Rais wa Marekani , Donald Trump ameonya kuwa kama kundi la Hamas (Gaza) hawatawaachilia mateka wote wa Nchi ya Israel kufikia Jumamosi ya Wiki hii basi Dunia itashuhudia mashambulizi halisi katika eneo hilo. Onyo la Trump linakuja siku moja baada ya Kundi la Wapiganaji wa Hamas kuvunja makubaliano ya usitishwaji vita na Israel kwa kugoma kuendelea na zoezi la kuwaachia huru mateka wa Israel mpaka watakapotoa taarifa nyingine.

Uamuzi huo wa Hamas umekuja siku chache baada ya Viongozi wake Wakuu kufanya ziara Nchini Iran na kukutana na Kiongozi Mkuu wa Iran, Ayatollah Ali Khemenei ambaye aliwapongeza kwa kuendelea kusimama imara dhidi ya Israel. Trump wiki iliyopita alionya kuwa Gaza haitofaa kuwa eneo la kuishi chini ya Uongozi wa Hamas na kupendekeza kwamba Marekani ingependa kulichukua eneo hilo na kulisimamia huku Wakazi wa eneo hilo wakihamishiwa Nchi za Misri na Jordan .

Rais huyo wa Marekani alisema Marekani ipo tayari kulinunua eneo hilo na kulimiliki na kuahidi kwamba Marekani italijenga na kulifanya kuwa eneo zuri la mfano Mashariki ya Kati. Kiufupi kundi la Hamas wanacheza na moto kwa sasa, Waziri wa ulinzi wa Israel, Israel Katz ameviagiza Vikosi vya Israel kukaa tayari kwa mashambulizi mapya iwapo Kundi hilo la Hamas likigoma kutii maelekezo ya kuachia mateka.

Marekani ndio imekuwa Nchi inayoipa misaada mikubwa ya kibinadamu na kiuchumi Gaza pamoja na kuizuia Israel kutokuifutilia mbali Gaza kwa miaka mingi sasa ambapo Hamas imekua ikifanya uchokozi. Ikumbukwe Trump ni kati ya Viongozi wa Marekani ambaye ana msimamo mkali mno dhidi ya kundi la Hamas na tokea kuanza kwa mapigano Oktoba 7 mwaka 2023 Trump alisema Israel inachopaswa kufanya ni kulifutilia mbali kundi hilo.

Rais wa Marekani ๐Ÿ‡บ๐Ÿ‡ธ, Donald Trump ameonya kuwa kama kundi la Hamas (Gaza) hawatawaachilia mateka wote wa Nchi ya Israel ๐Ÿ‡ฎ๐Ÿ‡ฑ kufikia Jumamosi ya Wiki hii basi Dunia itashuhudia mashambulizi halisi katika eneo hilo. Onyo la Trump linakuja siku moja baada ya Kundi la Wapiganaji wa Hamas kuvunja makubaliano ya usitishwaji vita na Israel kwa kugoma kuendelea na zoezi la kuwaachia huru mateka wa Israel mpaka watakapotoa taarifa nyingine. Uamuzi huo wa Hamas umekuja siku chache baada ya Viongozi wake Wakuu kufanya ziara Nchini Iran ๐Ÿ‡ฎ๐Ÿ‡ท na kukutana na Kiongozi Mkuu wa Iran, Ayatollah Ali Khemenei ambaye aliwapongeza kwa kuendelea kusimama imara dhidi ya Israel. Trump wiki iliyopita alionya kuwa Gaza haitofaa kuwa eneo la kuishi chini ya Uongozi wa Hamas na kupendekeza kwamba Marekani ingependa kulichukua eneo hilo na kulisimamia huku Wakazi wa eneo hilo wakihamishiwa Nchi za Misri ๐Ÿ‡ช๐Ÿ‡ฌ na Jordan ๐Ÿ‡ฏ๐Ÿ‡ด. Rais huyo wa Marekani alisema Marekani ipo tayari kulinunua eneo hilo na kulimiliki na kuahidi kwamba Marekani italijenga na kulifanya kuwa eneo zuri la mfano Mashariki ya Kati. Kiufupi kundi la Hamas wanacheza na moto kwa sasa, Waziri wa ulinzi wa Israel, Israel Katz ameviagiza Vikosi vya Israel kukaa tayari kwa mashambulizi mapya iwapo Kundi hilo la Hamas likigoma kutii maelekezo ya kuachia mateka. Marekani ndio imekuwa Nchi inayoipa misaada mikubwa ya kibinadamu na kiuchumi Gaza pamoja na kuizuia Israel kutokuifutilia mbali Gaza kwa miaka mingi sasa ambapo Hamas imekua ikifanya uchokozi. Ikumbukwe Trump ni kati ya Viongozi wa Marekani ambaye ana msimamo mkali mno dhidi ya kundi la Hamas na tokea kuanza kwa mapigano Oktoba 7 mwaka 2023 Trump alisema Israel inachopaswa kufanya ni kulifutilia mbali kundi hilo.
Like
1
ยท 0 Comments ยท0 Shares ยท116 Views