Undani wa bifu kati Rais wa DR Congo , Félix Tshisekedi na Kiongozi Mkuu wa Waasi wa M23, Corneille
Nanga.

Anaitwa Jenerali Corneille Nanga ambaye ni Kamanda Mkuu (Rais) wa makundi yote ya Waasi yanayopigana Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo likiwemo kundi la M23. Muungano huo unaitwa Congo River Allience na yeye ndio Kiongozi Mkuu na amesema malengo yao ni kuitwaa DR Congo yote mpaka Mji Mkuu Kinshasa.

Muungano wa makundi hayo aliutangaza rasmi mwaka 2023. Ikumbukwe kwamba Corneille Nanga alikuwa Mtumishi wa ngazi za juu ndani ya Serikali ya DR Congo kwa miaka mingi akifanya kazi katika programu mbalimbali za umoja wa mataifa. Mwaka 2015 mpaka 2021 alikuwa Mkuu wa tume ya Taifa ya uchaguzi Nchini humo CENI (Commission Electoral Ingependence) na ndiye aliyemtangaza Rais Felix Tshisekedi mshindi wa urais katika uchaguzi mwaka 2018.

Nanga alitofautiana na Mteuzi wake Rais mstaafu Joseph Kabila na Rais mpya Félix Tshisekedi kwamba kuna makubaliano walikubaliana katika uchaguzi wa 2018 ambapo anadai alichakachua uchaguzi kama Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi CENI na kumpa ushindi Tshisekedi ila baada ya ushindi Tshisekedi akageuka makubaliano yao. Tuhuma hizo Tshisekedi alizikanusha na kusema alishinda kihalali.

Baada ya mvutano mkali hatimaye Nanga alikimbia Nchi na mwaka 2023 katika mkutano wake uhamishoni Jijini Nairobi alitangaza Muungano wa makundi (17) ya Waasi wote wanaopigana Mashariki mwa DR Congo ikiwemo kundi la M23 na Muungano huo ukapewa jina la Congo River Allience na yeye kuwa ndio Kiongozi Mkuu mkuu wa makundi yote.

Wakati Nanga akiwa uhamishoni mahakama Kuu Jijini Kinshasa ilimuhukumu adhabu ya kifo akiwa hayupo mahakamani kwa kosa la uhaini. Kiufupi uasi wa DR Congo pakubwa umechangiwa na Uongozi mbovu, ukifuatilia mizizi ya mgogoro utagundua pia kuna mkataba Serikali ya Rais Laurent Kabila iliingia na jamii ya Watutsi Mashariki mwa DR Congo wakati wa kumpindua Rais wa zamani wa Nchi hiyo Mobutu Seseseko lakini baadaye akawageuka baada ya miaka mingi ya mvutano ndio ikaja kuundwa M23.

Moja makubaliano yao yalikua ni Jamii hiyo ya Watutsi kumsaidia Rais wa zamani Laurent Désiré Kabila (Baba Mzazi wa Joseph Kabila) kumpindua Mobutu kisa Watutsi wapewe sehemu ya Mkoa wa Sud-Kivu na wawe Raia wa DR Congo baada ya kuonekana kukataliwa na Paul Kagame kwa madai kwamba ni mmojawapo ya makundi yaliyohusika na mauwaji ya kimbari mwaka 1994.

Kundi hili la Waasi la M23, jana lilikanusha kwamba linaungwa mkono na Serikali ya Rwanda (Paul Kagame). Baadaye kwenye mkutano wa Marais wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Paul Kagame alisema kuwa Waasi wanaopigana Nchini DR Congo, wote ni Wakongo (Wakongomani) huku akimnyooshea kidole Félix Tshisekedi kuwa anashindwa kusema hadharani kiini halisi cha mgogoro uliopo kati ya Waasi hao na DR Congo ambapo Kagame alidai kuwa kuna mikataba yao ambao hataki kuzungumzwa na Serikali ya DR Congo akiwemo Tshisekedi na wakijificha kwenye kichaka cha kwamba Rwanda ndio mfadhili wa Waasi hao.

Undani wa bifu kati Rais wa DR Congo 🇨🇩, Félix Tshisekedi na Kiongozi Mkuu wa Waasi wa M23, Corneille Nanga. Anaitwa Jenerali Corneille Nanga ambaye ni Kamanda Mkuu (Rais) wa makundi yote ya Waasi yanayopigana Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo likiwemo kundi la M23. Muungano huo unaitwa Congo River Allience na yeye ndio Kiongozi Mkuu na amesema malengo yao ni kuitwaa DR Congo yote mpaka Mji Mkuu Kinshasa. Muungano wa makundi hayo aliutangaza rasmi mwaka 2023. Ikumbukwe kwamba Corneille Nanga alikuwa Mtumishi wa ngazi za juu ndani ya Serikali ya DR Congo kwa miaka mingi akifanya kazi katika programu mbalimbali za umoja wa mataifa. Mwaka 2015 mpaka 2021 alikuwa Mkuu wa tume ya Taifa ya uchaguzi Nchini humo CENI (Commission Electoral Ingependence) na ndiye aliyemtangaza Rais Felix Tshisekedi mshindi wa urais katika uchaguzi mwaka 2018. Nanga alitofautiana na Mteuzi wake Rais mstaafu Joseph Kabila na Rais mpya Félix Tshisekedi kwamba kuna makubaliano walikubaliana katika uchaguzi wa 2018 ambapo anadai alichakachua uchaguzi kama Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi CENI na kumpa ushindi Tshisekedi ila baada ya ushindi Tshisekedi akageuka makubaliano yao. Tuhuma hizo Tshisekedi alizikanusha na kusema alishinda kihalali. Baada ya mvutano mkali hatimaye Nanga alikimbia Nchi na mwaka 2023 katika mkutano wake uhamishoni Jijini Nairobi alitangaza Muungano wa makundi (17) ya Waasi wote wanaopigana Mashariki mwa DR Congo ikiwemo kundi la M23 na Muungano huo ukapewa jina la Congo River Allience na yeye kuwa ndio Kiongozi Mkuu mkuu wa makundi yote. Wakati Nanga akiwa uhamishoni mahakama Kuu Jijini Kinshasa ilimuhukumu adhabu ya kifo akiwa hayupo mahakamani kwa kosa la uhaini. Kiufupi uasi wa DR Congo pakubwa umechangiwa na Uongozi mbovu, ukifuatilia mizizi ya mgogoro utagundua pia kuna mkataba Serikali ya Rais Laurent Kabila iliingia na jamii ya Watutsi Mashariki mwa DR Congo wakati wa kumpindua Rais wa zamani wa Nchi hiyo Mobutu Seseseko lakini baadaye akawageuka baada ya miaka mingi ya mvutano ndio ikaja kuundwa M23. Moja makubaliano yao yalikua ni Jamii hiyo ya Watutsi kumsaidia Rais wa zamani Laurent Désiré Kabila (Baba Mzazi wa Joseph Kabila) kumpindua Mobutu kisa Watutsi wapewe sehemu ya Mkoa wa Sud-Kivu na wawe Raia wa DR Congo baada ya kuonekana kukataliwa na Paul Kagame kwa madai kwamba ni mmojawapo ya makundi yaliyohusika na mauwaji ya kimbari mwaka 1994. Kundi hili la Waasi la M23, jana lilikanusha kwamba linaungwa mkono na Serikali ya Rwanda 🇷🇼 (Paul Kagame). Baadaye kwenye mkutano wa Marais wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Paul Kagame alisema kuwa Waasi wanaopigana Nchini DR Congo, wote ni Wakongo (Wakongomani) huku akimnyooshea kidole Félix Tshisekedi kuwa anashindwa kusema hadharani kiini halisi cha mgogoro uliopo kati ya Waasi hao na DR Congo ambapo Kagame alidai kuwa kuna mikataba yao ambao hataki kuzungumzwa na Serikali ya DR Congo akiwemo Tshisekedi na wakijificha kwenye kichaka cha kwamba Rwanda ndio mfadhili wa Waasi hao.
1 Yorumlar ·0 hisse senetleri ·148 Views