Upgrade to Pro

Moto mwingine mkubwa umezuka hapo jana na kuteketeza eneo lenya ukubwa wa takribani ekari 9400 katika eneo la Castaic, Kaskazini mwa Mji wa Los Angeles, California Nchini Marekani .

Moto huo uliopewa jina la The Hughes Fire, unatajwa kuwa mkubwa kwa theluthi mbili ukilinganishwa na Moto wa Eaton ulioiteketeza vibaya Los Angeles. Zaidi ya watu 31,000 wametakiwa kuyahama makazi yao haraka iwezekanavyo wakati vikosi vya askari wa zimamoto na uokoaji zaidi ya 4000 wakiendelea kupambana na moto huo unaowaka umbali wa takribani kilometa 80, Kaskazini mwa Los Angeles.

Tangu kuzuka kwa jangala moto Mjini Los Angeles, vikosi vya zimamoto vimefanikiwa kuidhibiti mioto miwili tu huku juhudi zikiendelea usiku na mchana.

Moto mwingine mkubwa umezuka hapo jana na kuteketeza eneo lenya ukubwa wa takribani ekari 9400 katika eneo la Castaic, Kaskazini mwa Mji wa Los Angeles, California Nchini Marekani 🇺🇸. Moto huo uliopewa jina la The Hughes Fire, unatajwa kuwa mkubwa kwa theluthi mbili ukilinganishwa na Moto wa Eaton ulioiteketeza vibaya Los Angeles. Zaidi ya watu 31,000 wametakiwa kuyahama makazi yao haraka iwezekanavyo wakati vikosi vya askari wa zimamoto na uokoaji zaidi ya 4000 wakiendelea kupambana na moto huo unaowaka umbali wa takribani kilometa 80, Kaskazini mwa Los Angeles. Tangu kuzuka kwa jangala moto Mjini Los Angeles, vikosi vya zimamoto vimefanikiwa kuidhibiti mioto miwili tu huku juhudi zikiendelea usiku na mchana.
·17 Views