Kuna gereza, na kuna Guantanamo Bay.

Hili si gereza la kawaida. Ni shimo la mateso, mahali ambapo sheria za haki za binadamu zinaonekana kama hadithi za kufikirika.

Lipo Cuba, lakini linamilikiwa na Marekani.

Wanasema gereza ni sehemu ya kutumikia adhabu, lakini Guantanamo ni sehemu ambapo unatakiwa kusahau kama ulikuwa binadamu.

Kama umewekwa hapa, ni ishara kwamba dunia imeshakusahau.
Na hata kama hauna hatia, hutaweza kuthibitisha chochote.

Marekani ni taifa la haki, Ndio! angalau kwenye makaratasi.
Lakini hata Wamarekani wenyewe walikuwa hawapendi Guantanamo.

Kila mwaka, wanaharakati wa haki za binadamu walikuwa wakiandamana, wakitaka gereza hilo lifungwe.

Ilipofika mwaka 2008, Barack Obama alipoingia kwenye kinyang'anyiro cha urais, akaahidi jambo moja kubwa.

"Nikichaguliwa kuwa Rais, gereza la Guantanamo litafungwa mara moja!"

Ilionekana kama ahadi ya kweli.

Wamarekani wakashangilia, wakaamini kwamba hatimaye heshima ya taifa lao itarudi.
Kuna gereza, na kuna Guantanamo Bay. Hili si gereza la kawaida. Ni shimo la mateso, mahali ambapo sheria za haki za binadamu zinaonekana kama hadithi za kufikirika. Lipo Cuba, lakini linamilikiwa na Marekani. Wanasema gereza ni sehemu ya kutumikia adhabu, lakini Guantanamo ni sehemu ambapo unatakiwa kusahau kama ulikuwa binadamu. Kama umewekwa hapa, ni ishara kwamba dunia imeshakusahau. Na hata kama hauna hatia, hutaweza kuthibitisha chochote. Marekani ni taifa la haki, Ndio! angalau kwenye makaratasi. Lakini hata Wamarekani wenyewe walikuwa hawapendi Guantanamo. Kila mwaka, wanaharakati wa haki za binadamu walikuwa wakiandamana, wakitaka gereza hilo lifungwe. Ilipofika mwaka 2008, Barack Obama alipoingia kwenye kinyang'anyiro cha urais, akaahidi jambo moja kubwa. "Nikichaguliwa kuwa Rais, gereza la Guantanamo litafungwa mara moja!" Ilionekana kama ahadi ya kweli. Wamarekani wakashangilia, wakaamini kwamba hatimaye heshima ya taifa lao itarudi.
0 التعليقات ·0 المشاركات ·19 مشاهدة