Rais wa Marekani , Donald Trump amesaini amri ya utendaji kuiondoa rasmi Nchi ya Marekani kutoka Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa (UNHRC) na Shirika la Misaada na Kazi la Umoja wa Mataifa kwa Wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA).

Aidha, ameagiza mapitio ya ushiriki wa Marekani katika Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO). Hatua hiyo ilifanyika Februari 4, 2025, ambapo kipande cha video fupi kilichowekwa kwenye mtandao wa X wa Rais Trump kilionyesha Katibu wa Wafanyakazi wa Ikulu ya White House, Will Scharf, akimkabidhi Rais agizo hilo kwa ajili ya kutia saini.

"Kwa kuzingatia hatua nyingi zilizochukuliwa na mashirika kadhaa ya Umoja wa Mataifa ambazo zimeonyesha upendeleo mkubwa wa chuki dhidi ya Marekani, tuna agizo la utendaji lililotayarishwa kwa ajili yako ambalo lingeiondoa Marekani kutoka UNHRC na UNRWA, huku pia likipitia upya ushiriki wetu katika UNESCO." amesema Will Scharf kama sababu ya Donald Trump kuamua kujiondoa kwenye Mashirika hayo.

Ameongeza kuwa agizo hilo pia linaelekeza ukaguzi wa kina wa ushiriki wa Marekani katika Umoja wa Mataifa kwa ujumla, hususan kuhusu tofaudi kubwa za ufadhili zinazotolewa na Marekani ikilinganishwa na mataifa mengine ambayo "hayatendei haki Marekani".

Rais wa Marekani 🇺🇸, Donald Trump amesaini amri ya utendaji kuiondoa rasmi Nchi ya Marekani kutoka Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa (UNHRC) na Shirika la Misaada na Kazi la Umoja wa Mataifa kwa Wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA). Aidha, ameagiza mapitio ya ushiriki wa Marekani katika Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO). Hatua hiyo ilifanyika Februari 4, 2025, ambapo kipande cha video fupi kilichowekwa kwenye mtandao wa X wa Rais Trump kilionyesha Katibu wa Wafanyakazi wa Ikulu ya White House, Will Scharf, akimkabidhi Rais agizo hilo kwa ajili ya kutia saini. "Kwa kuzingatia hatua nyingi zilizochukuliwa na mashirika kadhaa ya Umoja wa Mataifa ambazo zimeonyesha upendeleo mkubwa wa chuki dhidi ya Marekani, tuna agizo la utendaji lililotayarishwa kwa ajili yako ambalo lingeiondoa Marekani kutoka UNHRC na UNRWA, huku pia likipitia upya ushiriki wetu katika UNESCO." amesema Will Scharf kama sababu ya Donald Trump kuamua kujiondoa kwenye Mashirika hayo. Ameongeza kuwa agizo hilo pia linaelekeza ukaguzi wa kina wa ushiriki wa Marekani katika Umoja wa Mataifa kwa ujumla, hususan kuhusu tofaudi kubwa za ufadhili zinazotolewa na Marekani ikilinganishwa na mataifa mengine ambayo "hayatendei haki Marekani".
0 Comentários ·0 Compartilhamentos ·163 Visualizações