#PART8

Kwahiyo wakati mapigano makali yakiendelea huko mashariki mwa Congo baina ya vikundi vya Waasi na wanamgambo wa Maimai, hali ikatulia mjini Kinshasa na Rais Kabila akapata nafasi ya kupumua kidogo. Maadui zako wakipigana wewe utafanya nini zaidi ya kunywa supu na chapati 2 kujipongeza?

Lakini alichosahau Kabila ni kwamba Kagame ni Jasusi mwandamizi. Wakati wa kusaini mkataba Lemera, Kagame alimchomekea "watu wake" kwenye kikosi chake cha ulinzi. Mmojawapo ni Luteni Rashid Kasereka, Mtutsi (Banyamulenge) wa Kivu Kusini. Januari 16, 2001, Luteni Kasereka alimfyatulia Rais Kabila risasi 4 za tumbo na kumuua papohapo.

Jumuiya ya kimataifa ikamtuhumu Kagame kuhusika, lakini akakanusha na kusema ni madai yasiyo na msingi. Baada ya kifo cha Mzee Kabila, mwanae Joseph akaapishwa kuwa Rais akiwa na miaka 29 tu. Joseph akafanya jitihada mbalimbali za kukomesha vita kwa kushirikisha Jumuiya ya kimataifa.

Julai 30, 2002, ukasainiwa Mkataba wa Pretoria (The Pretoria Agreement) uliotaka pande zote kusitisha mapigano. Desemba 17, 2002, ukasainiwa Mkataba mwingine ulioitwa Global &Inclusive Agreement (maarufu kama 2003 Peace Deal). Na hatimaye, Aprili 2, 2003, ukasainiwa Mkataba Maarufu wa Sun City Peace Agreement uliomaliza kabisa vita ya Congo.

Pamoja na mambo mengine, mkataba huo ulitaka kuondolewa kwa majeshi yote ya kigeni nchini Congo, kuwepo na utaratibu wa uchaguzi wa kidemokrasia, na kuwaingiza jeshini askari wa vikundi vya waasi. Mkataba huo ulihitimisha Vita vya Pili vya Congo. Vita mbaya mno katika historia. Vita hivi vilibatizwa jina "The Great war of Africa" kwa jinsi vilivyoshirikisha mataifa mengi, na jinsi vilivyoleta madhara makubwa kwa watu ikiwemo vifo vya zaidi ya watu 500,000.

Baada ya kumalizika kwa vita hivyo, Congo ikarudi kwenye amani, japokuwa kulikuwa na vikundi vidogo vya wanamgambo katika maeneo ya mashariki mwa nchi hiyo, hasa eneo la Kivu lakini makundi makubwa yote ya Waasi yalikubali kuweka silaha chini. Kuanzia mwaka 2003 hadi 2006 hali ikatulia kabisa. Kwa mara ya kwanza raia wa Congo wakalala pasi na kusikia milio ya risasi.!
(Malisa GJ)

#PART8 Kwahiyo wakati mapigano makali yakiendelea huko mashariki mwa Congo baina ya vikundi vya Waasi na wanamgambo wa Maimai, hali ikatulia mjini Kinshasa na Rais Kabila akapata nafasi ya kupumua kidogo. Maadui zako wakipigana wewe utafanya nini zaidi ya kunywa supu na chapati 2 kujipongeza? Lakini alichosahau Kabila ni kwamba Kagame ni Jasusi mwandamizi. Wakati wa kusaini mkataba Lemera, Kagame alimchomekea "watu wake" kwenye kikosi chake cha ulinzi. Mmojawapo ni Luteni Rashid Kasereka, Mtutsi (Banyamulenge) wa Kivu Kusini. Januari 16, 2001, Luteni Kasereka alimfyatulia Rais Kabila risasi 4 za tumbo na kumuua papohapo. Jumuiya ya kimataifa ikamtuhumu Kagame kuhusika, lakini akakanusha na kusema ni madai yasiyo na msingi. Baada ya kifo cha Mzee Kabila, mwanae Joseph akaapishwa kuwa Rais akiwa na miaka 29 tu. Joseph akafanya jitihada mbalimbali za kukomesha vita kwa kushirikisha Jumuiya ya kimataifa. Julai 30, 2002, ukasainiwa Mkataba wa Pretoria (The Pretoria Agreement) uliotaka pande zote kusitisha mapigano. Desemba 17, 2002, ukasainiwa Mkataba mwingine ulioitwa Global &Inclusive Agreement (maarufu kama 2003 Peace Deal). Na hatimaye, Aprili 2, 2003, ukasainiwa Mkataba Maarufu wa Sun City Peace Agreement uliomaliza kabisa vita ya Congo. Pamoja na mambo mengine, mkataba huo ulitaka kuondolewa kwa majeshi yote ya kigeni nchini Congo, kuwepo na utaratibu wa uchaguzi wa kidemokrasia, na kuwaingiza jeshini askari wa vikundi vya waasi. Mkataba huo ulihitimisha Vita vya Pili vya Congo. Vita mbaya mno katika historia. Vita hivi vilibatizwa jina "The Great war of Africa" kwa jinsi vilivyoshirikisha mataifa mengi, na jinsi vilivyoleta madhara makubwa kwa watu ikiwemo vifo vya zaidi ya watu 500,000. Baada ya kumalizika kwa vita hivyo, Congo ikarudi kwenye amani, japokuwa kulikuwa na vikundi vidogo vya wanamgambo katika maeneo ya mashariki mwa nchi hiyo, hasa eneo la Kivu lakini makundi makubwa yote ya Waasi yalikubali kuweka silaha chini. Kuanzia mwaka 2003 hadi 2006 hali ikatulia kabisa. Kwa mara ya kwanza raia wa Congo wakalala pasi na kusikia milio ya risasi.! (Malisa GJ)
Like
1
· 0 Commenti ·0 condivisioni ·395 Views