"Mapema leo katika kazi jijini Dodoma ambapo nchi yetu imeandika historia kwa kuzindua Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 Toleo la 2023, pamoja na mitaala iliyoboreshwa katika ngazi ya Elimu ya Awali, Elimu ya Msingi, Elimu ya Sekondari na Elimu ya Ualimu.
Uamuzi huu wa kihistoria wa kuboresha sera na muundo wa elimu yetu unakusudia kulipa Taifa letu vijana wenye elimu bora zaidi, wanaojiamini zaidi, na wenye nyenzo stahiki kushindana kikanda na kimataifa. Kazi ya msingi ya ujenzi wa miundombinu inayobeba utekelezaji wa sera na mabadiliko haya inaendelea, ambapo katika kipindi cha mwaka 2021 hadi 2024 tumejenga shule mpya za msingi 1,649, shule mpya za sekondari 1,042, vyuo 64 vya ufundi stadi (VETA) katika wilaya 64 ambazo awali hazikuwa navyo.
Nimeelekeza Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Wizara ya Fedha, Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) na Wizara ya Mipango na Uwekezaji kusimamia kikamilifu utekelezaji wa mabadiliko haya ili yaweze kuleta manufaa tunayokusudia. Utekelezaji huu uende sambamba na kupitia upya maslahi ya kada ya ualimu nchini ili kuipa hadhi inayostahili kama mama wa taaluma zote duniani." Dk Samia Suluhu Hassan, rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania

0 Commentarios
·0 Acciones
·25 Views