#PART7

Baada ya kundi la RCD kuvunjika, yalizaliwa makundi mawili ambayo ni RCD Goma (liliungwa mkono na Rwanda) na RCD Kisangani (likiungwa mkono na Uganda). Aliyekua Kiongozi wa RCD Ernest Wamba Dia Wamba akaamua kukaa pembeni baada ya kugundua wanatumika kupigana kwa maslahi ya watu wengine.

Kwahiyo makundi haya yakapata viongozi wapya. RCD-Goma ikaongozwa na Kanali Emile Ilunga na RCD-Kisangani, ikaongozwa na Jenerali Mbusa Nyamwisi. Ikumbukwe kabla kundi la RCD halijavunjika, lilikuwa limeshikilia maeneo mengi ya migodi huko Goma, Bukavu, na Katanga. Sasa baada ya kuvunjika, ukatokea mgogoro wa kugawana maeneo. Mgodi upi uende RCD Goma na upi uende RCD Kisangani.

Kwa hiyo wakaanza kupigana tena wao kwa wao. Ikapigwa vita moja kali sana pale Kisangani, ikabatizwa jina la ‘Six Day War’ maana ilipiganwa kwa siku sita. RCD-Goma, ikawatandika vibaya sana RCD-Kisangani. Tar.10 June 2000 RCD Kisangani ikaachia migodi yote na kukimbia. RCD-Goma wakataka RCD-Kisangani wabadili jina lao maana mji wa Kisangani haukuwa chini yao tena. Hatimaye, RCD-Kisangani wakabadili na kujiita RCD-ML, yaani Rally for Congolese Democracy - Liberation Movement.

RCD - ML walikimbilia kwenye milima Mikeno karibu na hifadhi ya Virunga kujipanga upya. RCD-Goma wakaendeleza mapigano kuelekea Kinshasa. Lakini kufika Bukavu wakakumbana na upinzani kutoka wanamgambo wa Maï-Maï waliokua wamepewa silaha na serikali za majimbo kupigana na askari yoyote mgeni kwenye ardhi yao.

Maï-Maï waliongozwa na Kanali Musa Sindi upande wa Kivu Kusini na Sheikh Ntabo Ntaberi kwa Kivu Kaskazini. Kwa hiyo safari ya RCD Goma kwenda Kinshasa kumng’oa Laurent Kabila ikakutana na kizuizi cha Maï-Maï. Wakachapana sana. Watu zaidi ya 1,000 wakapoteza maisha.

Kwahiyo vita ya kumng'oa Laurent Kabila ikawa ngumu maana vikundi vingi vya waasi vilianza kupigana vyenyewe kwa vyenyewe. Hali hiyo ilifanya vita kuwa ngumu zaidi, maana watu walipigana bila mpangilio. Risasi zikafyatuliwa hovyo hovyo na wananchi wengi wakapoteza maisha.
(Malisa GJ)

#PART7 Baada ya kundi la RCD kuvunjika, yalizaliwa makundi mawili ambayo ni RCD Goma (liliungwa mkono na Rwanda) na RCD Kisangani (likiungwa mkono na Uganda). Aliyekua Kiongozi wa RCD Ernest Wamba Dia Wamba akaamua kukaa pembeni baada ya kugundua wanatumika kupigana kwa maslahi ya watu wengine. Kwahiyo makundi haya yakapata viongozi wapya. RCD-Goma ikaongozwa na Kanali Emile Ilunga na RCD-Kisangani, ikaongozwa na Jenerali Mbusa Nyamwisi. Ikumbukwe kabla kundi la RCD halijavunjika, lilikuwa limeshikilia maeneo mengi ya migodi huko Goma, Bukavu, na Katanga. Sasa baada ya kuvunjika, ukatokea mgogoro wa kugawana maeneo. Mgodi upi uende RCD Goma na upi uende RCD Kisangani. Kwa hiyo wakaanza kupigana tena wao kwa wao. Ikapigwa vita moja kali sana pale Kisangani, ikabatizwa jina la ‘Six Day War’ maana ilipiganwa kwa siku sita. RCD-Goma, ikawatandika vibaya sana RCD-Kisangani. Tar.10 June 2000 RCD Kisangani ikaachia migodi yote na kukimbia. RCD-Goma wakataka RCD-Kisangani wabadili jina lao maana mji wa Kisangani haukuwa chini yao tena. Hatimaye, RCD-Kisangani wakabadili na kujiita RCD-ML, yaani Rally for Congolese Democracy - Liberation Movement. RCD - ML walikimbilia kwenye milima Mikeno karibu na hifadhi ya Virunga kujipanga upya. RCD-Goma wakaendeleza mapigano kuelekea Kinshasa. Lakini kufika Bukavu wakakumbana na upinzani kutoka wanamgambo wa Maï-Maï waliokua wamepewa silaha na serikali za majimbo kupigana na askari yoyote mgeni kwenye ardhi yao. Maï-Maï waliongozwa na Kanali Musa Sindi upande wa Kivu Kusini na Sheikh Ntabo Ntaberi kwa Kivu Kaskazini. Kwa hiyo safari ya RCD Goma kwenda Kinshasa kumng’oa Laurent Kabila ikakutana na kizuizi cha Maï-Maï. Wakachapana sana. Watu zaidi ya 1,000 wakapoteza maisha. Kwahiyo vita ya kumng'oa Laurent Kabila ikawa ngumu maana vikundi vingi vya waasi vilianza kupigana vyenyewe kwa vyenyewe. Hali hiyo ilifanya vita kuwa ngumu zaidi, maana watu walipigana bila mpangilio. Risasi zikafyatuliwa hovyo hovyo na wananchi wengi wakapoteza maisha. (Malisa GJ)
Like
1
· 0 Comments ·0 Shares ·393 Views