Katika uteuzi huo, pia wamemteua Meya wa Jiji la Goma pamoja na Wakuu wa Wilaya mbalimbali.

Hatua hii inakuja wakati maeneo kama Walikale, Lubero, na Beni bado yako chini ya udhibiti wa serikali ya DRC inayoongozwa na Félix Tshisekedi.

M23, kundi la waasi lenye silaha nzito na za kisasa, linadai kuwa linapigania haki za jamii ya Watutsi wa Congo.

Jamii ya Watutsi waishio Congo mara nyingi hutengwa, huku serikali ya DRC ikiwatambua kama Wanyarwanda wanaoishi nchini humo.

Taasisi mbalimbali za kitaifa na kimataifa, zikiwemo Umoja wa Mataifa na serikali ya DRC, zinadai kuwa kundi hili linaungwa mkono na Rwanda kwa maslahi ya kiuchumi na kisiasa.

Hata hivyo, M23 wamekanusha vikali tuhuma hizo, wakisisitiza kuwa hawapokei msaada wa kijeshi kutoka Rwanda na kwamba wanapigana kwa maslahi yao wenyewe..

Katika uteuzi huo, pia wamemteua Meya wa Jiji la Goma pamoja na Wakuu wa Wilaya mbalimbali. Hatua hii inakuja wakati maeneo kama Walikale, Lubero, na Beni bado yako chini ya udhibiti wa serikali ya DRC inayoongozwa na Félix Tshisekedi. M23, kundi la waasi lenye silaha nzito na za kisasa, linadai kuwa linapigania haki za jamii ya Watutsi wa Congo. Jamii ya Watutsi waishio Congo mara nyingi hutengwa, huku serikali ya DRC ikiwatambua kama Wanyarwanda wanaoishi nchini humo. Taasisi mbalimbali za kitaifa na kimataifa, zikiwemo Umoja wa Mataifa na serikali ya DRC, zinadai kuwa kundi hili linaungwa mkono na Rwanda kwa maslahi ya kiuchumi na kisiasa. Hata hivyo, M23 wamekanusha vikali tuhuma hizo, wakisisitiza kuwa hawapokei msaada wa kijeshi kutoka Rwanda na kwamba wanapigana kwa maslahi yao wenyewe..
0 Commentaires ·0 Parts ·217 Vue