo sheria za haki za binadamu zinaonekana kama hadithi za kufikirika. Lipo Cuba, lakini linamilikiwa na Marekani. Wanasema gereza ni sehemu ya kutumikia adhabu, lakini Guantanamo ni sehemu ambapo unatakiwa kusahau kama ulikuwa binadamu. Kama umewekwa hapa, ni ishara kwamba dunia imeshakusahau. Na hata kama hauna hatia, hutaweza kuthibitisha chochote. Marekani ni taifa la haki, Ndio! angalau kwenye makaratasi. Lakini hata Wamarekani wenyewe walikuwa hawapendi Guantanamo. Kila mwaka, wanaharakati wa haki za binadamu walikuwa wakiandamana, wakitaka gereza hilo lifungwe. Ilipofika mwaka 2008, Barack Obama alipoingia kwenye kinyang'anyiro cha urais, akaahidi jambo moja kubwa. "Nikichaguliwa kuwa Rais, gereza la Guantanamo litafungwa mara moja!" Ilionekana kama ahadi ya kweli. Wamarekani wakashangilia, wakaamini kwamba hatimaye heshima ya taifa lao itarudi.
0 Comments ·0 Shares ·405 Views
Recent Updates
  • Ilichukua zaidi ya miezi mitatu kuzima moto mkubwa na kusafisha eneo la tukio. Ujenzi, ambao uligharimu mamia ya mamilioni ya dola, ulidumu hadi 2007.
    Ilichukua zaidi ya miezi mitatu kuzima moto mkubwa na kusafisha eneo la tukio. Ujenzi, ambao uligharimu mamia ya mamilioni ya dola, ulidumu hadi 2007.
    Like
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·75 Views
  • PART 8

    Watu karibu 3,000 waangamia katika mashambulizi

    Mashambulizi haya manne, yaliyotekelezwa chini ya saa mbili, yaligharimu maisha ya watu 2,977, ikiwa ni pamoja na waokoaji 441 kutoka mji wa New York. Zaidi ya watu 6,000 walijeruhiwa na wengine waliumwa magonjwa yanayohusiana na mashambulio hayo, haswa kwa sababu walivuta chembe zenye sumu ambazo ziliendelea kwa wiki kadhaa baada ya mashambulio.
    PART 8 Watu karibu 3,000 waangamia katika mashambulizi Mashambulizi haya manne, yaliyotekelezwa chini ya saa mbili, yaligharimu maisha ya watu 2,977, ikiwa ni pamoja na waokoaji 441 kutoka mji wa New York. Zaidi ya watu 6,000 walijeruhiwa na wengine waliumwa magonjwa yanayohusiana na mashambulio hayo, haswa kwa sababu walivuta chembe zenye sumu ambazo ziliendelea kwa wiki kadhaa baada ya mashambulio.
    Like
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·90 Views
  • PART 7

    Saa 4:28 asubuhi, Mnara wa Kaskazini wa WTC ulianguka, dakika 102 baada ya athari iliyosababishwa na ndege ya shirika la ndege la American Airlines. Mamia ya watu, ambao hawakuweza kuondolewa, ikiwa ni pamoja na waokoaji waliokuwa katika ghorofa, walifukiwa na vifusi vya jengo hilo.
    Minara hiyo inayoanguka pia ilisababisha uharibifu mkubwa kwa majengo yaliyo kuwa karibu, kama mnara wa 7 wa WTC, ambao ulidondoka saa 11:20 jioni.
    PART 7 Saa 4:28 asubuhi, Mnara wa Kaskazini wa WTC ulianguka, dakika 102 baada ya athari iliyosababishwa na ndege ya shirika la ndege la American Airlines. Mamia ya watu, ambao hawakuweza kuondolewa, ikiwa ni pamoja na waokoaji waliokuwa katika ghorofa, walifukiwa na vifusi vya jengo hilo. Minara hiyo inayoanguka pia ilisababisha uharibifu mkubwa kwa majengo yaliyo kuwa karibu, kama mnara wa 7 wa WTC, ambao ulidondoka saa 11:20 jioni.
    Like
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·97 Views
  • PART 6

    Saa 3:59 asubuhi, Mnara wa Kusini wa kituo cha Biashara cha World Trade Center (WTC) ulidondoka wenyewe, dakika 55 matukio hayo ya kwanza.
    Ndege ya nne, ya shirika la ndege la United Airlines Flight 93, ilianguka saa 10: 03 asubuhi kwenye chamba moja karibu na Pittsburg, huko Pennsylvania, ikiwa na watu 44, wakiwemo magaidi wanne. Abiria kwenye ndege hiyo waliripotiwa kupigana na watekaji nyara baada ya kuambiwa juu ya mkasa huo kwenye simu zao za rununu. Inaaminika kwamba ndege hii, iliyokuwa ikielekea Washington,ilienda kushambulia Capitol, makao makuu ya Bunge la Marekani.
    PART 6 Saa 3:59 asubuhi, Mnara wa Kusini wa kituo cha Biashara cha World Trade Center (WTC) ulidondoka wenyewe, dakika 55 matukio hayo ya kwanza. Ndege ya nne, ya shirika la ndege la United Airlines Flight 93, ilianguka saa 10: 03 asubuhi kwenye chamba moja karibu na Pittsburg, huko Pennsylvania, ikiwa na watu 44, wakiwemo magaidi wanne. Abiria kwenye ndege hiyo waliripotiwa kupigana na watekaji nyara baada ya kuambiwa juu ya mkasa huo kwenye simu zao za rununu. Inaaminika kwamba ndege hii, iliyokuwa ikielekea Washington,ilienda kushambulia Capitol, makao makuu ya Bunge la Marekani.
    Like
    Love
    2
    · 0 Comments ·0 Shares ·94 Views
  • PART 5

    Lakini saa 3:37 asubuhi huko Virginia, ndege ya tatu, ya shirika la ndege la American Airlines Flight 77, ilianguka katika sehemu ya magharibi ya Pentagon, makao makuu ya wizara ya Ulinzi ya Marekani, ikiwa na watu 64, wakiwemo watu watano wa kujitoa mhanga.
    PART 5 Lakini saa 3:37 asubuhi huko Virginia, ndege ya tatu, ya shirika la ndege la American Airlines Flight 77, ilianguka katika sehemu ya magharibi ya Pentagon, makao makuu ya wizara ya Ulinzi ya Marekani, ikiwa na watu 64, wakiwemo watu watano wa kujitoa mhanga.
    Like
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·87 Views
  • PART 4

    2:46 asubuhi, ulimwengu wapigwa na bumbuwazi

    Ilikuwa saa 2:46 asubuhi, saa zahuko New York, wakati Boeing 767 kutoka shirika la ndege la American Airlines Flight 11 ilipoanguka kwenye Mnara wa Kaskazini wa kituo cha Biashara cha World Trade Center , ikiwa na watu 92 , wakiwemo magaidi watano.
    Dakika kumi na saba baadaye, saa 3:03 asubuhi, vituo kadhaa vya televisheni vilikuwa vikitangaza tukio hilo, watu waliona ndege ya shirika la ndege la United Airlines Flight 175 ikigonga Mnara wa Kusini wa jengo hilo la kibiashara. Watu 65 walikuemo, ikiwa ni pamoja na watekaji nyara watano. Wakati moto ukiharibu sakafu za juu za minara hiyo miwili, Andrew Card, mkurugenzi katika ofisi ya rais, alimfahamisha rais George W. Bush: “Ndege ya pili imegonga mnara mwingine na Marekani sasa inashambuliwa. "
    PART 4 2:46 asubuhi, ulimwengu wapigwa na bumbuwazi Ilikuwa saa 2:46 asubuhi, saa zahuko New York, wakati Boeing 767 kutoka shirika la ndege la American Airlines Flight 11 ilipoanguka kwenye Mnara wa Kaskazini wa kituo cha Biashara cha World Trade Center , ikiwa na watu 92 , wakiwemo magaidi watano. Dakika kumi na saba baadaye, saa 3:03 asubuhi, vituo kadhaa vya televisheni vilikuwa vikitangaza tukio hilo, watu waliona ndege ya shirika la ndege la United Airlines Flight 175 ikigonga Mnara wa Kusini wa jengo hilo la kibiashara. Watu 65 walikuemo, ikiwa ni pamoja na watekaji nyara watano. Wakati moto ukiharibu sakafu za juu za minara hiyo miwili, Andrew Card, mkurugenzi katika ofisi ya rais, alimfahamisha rais George W. Bush: “Ndege ya pili imegonga mnara mwingine na Marekani sasa inashambuliwa. "
    Like
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·91 Views
  • PART 3

    Chini ya saa mbili, majengo muhimu ya nchi hii yenye nguvu duniani yalishambuliwa, na kuua karibu watu 3,000 na kujeruhi maelfu kadhaa. Mashambulio haya, ambayo ni mabaya zaidi katika historia ya kisasa, yaliuacha ulimwengu wote kwa mshtuko mkubwa.
    PART 3 Chini ya saa mbili, majengo muhimu ya nchi hii yenye nguvu duniani yalishambuliwa, na kuua karibu watu 3,000 na kujeruhi maelfu kadhaa. Mashambulio haya, ambayo ni mabaya zaidi katika historia ya kisasa, yaliuacha ulimwengu wote kwa mshtuko mkubwa.
    Like
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·92 Views
  • PART 2

    Kwa mara ya pili katika historia yake, Marekani ilikumbwa na shambulio la ndani, hali ambayo ilishuwa wengi wakati Marekani ni mojawapo ya nchi zenye nguvu duniani ambapo ni vigumu kupenya na kufanya shambulizi kubwa kama hilo.
    PART 2 Kwa mara ya pili katika historia yake, Marekani ilikumbwa na shambulio la ndani, hali ambayo ilishuwa wengi wakati Marekani ni mojawapo ya nchi zenye nguvu duniani ambapo ni vigumu kupenya na kufanya shambulizi kubwa kama hilo.
    Like
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·81 Views
  • PART 1

    Miaka ishirini iliyopita, asubuhi ya Septemba 11, 2001 katika pwani ya mashariki mwa Marekani, ndege nne za abiria zilitekwa nyara kwa wakati mmoja na magaidi 19 na kusababisha vifo vya maelfu ya watu baada ya kugonga minara pacha ya kituo cha bisahara cha World Trade Center nchini Marekani.
    PART 1 Miaka ishirini iliyopita, asubuhi ya Septemba 11, 2001 katika pwani ya mashariki mwa Marekani, ndege nne za abiria zilitekwa nyara kwa wakati mmoja na magaidi 19 na kusababisha vifo vya maelfu ya watu baada ya kugonga minara pacha ya kituo cha bisahara cha World Trade Center nchini Marekani.
    Like
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·41 Views
  • Osama Bin Laden, al-Qaeda na mwanzo wa shambulio la Septemba 11, 2001.

    Uzi👇🏿
    Osama Bin Laden, al-Qaeda na mwanzo wa shambulio la Septemba 11, 2001.🧨 Uzi🧵👇🏿
    Like
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·30 Views
  • Issue ya Harold Shipman ilitikisa ulimwengu wa kitabibu.

    Ilizua hofu na maswali mengi—je, kuna wauaji wengine waliyojificha kwenye taaluma ya tiba?

    Serikali ya Uingereza ilibadilisha sheria za matibabu, na hospitali nyingi duniani ziliboresha mifumo yao ili kuhakikisha hakuna daktari mwingine anayeweza kufanya alichofanya Shipman.
    Issue ya Harold Shipman ilitikisa ulimwengu wa kitabibu. Ilizua hofu na maswali mengi—je, kuna wauaji wengine waliyojificha kwenye taaluma ya tiba? Serikali ya Uingereza ilibadilisha sheria za matibabu, na hospitali nyingi duniani ziliboresha mifumo yao ili kuhakikisha hakuna daktari mwingine anayeweza kufanya alichofanya Shipman.
    Like
    Love
    2
    · 0 Comments ·0 Shares ·223 Views
  • (F)
    Baada ya uchunguzi wa haraka, polisi walifukua miili kadhaa ya wagonjwa wa Shipman na kugundua kitu cha kutisha—miili yao ilikuwa na kiwango kikubwa cha morphine.

    Shipman alikamatwa na kushtakiwa kwa mauaji ya wagonjwa 15, lakini uchunguzi wa kina ulionesha kuwa huenda alikuwa amewaua zaidi ya watu 250 kwa kipindi cha miaka 23!

    Alifungwa jela mwaka 2000, na mwaka 2004, alipatikana amejinyonga kwenye seli yake.
    (F) Baada ya uchunguzi wa haraka, polisi walifukua miili kadhaa ya wagonjwa wa Shipman na kugundua kitu cha kutisha—miili yao ilikuwa na kiwango kikubwa cha morphine. Shipman alikamatwa na kushtakiwa kwa mauaji ya wagonjwa 15, lakini uchunguzi wa kina ulionesha kuwa huenda alikuwa amewaua zaidi ya watu 250 kwa kipindi cha miaka 23! Alifungwa jela mwaka 2000, na mwaka 2004, alipatikana amejinyonga kwenye seli yake.
    Like
    Love
    2
    · 0 Comments ·0 Shares ·185 Views
  • (E)
    Kwa miaka mingi, Shipman aliendelea na mauaji yake bila kugundulika.

    Lakini mnamo 1998, alifanya kosa moja kubwa—alijaribu kughushi wosia wa mgonjwa wake mmoja, Kathleen Grundy.

    Kathleen alikuwa mama mwenye afya njema mwenye umri wa miaka 81. Alipoaga dunia ghafla, binti yake, Angela Woodruff, alishangazwa na jinsi kifo hicho kilivyotokea bila onyo.

    Lakini mshangao mkubwa zaidi ulikuja alipogundua kuwa mama yake alikuwa ameandika wosia mpya, ukisema kuwa mali yake yote iende kwa daktari wake—Harold Shipman!

    Huo ulikuwa ushahidi wa kwanza wa kweli kwamba huyu hakuwa daktari wa kawaida—alikuwa muuaji.
    (E) Kwa miaka mingi, Shipman aliendelea na mauaji yake bila kugundulika. Lakini mnamo 1998, alifanya kosa moja kubwa—alijaribu kughushi wosia wa mgonjwa wake mmoja, Kathleen Grundy. Kathleen alikuwa mama mwenye afya njema mwenye umri wa miaka 81. Alipoaga dunia ghafla, binti yake, Angela Woodruff, alishangazwa na jinsi kifo hicho kilivyotokea bila onyo. Lakini mshangao mkubwa zaidi ulikuja alipogundua kuwa mama yake alikuwa ameandika wosia mpya, ukisema kuwa mali yake yote iende kwa daktari wake—Harold Shipman! Huo ulikuwa ushahidi wa kwanza wa kweli kwamba huyu hakuwa daktari wa kawaida—alikuwa muuaji.
    Like
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·226 Views
  • (D)
    Shipman alikuwa daktari wa kuaminika. Wagonjwa wake walimpenda kwa sababu alikuwa mwenye huruma, na alikuwa akiwatembelea hata majumbani kwao.

    Lakini ilianza kuonekana kuwa wagonjwa wake walikuwa wakifa kwa wingi kuliko kawaida.

    Walikuwa wakifa kwa "mashambulizi ya moyo" au "udhaifu wa uzee." Hakukuwa na ishara ya mateso—ilikuwa ni kama waliaga dunia kwa utulivu.

    Mara nyingi, alikuwa daktari pekee aliyekuwepo wakati wa vifo hivyo.

    Hakuna aliyeshuku lolote, hasa kwa sababu wengi wa waliokufa walikuwa wazee.

    Lakini jambo la ajabu ni kwamba, tofauti na madaktari wengine ambao hujaribu kuwaokoa wagonjwa wao hadi dakika ya mwisho, Shipman hakuwahi kujaribu kuwapigania—hakuwahi kupiga simu kwa ambulansi.

    Alikuwa akiwapatia sindano ya morphine katika dozi kubwa—sawa na aliyowahi kuona ikitumiwa kwa mama yake alipokuwa kijana. Na ndani ya dakika chache, walikuwa wakiondoka duniani kimyakimya
    (D) Shipman alikuwa daktari wa kuaminika. Wagonjwa wake walimpenda kwa sababu alikuwa mwenye huruma, na alikuwa akiwatembelea hata majumbani kwao. Lakini ilianza kuonekana kuwa wagonjwa wake walikuwa wakifa kwa wingi kuliko kawaida. Walikuwa wakifa kwa "mashambulizi ya moyo" au "udhaifu wa uzee." Hakukuwa na ishara ya mateso—ilikuwa ni kama waliaga dunia kwa utulivu. Mara nyingi, alikuwa daktari pekee aliyekuwepo wakati wa vifo hivyo. Hakuna aliyeshuku lolote, hasa kwa sababu wengi wa waliokufa walikuwa wazee. Lakini jambo la ajabu ni kwamba, tofauti na madaktari wengine ambao hujaribu kuwaokoa wagonjwa wao hadi dakika ya mwisho, Shipman hakuwahi kujaribu kuwapigania—hakuwahi kupiga simu kwa ambulansi. Alikuwa akiwapatia sindano ya morphine katika dozi kubwa—sawa na aliyowahi kuona ikitumiwa kwa mama yake alipokuwa kijana. Na ndani ya dakika chache, walikuwa wakiondoka duniani kimyakimya
    Like
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·201 Views
  • (C)
    Baada ya kifo cha mama yake, Shipman aliamua kuwa daktari. Alijiunga na Chuo Kikuu cha Leeds na baadaye akawa tabibu wa familia.

    Katika mwonekano wa nje, alikuwa mtu mwema, mtu wa familia, mwenye mke na watoto, anayependwa na wagonjwa wake. Lakini ndani yake, alikuwa akijificha kwenye kivuli cha giza na mauaji l.

    Alianza kazi yake kama daktari huko Yorkshire, na ilisemekana kuwa alikuwa mzuri sana kwa wagonjwa wake.

    Hata hivyo, mnamo 1975, alinaswa akiandika dawa za opioid (pethidine) kwa matumizi yake binafsi. Alipatikana na hatia, lakini badala ya kufungwa jela, alipigwa faini na kupoteza kazi kwa muda mfupi.

    Baadaye, alihamia mji wa Hyde na kuanza upya maisha yake kama daktari wa familia.

    Huko ndipo msururu wa vifo vya ajabu ulipoanza.
    (C) Baada ya kifo cha mama yake, Shipman aliamua kuwa daktari. Alijiunga na Chuo Kikuu cha Leeds na baadaye akawa tabibu wa familia. Katika mwonekano wa nje, alikuwa mtu mwema, mtu wa familia, mwenye mke na watoto, anayependwa na wagonjwa wake. Lakini ndani yake, alikuwa akijificha kwenye kivuli cha giza na mauaji l. Alianza kazi yake kama daktari huko Yorkshire, na ilisemekana kuwa alikuwa mzuri sana kwa wagonjwa wake. Hata hivyo, mnamo 1975, alinaswa akiandika dawa za opioid (pethidine) kwa matumizi yake binafsi. Alipatikana na hatia, lakini badala ya kufungwa jela, alipigwa faini na kupoteza kazi kwa muda mfupi. Baadaye, alihamia mji wa Hyde na kuanza upya maisha yake kama daktari wa familia. Huko ndipo msururu wa vifo vya ajabu ulipoanza.
    Like
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·209 Views
  • (B)
    Dr. Harold Frederick Shipman alizaliwa mnamo 1946 huko Nottingham, Uingereza.

    Alikua katika familia yenye maisha ya kawaida, lakini kitu kimoja kilimtofautisha na watoto wengine—upendo wake kwa mama yake.

    Mama yake, Vera, alikuwa kila kitu kwake. Lakini alipofikisha miaka 17, alishuhudia kitu ambacho pengine kingemuumba kuwa mtu wa kutisha zaidi katika historia ya madaktari.

    Mama yake aligunduliwa kuwa na saratani ya mapafu.

    Katika miezi ya mwisho ya ugonjwa wake, alikuwa akipewa dawa za kupunguza maumivu—morphine—na Harold kijana aliona jinsi dawa hizo zilivyomfanya mama yake awe mtulivu kabla ya kufariki.

    Ilikuwa ni tukio lililobadilisha maisha yake.

    Lakini hakuna aliyefikiria kwamba tukio hili lingekuwa chanzo cha wimbi la vifo visivyoelezeka.
    (B) Dr. Harold Frederick Shipman alizaliwa mnamo 1946 huko Nottingham, Uingereza. Alikua katika familia yenye maisha ya kawaida, lakini kitu kimoja kilimtofautisha na watoto wengine—upendo wake kwa mama yake. Mama yake, Vera, alikuwa kila kitu kwake. Lakini alipofikisha miaka 17, alishuhudia kitu ambacho pengine kingemuumba kuwa mtu wa kutisha zaidi katika historia ya madaktari. Mama yake aligunduliwa kuwa na saratani ya mapafu. Katika miezi ya mwisho ya ugonjwa wake, alikuwa akipewa dawa za kupunguza maumivu—morphine—na Harold kijana aliona jinsi dawa hizo zilivyomfanya mama yake awe mtulivu kabla ya kufariki. Ilikuwa ni tukio lililobadilisha maisha yake. Lakini hakuna aliyefikiria kwamba tukio hili lingekuwa chanzo cha wimbi la vifo visivyoelezeka.
    Like
    2
    · 0 Comments ·0 Shares ·263 Views
  • (A)
    Katika jamii, daktari ni mtu unayemwamini zaidi unapokuwa unaumwa au dhaifu.

    Ni mtu anayeshika maisha yako mikononi mwake na kufanya kila awezalo kuhakikisha unabaki hai.

    But vipi yule unayemtegemea ndio anayekuua taratibu, bila hata wewe kujua?

    Huyu ni Harold Shipman, daktari aliyekuwa muuaji wa kutisha zaidi katika historia ya Uingereza—pengine duniani kote.

    Muuaji hatari aliyejificha kwenye taaluma ya tiba.

    Thread
    (A) Katika jamii, daktari ni mtu unayemwamini zaidi unapokuwa unaumwa au dhaifu. Ni mtu anayeshika maisha yako mikononi mwake na kufanya kila awezalo kuhakikisha unabaki hai. But vipi yule unayemtegemea ndio anayekuua taratibu, bila hata wewe kujua? Huyu ni Harold Shipman, daktari aliyekuwa muuaji wa kutisha zaidi katika historia ya Uingereza—pengine duniani kote. Muuaji hatari aliyejificha kwenye taaluma ya tiba. Thread 🧵
    Like
    Wow
    2
    · 0 Comments ·0 Shares ·207 Views
  • 10. DAMASCUS

    Sauli wa Tarso (ambaye baadaye alikuja kuwa Paulo) ndiye mtu anayekuja akilini kwa mara ya kwanza mtu anapofikiria Damasko.

    Ilikuwa ni njiani pale alipokutana na Kristo.

    Ajabu alikuwa njiani kuwatesa Wakristo kutoka Kanisa la kwanza.

    Katika Matendo sura ya 9 inasema, “Ikawa alipokuwa akienda zake, akikaribia Dameski, ghafula nuru kutoka mbinguni ilimwangazia pande zote.” Alianguka chini na kupoteza uwezo wake wa kuona. Sauli aliongoka baadaye na kuwa mmoja wa watetezi wa Kristo wenye shauku zaidi.
    10. DAMASCUS Sauli wa Tarso (ambaye baadaye alikuja kuwa Paulo) ndiye mtu anayekuja akilini kwa mara ya kwanza mtu anapofikiria Damasko. Ilikuwa ni njiani pale alipokutana na Kristo. Ajabu alikuwa njiani kuwatesa Wakristo kutoka Kanisa la kwanza. Katika Matendo sura ya 9 inasema, “Ikawa alipokuwa akienda zake, akikaribia Dameski, ghafula nuru kutoka mbinguni ilimwangazia pande zote.” Alianguka chini na kupoteza uwezo wake wa kuona. Sauli aliongoka baadaye na kuwa mmoja wa watetezi wa Kristo wenye shauku zaidi.
    Like
    Love
    2
    · 0 Comments ·0 Shares ·152 Views
  • 9. MTO YORDANI

    Mto Yordani ulikuwa sehemu ya matukio kadhaa muhimu yaliyorekodiwa katika Biblia. Katika nyakati za awali za kuwepo kwa Israeli ilikuwa ni "daraja" au ishara ya mpito katika nchi ya ahadi ya Mungu.

    Sehemu kubwa za Nchi ya Ahadi zilikuwa ng’ambo ya mto. Ilikuwa ni Mto Yordani ambao nabii Eliya aliupiga kwa vazi lake la kukunjwa na kuyagawanya maji (2 Wafalme 2:8).
    9. MTO YORDANI Mto Yordani ulikuwa sehemu ya matukio kadhaa muhimu yaliyorekodiwa katika Biblia. Katika nyakati za awali za kuwepo kwa Israeli ilikuwa ni "daraja" au ishara ya mpito katika nchi ya ahadi ya Mungu. Sehemu kubwa za Nchi ya Ahadi zilikuwa ng’ambo ya mto. Ilikuwa ni Mto Yordani ambao nabii Eliya aliupiga kwa vazi lake la kukunjwa na kuyagawanya maji (2 Wafalme 2:8).
    Like
    Love
    2
    · 0 Comments ·0 Shares ·125 Views
  • 8. Zamani mji wa Gadara, Umm Qais anaangalia Bahari ya Galilaya.

    Hapa ndipo Yesu aliweza kufanya Muujiza wa Nguruwe wa Gadarene.

    Simulizi moja la Biblia linasema kwamba alipokutana na wanaume wawili walioishi makaburini karibu na mwingilio wa Gadara na waliokuwa na roho waovu, Yesu aliwafukuza roho waovu hao na kuwaingiza ndani ya kundi la nguruwe.

    Kisha nguruwe hao wakakimbia kutoka kwenye jabali hadi kwenye Bahari ya Galilaya, ambako walikufa maji.
    8. Zamani mji wa Gadara, Umm Qais anaangalia Bahari ya Galilaya. Hapa ndipo Yesu aliweza kufanya Muujiza wa Nguruwe wa Gadarene. Simulizi moja la Biblia linasema kwamba alipokutana na wanaume wawili walioishi makaburini karibu na mwingilio wa Gadara na waliokuwa na roho waovu, Yesu aliwafukuza roho waovu hao na kuwaingiza ndani ya kundi la nguruwe. Kisha nguruwe hao wakakimbia kutoka kwenye jabali hadi kwenye Bahari ya Galilaya, ambako walikufa maji.
    Like
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·125 Views
  • 7. Tel Hazor
    Katika eneo la ekari 200 hivi, eneo hili lililo katika Galilaya ya Juu (sasa ni mbuga ya kitaifa) ndilo kubwa zaidi kati ya “tels” za Israeli,

    Kulingana na Agano la Kale, Hazori ilikuwa mahali pa ushindi muhimu wa Yoshua katika ushindi wake wa Kanaani baada ya kifo cha Musa; eti aliteketeza jiji hilo kabisa, akisafisha njia kwa ajili ya makazi ya Waisraeli.
    7. Tel Hazor Katika eneo la ekari 200 hivi, eneo hili lililo katika Galilaya ya Juu (sasa ni mbuga ya kitaifa) ndilo kubwa zaidi kati ya “tels” za Israeli, Kulingana na Agano la Kale, Hazori ilikuwa mahali pa ushindi muhimu wa Yoshua katika ushindi wake wa Kanaani baada ya kifo cha Musa; eti aliteketeza jiji hilo kabisa, akisafisha njia kwa ajili ya makazi ya Waisraeli.
    0 Comments ·0 Shares ·197 Views
  • 6. BONDE LA ELAH

    Bonde hili linajulikana kwa kuandaa moja ya pambano maarufu katika historia.

    Goliathi, jitu la Mfilisti, alitoa changamoto kwa jeshi la Israeli kutuma mtu wa kupigana naye mahali hapa.

    Watu wote wa Sauli walimwogopa yule shujaa mkubwa ambaye alikuwa na urefu wa zaidi ya futi nane. Mchungaji kijana Daudi alisimama na kujitolea kwenda kinyume naye. Jitu lilishindwa na Israeli wakashinda jeshi la Wafilisti.
    6. BONDE LA ELAH Bonde hili linajulikana kwa kuandaa moja ya pambano maarufu katika historia. Goliathi, jitu la Mfilisti, alitoa changamoto kwa jeshi la Israeli kutuma mtu wa kupigana naye mahali hapa. Watu wote wa Sauli walimwogopa yule shujaa mkubwa ambaye alikuwa na urefu wa zaidi ya futi nane. Mchungaji kijana Daudi alisimama na kujitolea kwenda kinyume naye. Jitu lilishindwa na Israeli wakashinda jeshi la Wafilisti.
    0 Comments ·0 Shares ·133 Views
  • 5.BETHLEHEMU

    “Nyumba ya mkate” imetajwa katika sehemu mbalimbali za Maandiko.

    Zamani iliitwa Efratha na katika visa vingine Bethlehemu ya Yuda au Bethlehemu-Yuda. Elimeleki, ambaye angekuwa baba-mkwe wa Ruthu aliyetajwa hapo juu alikuwa raia wa Bethlehemu.

    Mfalme Daudi wa Israeli pia alikuwa Mbethlehemu.

    Zaidi sana ingawa, ulikuwa ni mji ambao ulitupa Kristo mwenyewe.

    Hapa palikuwa mahali pa kuzaliwa kwa mtoto wa kwanza wa Mariamu. “Akamzaa mwanawe mzaliwa wa kwanza, akamvika nguo za kitoto, akamlaza katika hori ya kulia ng’ombe; kwa sababu hapakuwa na nafasi katika nyumba ya wageni”, Luka 2:7 inasema.
    5.BETHLEHEMU “Nyumba ya mkate” imetajwa katika sehemu mbalimbali za Maandiko. Zamani iliitwa Efratha na katika visa vingine Bethlehemu ya Yuda au Bethlehemu-Yuda. Elimeleki, ambaye angekuwa baba-mkwe wa Ruthu aliyetajwa hapo juu alikuwa raia wa Bethlehemu. Mfalme Daudi wa Israeli pia alikuwa Mbethlehemu. Zaidi sana ingawa, ulikuwa ni mji ambao ulitupa Kristo mwenyewe. Hapa palikuwa mahali pa kuzaliwa kwa mtoto wa kwanza wa Mariamu. “Akamzaa mwanawe mzaliwa wa kwanza, akamvika nguo za kitoto, akamlaza katika hori ya kulia ng’ombe; kwa sababu hapakuwa na nafasi katika nyumba ya wageni”, Luka 2:7 inasema.
    Love
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·122 Views
  • 4. Mji Mkongwe Jerusalem

    Kulingana na mapokeo ya Kiyahudi, Mlima wa Hekalu (ambao sasa uko ndani ya kiwanja cha kuta ndani ya Jiji la Kale) ndipo Mungu alipokusanya vumbi ili kumuumba mwanadamu wa kwanza, Adamu, na ambapo mwana wa Mfalme Daudi, Sulemani, alijenga hekalu la kwanza karibu 1000 K.K. (baadaye iliangushwa na Wababeli).

    Waislamu pia wanaabudu katika eneo hilo, ambalo sasa ni nyumbani kwa Dome of the Rock, madhabahu ya Kiislamu, na Msikiti wa al-Aqsa.

    Madai haya yanayoshindana yamesababisha hii kuwa moja ya maeneo yanayoshindaniwa zaidi ulimwenguni. Mji wa Kale una maeneo mengine muhimu ya kidini, ikiwa ni pamoja na Kanisa la Kaburi Takatifu, mahali pa kusulubiwa kwa Yesu na kaburi lake (tupu), na Ukuta wa Magharibi, mabaki ya Hekalu la Pili (lililojengwa na Mfalme Herode katika karne ya kwanza B.K.) ambalo ni eneo takatifu zaidi ambalo Wayahudi wanaweza kwenda kusali.
    4. Mji Mkongwe Jerusalem Kulingana na mapokeo ya Kiyahudi, Mlima wa Hekalu (ambao sasa uko ndani ya kiwanja cha kuta ndani ya Jiji la Kale) ndipo Mungu alipokusanya vumbi ili kumuumba mwanadamu wa kwanza, Adamu, na ambapo mwana wa Mfalme Daudi, Sulemani, alijenga hekalu la kwanza karibu 1000 K.K. (baadaye iliangushwa na Wababeli). Waislamu pia wanaabudu katika eneo hilo, ambalo sasa ni nyumbani kwa Dome of the Rock, madhabahu ya Kiislamu, na Msikiti wa al-Aqsa. Madai haya yanayoshindana yamesababisha hii kuwa moja ya maeneo yanayoshindaniwa zaidi ulimwenguni. Mji wa Kale una maeneo mengine muhimu ya kidini, ikiwa ni pamoja na Kanisa la Kaburi Takatifu, mahali pa kusulubiwa kwa Yesu na kaburi lake (tupu), na Ukuta wa Magharibi, mabaki ya Hekalu la Pili (lililojengwa na Mfalme Herode katika karne ya kwanza B.K.) ambalo ni eneo takatifu zaidi ambalo Wayahudi wanaweza kwenda kusali.
    Love
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·241 Views
  • 3. JOPPA

    Katika bandari hii Yona alipanda meli iendayo Tarshishi ili kumkimbia Mungu.

    Akiwa njiani, dhoruba kali ilikutana na chombo na nabii huyo akajikuta “katika moyo wa bahari” (Yona 2:3).

    Baadaye alitemwa ufukweni na samaki mkubwa aliyemmeza. Tarshishi (mahali alipoenda Yona) ilikuwa nchi ya pwani na kitovu cha biashara wakati huo.

    Mfalme Sulemani alikuwa na kundi la meli ambazo zilifika huko mara moja kila baada ya miaka mitatu na kuleta fedha, dhahabu, pembe za ndovu, nyani, tausi na hazina zingine za kigeni.
    3. JOPPA Katika bandari hii Yona alipanda meli iendayo Tarshishi ili kumkimbia Mungu. Akiwa njiani, dhoruba kali ilikutana na chombo na nabii huyo akajikuta “katika moyo wa bahari” (Yona 2:3). Baadaye alitemwa ufukweni na samaki mkubwa aliyemmeza. Tarshishi (mahali alipoenda Yona) ilikuwa nchi ya pwani na kitovu cha biashara wakati huo. Mfalme Sulemani alikuwa na kundi la meli ambazo zilifika huko mara moja kila baada ya miaka mitatu na kuleta fedha, dhahabu, pembe za ndovu, nyani, tausi na hazina zingine za kigeni.
    Love
    1
    · 0 Comments ·0 Shares ·179 Views
More Stories