Rais wa Rwanda , Paul Kagame amesema kuwa hajui kama Wanajeshi wa Nchi yake wako mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), ambako mapigano kati ya kundi la Waasi la M23 na Wanajeshi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo yanaendelea.

Rais huyo ameyaomba hayo jana Februari 3, alipohojiwa na Mwandishi Larry Madowo wa CNN aliyetaka kufahamu ikiwa hadi kufikia jana kulikuwa na Vikosi vya kijeshi vya Rwanda Nchini Kongo. Licha ya kuwa Amiri Jeshi Mkuu amesema hajui.

"Sijui. Ni kweli mimi ni Amiri Jeshi Mkuu ila kuna vitu vingi ambavyo sivifahamu, ila kama utaniuliza kama kuna tatizo Kongo linaloihusu Rwanda na kwamba Rwanda inapaswa kufanya chochote ili kujilinda nitakwambia asilimia mia moja," Paul Kagame, Rais wa Rwanda.

Majibu ya Kagame yanakuja katika kipindi ambacho sehemu kubwa ya Jumuiya ya kimataifa inaamini kuwa Rwanda inawaunga mkono Waasi wa M23, waliodai kuuteka Mji wa Goma mashariki mwa Kongo wiki iliyopita.

Wataalamu wa Umoja wa Mataifa wanaamini kuwa takribani Wanajeshi 3,000 - 4,000 wa Rwanda wanawasimamia na kuwaunga mkono wapiganaji wa M23 mashariki mwa DR Congo. Ikinukuu Shirika la Afya Ulimwenguni, Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu katika ripoti ya Jumatatu ilidai kuwa kufikia tarehe 31 Januari, takribani miili 900 imepatikana kutoka mitaani.

Rais wa Rwanda 🇷🇼, Paul Kagame amesema kuwa hajui kama Wanajeshi wa Nchi yake wako mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), ambako mapigano kati ya kundi la Waasi la M23 na Wanajeshi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo 🇨🇩 yanaendelea. Rais huyo ameyaomba hayo jana Februari 3, alipohojiwa na Mwandishi Larry Madowo wa CNN aliyetaka kufahamu ikiwa hadi kufikia jana kulikuwa na Vikosi vya kijeshi vya Rwanda Nchini Kongo. Licha ya kuwa Amiri Jeshi Mkuu amesema hajui. "Sijui. Ni kweli mimi ni Amiri Jeshi Mkuu ila kuna vitu vingi ambavyo sivifahamu, ila kama utaniuliza kama kuna tatizo Kongo linaloihusu Rwanda na kwamba Rwanda inapaswa kufanya chochote ili kujilinda nitakwambia asilimia mia moja," Paul Kagame, Rais wa Rwanda. Majibu ya Kagame yanakuja katika kipindi ambacho sehemu kubwa ya Jumuiya ya kimataifa inaamini kuwa Rwanda inawaunga mkono Waasi wa M23, waliodai kuuteka Mji wa Goma mashariki mwa Kongo wiki iliyopita. Wataalamu wa Umoja wa Mataifa wanaamini kuwa takribani Wanajeshi 3,000 - 4,000 wa Rwanda wanawasimamia na kuwaunga mkono wapiganaji wa M23 mashariki mwa DR Congo. Ikinukuu Shirika la Afya Ulimwenguni, Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu katika ripoti ya Jumatatu ilidai kuwa kufikia tarehe 31 Januari, takribani miili 900 imepatikana kutoka mitaani.
0 Σχόλια ·0 Μοιράστηκε ·300 Views