Uamuzi huo ulizua sintofahamu kubwa, kwani upinzani ulidai kuwa matokeo hayo yalikuwa na mizengwe.

Wapo waliodai kuwa Nangaa alihusika moja kwa moja kuhakikisha Tshisekedi anashinda ili kumaliza utawala wa muda mrefu wa Joseph Kabila.

Lakini wakati watu walidhani kuwa jukumu lake katika siasa za Congo limeishia hapo, mambo yalibadilika ghafla.

Badala ya kustaafu kwenye siasa, Corneille Nangaa aliibuka na Action for Change (AFC), chama kipya cha kisiasa ambacho kilionekana kuja na ajenda tofauti.

Alianza kujenga ushawishi mkubwa ndani na nje ya Congo, huku akijitokeza kama mpinzani wa utawala wa Tshisekedi aliyechangia kumuweka madarakani.

Lakini hatua iliyotikisa Congo ni pale ilipogundulika kuwa Nangaa sasa alikuwa na uhusiano wa karibu na kundi la waasi la M23, ambalo linajulikana kwa mapigano yake dhidi ya serikali ya Congo.

Kwa muda mrefu, kundi la M23 limekuwa likipambana na serikali, likidai haki kwa jamii ya Watutsi wa Congo.

Lakini sasa, kulikuwa na mabadiliko makubwa M23, haikuwa tu kundi la waasi, bali lilionekana kama jeshi binafsi la Corneille Nangaa.

Uamuzi huo ulizua sintofahamu kubwa, kwani upinzani ulidai kuwa matokeo hayo yalikuwa na mizengwe. Wapo waliodai kuwa Nangaa alihusika moja kwa moja kuhakikisha Tshisekedi anashinda ili kumaliza utawala wa muda mrefu wa Joseph Kabila. Lakini wakati watu walidhani kuwa jukumu lake katika siasa za Congo limeishia hapo, mambo yalibadilika ghafla. Badala ya kustaafu kwenye siasa, Corneille Nangaa aliibuka na Action for Change (AFC), chama kipya cha kisiasa ambacho kilionekana kuja na ajenda tofauti. Alianza kujenga ushawishi mkubwa ndani na nje ya Congo, huku akijitokeza kama mpinzani wa utawala wa Tshisekedi aliyechangia kumuweka madarakani. Lakini hatua iliyotikisa Congo ni pale ilipogundulika kuwa Nangaa sasa alikuwa na uhusiano wa karibu na kundi la waasi la M23, ambalo linajulikana kwa mapigano yake dhidi ya serikali ya Congo. Kwa muda mrefu, kundi la M23 limekuwa likipambana na serikali, likidai haki kwa jamii ya Watutsi wa Congo. Lakini sasa, kulikuwa na mabadiliko makubwa M23, haikuwa tu kundi la waasi, bali lilionekana kama jeshi binafsi la Corneille Nangaa.
Like
1
· 0 Comentários ·0 Compartilhamentos ·105 Visualizações