Kinara wa mabao ndani ya Simba hatua ya makundi, Kibu Denis aliyefunga matatu, amefunguka kuwa haikuwa rahisi kufuzu robo fainali na kuongoza kundi, hivyo kwa sasa wanajipanga kuhakikisha wanatwaa ubingwa wa michuano hiyo.
.
“Tumeweza kutoboa hatua ya mtoano na makundi, sasa tumetinga robo fainali, zote zilikuwa ngumu, tunapoenda ndio kuna ugumu zaidi, mipango yetu ni kuona tunaweka rekodi nyingine kubwa ya kutwaa taji,”
.
“Hakuna kisichowezekana, kila mipango tuliyoipanga kuanzia hatua ya awali hadi sasa tumeifanikisha kwa usahihi, naamini hata hatua inayofuata tunaweza kuipambania na hatimaye kuandika historia ya ubingwa wa Kombe la Shirikisho.”
.
“Licha ya kutokuwa bora Ligi Kuu naamini pia nina nafasi ya kusawazisha makosa na kuwa bora kama ilivyo kwenye michuano hii ambayo bado tuna nafasi ya kuendelea kuipambania bendera ya nchi lakini pia timu kwa ujumla tuweze kuandika historia.”
#paulswai

1 Comments
·81 Views