Waziri Mkuu wa Israel , Benjamin Netanyahu, amefikishwa mbele ya mahakama Jijini Tel Aviv kujibu mashtaka ya muda mrefu ya rushwa. Waziri huyo aliwasili akiwa na Timu yake ya Mawakili inayoongozwa na Amit Hadad, baada ya kuamriwa kutoa ushahidi katika kesi tatu (3) za rushwa za mwaka 2019, zinazohusisha zawadi kutoka kwa Marafiki Mamilionea na madai ya kutafuta hisani kutoka kwa Matajiri wa vyombo vya habari kwa kubadilishana na fursa bora ya utangazaji.

Hata hivyo, Netanyahu amekana mashtaka yote yanayomkabili. Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu (75) ameweka rekodi ya kuwa Waziri Mkuu wa kwanza Nchini humo kushtakiwa kwa uhalifu.

Waziri Mkuu wa Israel 🇮🇱, Benjamin Netanyahu, amefikishwa mbele ya mahakama Jijini Tel Aviv kujibu mashtaka ya muda mrefu ya rushwa. Waziri huyo aliwasili akiwa na Timu yake ya Mawakili inayoongozwa na Amit Hadad, baada ya kuamriwa kutoa ushahidi katika kesi tatu (3) za rushwa za mwaka 2019, zinazohusisha zawadi kutoka kwa Marafiki Mamilionea na madai ya kutafuta hisani kutoka kwa Matajiri wa vyombo vya habari kwa kubadilishana na fursa bora ya utangazaji. Hata hivyo, Netanyahu amekana mashtaka yote yanayomkabili. Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu (75) ameweka rekodi ya kuwa Waziri Mkuu wa kwanza Nchini humo kushtakiwa kwa uhalifu.
Love
Wow
2
· 0 Σχόλια ·0 Μοιράστηκε ·81 Views