Kama utafuatilia kwa undani kinachoendelea Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo , lazima utagundua kuwa Nchi ya Kongo ilikua na kila sababu kuweza kudhibiti hali ya Mashariki mwa Taifa hilo ila kutokana na mipango mibovu na kutegemea misaada na uthaifu wa Viongozi wa Nchi akiwemo Raisi Félix Tshisekedi ndio maana waliodharauliwa sasa wanasonga mbele kwa namna isiyo ya kawaida.

Toka Rais Tshisekedi aingia madarakani mwaka 2018 ni mambo yapi ya kimkakati amefanya ili kuhakikisha anakomesha makundi ya uasi mashariki mwa Kongo utabaini hakuna, yeye anaongoza tu akiwa Kinshasa ukanda wa mashariki ni kama amewasusa hali imezidi kuwa mbaya. Hajafanikiwa kubadili upepo kwa namna yoyote sio kijeshi wala kimazungumzo.

Mojawapo ya jukumu kuu la Rais wa Nchi yoyote Duniani ni kuhakikisha usalama na amani ya Raia anaowaongoza, sasa Tshisekedi zaidi ya miaka saba (7) sasa yupo madarakani huku Raia wakiendelea kuteswa na vita Mashariki mwa Nchi hiyo huku yeye akiwa hana jipya alilofanya kama Rais kuwanusuru Raia wake, sasa hapo mnatarajia nini kama sio kuvamiwa?

Kilichotokea na kinachoelea kwa sasa hivi Nchini Kongo, Viongozi Wakuu wanapaswa kujilaumu wenyewe, maadui zao wanatumia udhaifu wa kimkakati na kufanikisha ajenda zao.Tshisekedi alipaswa baada ya kutwaa Urais tu angehakikisha nguvu kubwa na mipango anaelekeza Mashariki mwa Nchi kwa sababu kule ndipo kwenye changamoto kubwa Nchini Kongo ila hadi sasa anatoa hotuba za kuilaumu Rwanda tu, yeye hajaja na mpango kwamba amejipanga vipi kukomesha uasi eneo hilo la mashariki na kuweka amani ya kudumu.

Inashauriwa kabla ya kutaka uongozi wa juu wa Nchi, jipime kwanza. Je, wanafaa? utaweza majukumu? au unafikiri kuongoza Nchi ni rahisi tu kama kumsukuma Mlevi kwenye shimo!

Kwa kumalizia, kama Kongo ingekuwa na uongozi thabiti, wenye maono, nguvu, mipango na mikakati madhubuti kupitia tu Jeshi la ndani ilikua na uwezo wa kukomesha Maadui wote. Mipaka ya Kongo inaimgilika kama maji ya kunywa, misitu kama yote haina uangalizi au ulinzi wowote ule. Tuendelee kuiombea Nchi ya Kongo ipate kwanza Viongozi bora na sio bora Viongozi.

Kama utafuatilia kwa undani kinachoendelea Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo 🇨🇩, lazima utagundua kuwa Nchi ya Kongo ilikua na kila sababu kuweza kudhibiti hali ya Mashariki mwa Taifa hilo ila kutokana na mipango mibovu na kutegemea misaada na uthaifu wa Viongozi wa Nchi akiwemo Raisi Félix Tshisekedi ndio maana waliodharauliwa sasa wanasonga mbele kwa namna isiyo ya kawaida. Toka Rais Tshisekedi aingia madarakani mwaka 2018 ni mambo yapi ya kimkakati amefanya ili kuhakikisha anakomesha makundi ya uasi mashariki mwa Kongo utabaini hakuna, yeye anaongoza tu akiwa Kinshasa ukanda wa mashariki ni kama amewasusa hali imezidi kuwa mbaya. Hajafanikiwa kubadili upepo kwa namna yoyote sio kijeshi wala kimazungumzo. Mojawapo ya jukumu kuu la Rais wa Nchi yoyote Duniani ni kuhakikisha usalama na amani ya Raia anaowaongoza, sasa Tshisekedi zaidi ya miaka saba (7) sasa yupo madarakani huku Raia wakiendelea kuteswa na vita Mashariki mwa Nchi hiyo huku yeye akiwa hana jipya alilofanya kama Rais kuwanusuru Raia wake, sasa hapo mnatarajia nini kama sio kuvamiwa? Kilichotokea na kinachoelea kwa sasa hivi Nchini Kongo, Viongozi Wakuu wanapaswa kujilaumu wenyewe, maadui zao wanatumia udhaifu wa kimkakati na kufanikisha ajenda zao.Tshisekedi alipaswa baada ya kutwaa Urais tu angehakikisha nguvu kubwa na mipango anaelekeza Mashariki mwa Nchi kwa sababu kule ndipo kwenye changamoto kubwa Nchini Kongo ila hadi sasa anatoa hotuba za kuilaumu Rwanda tu, yeye hajaja na mpango kwamba amejipanga vipi kukomesha uasi eneo hilo la mashariki na kuweka amani ya kudumu. Inashauriwa kabla ya kutaka uongozi wa juu wa Nchi, jipime kwanza. Je, wanafaa? utaweza majukumu? au unafikiri kuongoza Nchi ni rahisi tu kama kumsukuma Mlevi kwenye shimo! Kwa kumalizia, kama Kongo ingekuwa na uongozi thabiti, wenye maono, nguvu, mipango na mikakati madhubuti kupitia tu Jeshi la ndani ilikua na uwezo wa kukomesha Maadui wote. Mipaka ya Kongo inaimgilika kama maji ya kunywa, misitu kama yote haina uangalizi au ulinzi wowote ule. Tuendelee kuiombea Nchi ya Kongo ipate kwanza Viongozi bora na sio bora Viongozi.
Like
1
· 0 Commentaires ·0 Parts ·57 Vue