Kwa mujibu wa The Citizens, zaidi ya kampuni tano (5) za kigeni kutoka Nchini Ufaransa na Misri pamoja na Wawekezaji wa ndani ya Tanzania , wameonyesha nia ya kuwekeza katika usafirishaji wa nyaya yaani "cable" kwa lugha ya Kiingereza. Ili kufanikisha hilo sasa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Ardhini (LATRA) inakamilisha Kanuni za Usafiri wa Waya za Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini za Mwaka, 2024 katika ngazi ya Serikali.

Kanuni zingine zinazoendelea zinazopendekezwa ni pamoja na Kanuni za LATRA (Utoaji Leseni kwa Waendeshaji Reli) 2024 na Kanuni ya Utoaji Leseni ya Usafiri (Leseni ya Kipekee ya Usafiri wa Umma), 2024. Mkuu wa Idara ya Uhusiano na Mawasiliano wa LATRA, Salum Pazzy ameiambia The Citizen kwamba kampuni mbili kutoka Ufaransa na moja kutoka Misri zimejitokeza zikisubiri idhini ya kuwekeza katika sekta hiyo.

Kampuni hizi zimewasilisha mapendekezo yao na yanasubiri kuidhinishwa kwa kanuni ili kujihakikishia mazingira mazuri kwani usafiri wa waya unaonekana kuwa fursa kubwa ya kiuwekezaji.

Kwa mujibu wa The Citizens, zaidi ya kampuni tano (5) za kigeni kutoka Nchini Ufaransa 🇫🇷 na Misri 🇪🇬 pamoja na Wawekezaji wa ndani ya Tanzania 🇹🇿, wameonyesha nia ya kuwekeza katika usafirishaji wa nyaya yaani "cable" kwa lugha ya Kiingereza. Ili kufanikisha hilo sasa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Ardhini (LATRA) inakamilisha Kanuni za Usafiri wa Waya za Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini za Mwaka, 2024 katika ngazi ya Serikali. Kanuni zingine zinazoendelea zinazopendekezwa ni pamoja na Kanuni za LATRA (Utoaji Leseni kwa Waendeshaji Reli) 2024 na Kanuni ya Utoaji Leseni ya Usafiri (Leseni ya Kipekee ya Usafiri wa Umma), 2024. Mkuu wa Idara ya Uhusiano na Mawasiliano wa LATRA, Salum Pazzy ameiambia The Citizen kwamba kampuni mbili kutoka Ufaransa na moja kutoka Misri zimejitokeza zikisubiri idhini ya kuwekeza katika sekta hiyo. Kampuni hizi zimewasilisha mapendekezo yao na yanasubiri kuidhinishwa kwa kanuni ili kujihakikishia mazingira mazuri kwani usafiri wa waya unaonekana kuwa fursa kubwa ya kiuwekezaji.
Like
Love
2
· 0 Yorumlar ·0 hisse senetleri ·151 Views