Usichanganye hivi vitu viwili, ni tofauti sana. Mapenzi na upendo, hivi ni vitu tofauti. Mapenzi Yana utumwa lakini upendo una uhuru, mapenzi yana visasi lakini upendo una msamaha, mapenzi yanamiliki lakini upendo una utu, mapenzi yana mwisho lakini upendo ni wa milele.

Mahusiano ya mwanaume na mwanamke ni mapenzi siyo upendo. Huu ni muungano wa kimaslahi, utake usitake ni maslahi. Kila upande una maslahi yake na siyo upendo. Angalia wanavyohesabiana waliyofanyiana aidha mema au mabaya siku wanapoachana. Upendo huwa hauhesabu na hauna kumbukumbu kabisa.

Mtu akikuambia nilikupenda sana, wala usijione na hatia, huyo muongo mkubwa. Neno analotakiwa kusema ni "nilikuwa na hisia kali za mapenzi kwako". Huwezi kumpiga mtu unayempenda, wala huwezi kutamani apatwe na mabaya sababu amekuacha. Mtu unayempenda utamtakia mema hata kama kukuacha kwake kulikuumiza. Siku zote utamuunga mkono kwa lolote linalompa furaha na amani hata kama ni kukuacha.

Usichanganye upendo na mapenzi ni vitu tofauti. Upendo ni nishati ya asili inayoishi ndani ya mtu lakini mapenzi ni hisia inayotokana na mvuto wa kimahaba.
Usichanganye hivi vitu viwili, ni tofauti sana. Mapenzi na upendo, hivi ni vitu tofauti. Mapenzi Yana utumwa lakini upendo una uhuru, mapenzi yana visasi lakini upendo una msamaha, mapenzi yanamiliki lakini upendo una utu, mapenzi yana mwisho lakini upendo ni wa milele. Mahusiano ya mwanaume na mwanamke ni mapenzi siyo upendo. Huu ni muungano wa kimaslahi, utake usitake ni maslahi. Kila upande una maslahi yake na siyo upendo. Angalia wanavyohesabiana waliyofanyiana aidha mema au mabaya siku wanapoachana. Upendo huwa hauhesabu na hauna kumbukumbu kabisa. Mtu akikuambia nilikupenda sana, wala usijione na hatia, huyo muongo mkubwa. Neno analotakiwa kusema ni "nilikuwa na hisia kali za mapenzi kwako". Huwezi kumpiga mtu unayempenda, wala huwezi kutamani apatwe na mabaya sababu amekuacha. Mtu unayempenda utamtakia mema hata kama kukuacha kwake kulikuumiza. Siku zote utamuunga mkono kwa lolote linalompa furaha na amani hata kama ni kukuacha. Usichanganye upendo na mapenzi ni vitu tofauti. Upendo ni nishati ya asili inayoishi ndani ya mtu lakini mapenzi ni hisia inayotokana na mvuto wa kimahaba.
Like
1
· 0 Comentários ·0 Compartilhamentos ·466 Visualizações