Jeshi la Uganda (UPDF) limesema Wanajeshi wake walioko Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo , watatafuta mbinu ya kujiimarisha kiulinzi ili kuyazuwia makundi mengine ya Waasi kuingia mashariki mwa Taifa hilo.

Hali inazidi kuwa tete mashariki mwa Kongo, huku Waasi wa kujndi la M23 wanaosemekana kuungwa mkono na Rwanda wakiendelea kuyadhibiti maeneo kadhaa ya eneo hilo ukiwemo Mji wa Goma, hali iliyoisababisha Uganda kupitia Jeshi lake kusema inataka kujipanga upya kiulinzi, katika eneo inayofanyia operesheni zake hadi mzozo huo wa DR Congo utakapotulia. Imesema nia yake ni kuyazuwia makundi mengine ya Waasi yasitumie mwanya wa vita kuingia mashariki mwa Taifa hilo. 

Nchi ya Uganda ina jukumu muhimu katika kanda hiyo. Inafanya kazi pamoja na Wanajeshi wa Kongo katika mpango wa Operesheni Shujaa dhidi ya makundi yaliyo na itikadi kali kama Allied Democratic Forces, ADF, ambalo limekuwa likifungamanishwa na kundi la dola la kiislamu. Lakini kando na hayo, Uganda pia imekuwa ikishutumiwa na Wataalamu wa Umoja wa Mataifa na mashirika mengine kwa kuwaunga mkono Waasi wa M23 kwa kuwaruhusu kutumia ardhi yake kupitisha silaha zake madai ambayo Uganda imeyakanusha vikali.

Jeshi la Uganda πŸ‡ΊπŸ‡¬ (UPDF) limesema Wanajeshi wake walioko Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo πŸ‡¨πŸ‡©, watatafuta mbinu ya kujiimarisha kiulinzi ili kuyazuwia makundi mengine ya Waasi kuingia mashariki mwa Taifa hilo. Hali inazidi kuwa tete mashariki mwa Kongo, huku Waasi wa kujndi la M23 wanaosemekana kuungwa mkono na Rwanda πŸ‡·πŸ‡Ό wakiendelea kuyadhibiti maeneo kadhaa ya eneo hilo ukiwemo Mji wa Goma, hali iliyoisababisha Uganda kupitia Jeshi lake kusema inataka kujipanga upya kiulinzi, katika eneo inayofanyia operesheni zake hadi mzozo huo wa DR Congo utakapotulia. Imesema nia yake ni kuyazuwia makundi mengine ya Waasi yasitumie mwanya wa vita kuingia mashariki mwa Taifa hilo.  Nchi ya Uganda ina jukumu muhimu katika kanda hiyo. Inafanya kazi pamoja na Wanajeshi wa Kongo katika mpango wa Operesheni Shujaa dhidi ya makundi yaliyo na itikadi kali kama Allied Democratic Forces, ADF, ambalo limekuwa likifungamanishwa na kundi la dola la kiislamu. Lakini kando na hayo, Uganda pia imekuwa ikishutumiwa na Wataalamu wa Umoja wa Mataifa na mashirika mengine kwa kuwaunga mkono Waasi wa M23 kwa kuwaruhusu kutumia ardhi yake kupitisha silaha zake madai ambayo Uganda imeyakanusha vikali.
0 Comments Β·0 Shares Β·41 Views