Chama cha Economic Freedom Fighters (EFF) cha Afrika Kusini kimeitaka Serikali ya Afrika Kusini kufunga ubalozi wa Rwanda Nchini humo, kikidai kuwa hakuna haja ya kuendeleza uhusiano wa kidiplomasia na nchi inayodhoofisha uhuru wa taifa hilo.

Akizungumza katika mkutano na Waandishi wa habari Jijini Johannesburg, Afrika Kusini, Jumatatu, Februari 3, 2025, Kiongozi wa EFF, Julius Malema, amemtaka Rais Cyril Ramaphosa kuchukua hatua kali dhidi ya Nchi ya Rwanda endapo itabainika imehusika katika shambulio dhidi ya Wanajeshi wa Afrika Kusini waliopo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwa shughuli za ulinzi wa amani.

"Haikubaliki kwa wanajeshi wetu kushiriki kwenye mzozo ambao hauleti amani katika eneo hilo. Kama itathibitishwa kuwa Rwanda ililenga vikosi vya Afrika Kusini kwa makusudi, basi Rais Cyril Ramaphosa lazima achukue hatua kali," Julius Malema, Kiongozi wa EFF.

Aidha, Malema amesisitiza kuwa Nchi ya Afrika Kusini inapaswa kuondoa Wanajeshi wake kutoka DR Congo mara moja na kusitisha makubaliano yote ya kibiashara na Rwanda.

"Iwapo Rwanda itathibitishwa kuhusika moja kwa moja katika mashambulizi dhidi ya wanajeshi wetu, basi makubaliano yote ya biashara na ushirikiano na nchi hiyo yafutwe mara moja. Ubalozi wa Rwanda unapaswa kufungwa bila kuchelewa," amemalizia kusema Malema.

Chama cha Economic Freedom Fighters (EFF) cha Afrika Kusini 🇿🇦 kimeitaka Serikali ya Afrika Kusini kufunga ubalozi wa Rwanda Nchini humo, kikidai kuwa hakuna haja ya kuendeleza uhusiano wa kidiplomasia na nchi inayodhoofisha uhuru wa taifa hilo. Akizungumza katika mkutano na Waandishi wa habari Jijini Johannesburg, Afrika Kusini, Jumatatu, Februari 3, 2025, Kiongozi wa EFF, Julius Malema, amemtaka Rais Cyril Ramaphosa kuchukua hatua kali dhidi ya Nchi ya Rwanda endapo itabainika imehusika katika shambulio dhidi ya Wanajeshi wa Afrika Kusini waliopo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo 🇨🇩 kwa shughuli za ulinzi wa amani. "Haikubaliki kwa wanajeshi wetu kushiriki kwenye mzozo ambao hauleti amani katika eneo hilo. Kama itathibitishwa kuwa Rwanda ililenga vikosi vya Afrika Kusini kwa makusudi, basi Rais Cyril Ramaphosa lazima achukue hatua kali," Julius Malema, Kiongozi wa EFF. Aidha, Malema amesisitiza kuwa Nchi ya Afrika Kusini inapaswa kuondoa Wanajeshi wake kutoka DR Congo mara moja na kusitisha makubaliano yote ya kibiashara na Rwanda. "Iwapo Rwanda itathibitishwa kuhusika moja kwa moja katika mashambulizi dhidi ya wanajeshi wetu, basi makubaliano yote ya biashara na ushirikiano na nchi hiyo yafutwe mara moja. Ubalozi wa Rwanda unapaswa kufungwa bila kuchelewa," amemalizia kusema Malema.
Like
2
· 0 Commentarios ·0 Acciones ·245 Views