Nchi ya Rwanda imekanusha taarifa ya madai iliyotolewa na Mkutano wa wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kuhusu uhusika wake na machafuko yanayoendelea Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia Congo . Licha ya kukanusha madai hayo, imeinyooshea kidole DR Congo ikiishutumu kutaka kuipindua Serikali ya Rwanda iliyopo madarakani.

Hayo yameelezwa leo Jumapili Februari 2, 2025 na taarifa iliyotolewa na kuchapishwa kwenye mtandao wa X wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Rwanda.

“Rwanda inakana shutuma dhidi ya Jeshi la Ulinzi la Rwanda (RDF) iliyotolewa katika taarifa ya Mkutano wa Kilele wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) uliofanyika Januari 31, 2025. RDF inatetea mipaka ya Rwanda dhidi ya vitisho na inalinda Raia, haishambulii Raia.

“SADC imetuma kikosi cha mashambulizi, SAMIDRC, kusaidia vita vya Serikali ya DRC dhidi ya Watu wake wenyewe - M23 na Wanachama wa Jumuiya yao - wengi wao wamekimbilia kama Wakimbizi Nchini Rwanda na katika kanda nzima. Serikali ya DRC pia ina nia ya kushambulia Rwanda na kupindua Serikali yake, kama ilivyosemwa mara kwa mara na hadharani na Rais Tshisekedi,” imesema taarifa hiyo.

Nchi ya Rwanda 🇷🇼 imekanusha taarifa ya madai iliyotolewa na Mkutano wa wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kuhusu uhusika wake na machafuko yanayoendelea Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia Congo 🇨🇩. Licha ya kukanusha madai hayo, imeinyooshea kidole DR Congo ikiishutumu kutaka kuipindua Serikali ya Rwanda iliyopo madarakani. Hayo yameelezwa leo Jumapili Februari 2, 2025 na taarifa iliyotolewa na kuchapishwa kwenye mtandao wa X wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Rwanda. “Rwanda inakana shutuma dhidi ya Jeshi la Ulinzi la Rwanda (RDF) iliyotolewa katika taarifa ya Mkutano wa Kilele wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) uliofanyika Januari 31, 2025. RDF inatetea mipaka ya Rwanda dhidi ya vitisho na inalinda Raia, haishambulii Raia. “SADC imetuma kikosi cha mashambulizi, SAMIDRC, kusaidia vita vya Serikali ya DRC dhidi ya Watu wake wenyewe - M23 na Wanachama wa Jumuiya yao - wengi wao wamekimbilia kama Wakimbizi Nchini Rwanda na katika kanda nzima. Serikali ya DRC pia ina nia ya kushambulia Rwanda na kupindua Serikali yake, kama ilivyosemwa mara kwa mara na hadharani na Rais Tshisekedi,” imesema taarifa hiyo.
Like
1
· 0 Yorumlar ·0 hisse senetleri ·24 Views