Rwanda inalichukulia jeshi la Burundi kama tishio jingine la usalama katika eneo la mashariki mwa Jamhuri ya demokrasi ya Congo (DRC).

Nchi inayopakana na Rwanda na DRC imekuwa na maelfu ya wanajeshi huko kwa miaka mingi.

Walikwenda kuwafuatilia waasi wa Burundi lakini sasa wanasaidia jeshi la Kinshasa katika vita dhidi ya M23.

Uhusiano kati ya Rwanda na Burundi ni mbaya.

Nchi hizi mbili zina muundo wa kikabila unaofanana lakini kinyume na Rwanda, Hutu ndiyo wanaoshikilia madaraka nchini Burundi.

Nchi zote mbili zimekashifiana kwa kudai kujaribu kuangusha serikali zao.

Rais wa Burundi, Evariste Ndayishimiye, ametoa onyo kali kwenye mitandao ya kijamii.

"Ikizidi, Rwanda itaendelea na mashambulizi," aliandika, "Najua vita vitafika Burundi… Siku moja atataka kuingia Burundi - hatutakubaliana na hilo. Vita vitapanuka."

Tishio hili litakuwa kubwa zaidi ikiwa M23 itaendelea na mashambulizi kutoka Goma kuelekea mkoa wa Kivu kusini karibu na mpaka wa Burundi, ambapo vikosi vyake viko.

"Kile kinachotafutwa na Burundi hapa ni kuokoa utawala wake," alisema Bw. Stearns.

"Burundi inahofia kuwa kama vikosi vya Rwanda vitaimarisha ushawishi wao katika eneo la Kivu kusini, inaweza kuteteresha serikali ya Bujumbura. Kile kilicho hatarini hapa ni kuzima uasi huu kabla haujaingilia karibu zaidi."

Wengine wanahofia kurudi kwa vita mbili zilizoshambulia eneo hilo mwishoni mwa miaka ya 1990, ambazo zilihusisha nchi tisa na kusababisha vifo vya mamilioni ya watu.

Mara hii, mapigano ya moja kwa moja kati ya majeshi mawili yanaweza kupelekea mgogoro wa DRC kuvuka nje ya mipaka yake.
(BBC Swahili)

Rwanda inalichukulia jeshi la Burundi kama tishio jingine la usalama katika eneo la mashariki mwa Jamhuri ya demokrasi ya Congo (DRC). Nchi inayopakana na Rwanda na DRC imekuwa na maelfu ya wanajeshi huko kwa miaka mingi. Walikwenda kuwafuatilia waasi wa Burundi lakini sasa wanasaidia jeshi la Kinshasa katika vita dhidi ya M23. Uhusiano kati ya Rwanda na Burundi ni mbaya. Nchi hizi mbili zina muundo wa kikabila unaofanana lakini kinyume na Rwanda, Hutu ndiyo wanaoshikilia madaraka nchini Burundi. Nchi zote mbili zimekashifiana kwa kudai kujaribu kuangusha serikali zao. Rais wa Burundi, Evariste Ndayishimiye, ametoa onyo kali kwenye mitandao ya kijamii. "Ikizidi, Rwanda itaendelea na mashambulizi," aliandika, "Najua vita vitafika Burundi… Siku moja atataka kuingia Burundi - hatutakubaliana na hilo. Vita vitapanuka." Tishio hili litakuwa kubwa zaidi ikiwa M23 itaendelea na mashambulizi kutoka Goma kuelekea mkoa wa Kivu kusini karibu na mpaka wa Burundi, ambapo vikosi vyake viko. "Kile kinachotafutwa na Burundi hapa ni kuokoa utawala wake," alisema Bw. Stearns. "Burundi inahofia kuwa kama vikosi vya Rwanda vitaimarisha ushawishi wao katika eneo la Kivu kusini, inaweza kuteteresha serikali ya Bujumbura. Kile kilicho hatarini hapa ni kuzima uasi huu kabla haujaingilia karibu zaidi." Wengine wanahofia kurudi kwa vita mbili zilizoshambulia eneo hilo mwishoni mwa miaka ya 1990, ambazo zilihusisha nchi tisa na kusababisha vifo vya mamilioni ya watu. Mara hii, mapigano ya moja kwa moja kati ya majeshi mawili yanaweza kupelekea mgogoro wa DRC kuvuka nje ya mipaka yake. (BBC Swahili)
0 Reacties ·0 aandelen ·23 Views