Shirika la habari la New York Post imeripoti kuwa Rais wa Marekani , Donald Trump amesitisha ufadhili wa kifedha kwenye mifuko inayopambana na virusi vya ukimwi Duniani kwa muda wa miezi mitatu. Zuio hilo litasababisha wasiwasi mkubwa wa upatikanaji wa dawa za kupambana na ugonjwa huo hatari kwa Wagonjwa takribani milioni (25) waliokuwa wanufaika na dawa hizo.

Baadhi ya mifuko mikubwa iliyokuwa ikipokea fedha ikiwemo PEPFAR na Shirika la USAID yataathirika na zuio hilo. Zuio hilo ni moja ya mazuio ya Donald Trump ya utoaji fedha nje kwa ajili ya misaada ambao unafanyiwa mapitio na Serikali yake kuona tija yake ili kuona kama kuna haja ya kuendelea na ufadhili.

Waathirika wakubwa katika zuio hilo ni bara la Afrika ambako idadi ya maambukizi na Wagonjwa bado ni kubwa huku hali ya umasikini kuweza kumudu gharama za dawa ikiwa sio nzuri. Trump anaendelea na sera ambazo zinatajwa kugusa makundi mbalimbali ulimwenguni kwa kila namna.

Ikumbukwe kwamba Marekani ndio Nchi linaloongoza kwa kutoa misaada Duniani ikiwemo ya kugharamia udhibiti wa magonjwa mbalimbali ikiwemo ugonjwa hatari wa UKIMWI, malaria na kifua kikuu.

Shirika la habari la New York Post imeripoti kuwa Rais wa Marekani 🇺🇸, Donald Trump amesitisha ufadhili wa kifedha kwenye mifuko inayopambana na virusi vya ukimwi Duniani kwa muda wa miezi mitatu. Zuio hilo litasababisha wasiwasi mkubwa wa upatikanaji wa dawa za kupambana na ugonjwa huo hatari kwa Wagonjwa takribani milioni (25) waliokuwa wanufaika na dawa hizo. Baadhi ya mifuko mikubwa iliyokuwa ikipokea fedha ikiwemo PEPFAR na Shirika la USAID yataathirika na zuio hilo. Zuio hilo ni moja ya mazuio ya Donald Trump ya utoaji fedha nje kwa ajili ya misaada ambao unafanyiwa mapitio na Serikali yake kuona tija yake ili kuona kama kuna haja ya kuendelea na ufadhili. Waathirika wakubwa katika zuio hilo ni bara la Afrika ambako idadi ya maambukizi na Wagonjwa bado ni kubwa huku hali ya umasikini kuweza kumudu gharama za dawa ikiwa sio nzuri. Trump anaendelea na sera ambazo zinatajwa kugusa makundi mbalimbali ulimwenguni kwa kila namna. Ikumbukwe kwamba Marekani ndio Nchi linaloongoza kwa kutoa misaada Duniani ikiwemo ya kugharamia udhibiti wa magonjwa mbalimbali ikiwemo ugonjwa hatari wa UKIMWI, malaria na kifua kikuu.
0 Commentarii ·0 Distribuiri ·111 Views