Kikundi cha misaada cha Denmark kimetoa dola trilioni moja (1) kwa ajili ya kulinunua Jimbo la California Nchini Marekani siku chache baada ya Rais wa Marekani Donald Trump kusema anataka kulinunua eneo la Greenland lililoko Nchini Denmark. Raia Denmark hao ambao wameonesha kumkejeli Rais trump wamesema watasambaza keki za Denmark katika Jimbo hilo bila kikomo ikiwa wazo lao litapokelewa.

Trump amekuwa akijadili mara kwa mara kuhusu ununuzi wa Greenland eneo lenye uhuru la Denmark akionyesha thamani yake ya kimkakati na kiuchumi kwa Marekani. Hata hivyo, Maafisa wa Denmark na Greenland wamepinga vikali wazo hilo.

Trump amesisitiza anaweza kutumia nguvu za kijeshi na kiuchumi ili kupata eneo hilo. Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Marco Rubio, alisisitiza mwezi uliopita kwamba ununuzi wa Greenland ni lengo la kweli na "si jambo la kuchekesha."

Kikundi cha misaada cha Denmark 🇩🇰 kimetoa dola trilioni moja (1) kwa ajili ya kulinunua Jimbo la California Nchini Marekani 🇺🇸 siku chache baada ya Rais wa Marekani Donald Trump kusema anataka kulinunua eneo la Greenland lililoko Nchini Denmark. Raia Denmark hao ambao wameonesha kumkejeli Rais trump wamesema watasambaza keki za Denmark katika Jimbo hilo bila kikomo ikiwa wazo lao litapokelewa. Trump amekuwa akijadili mara kwa mara kuhusu ununuzi wa Greenland eneo lenye uhuru la Denmark akionyesha thamani yake ya kimkakati na kiuchumi kwa Marekani. Hata hivyo, Maafisa wa Denmark na Greenland wamepinga vikali wazo hilo. Trump amesisitiza anaweza kutumia nguvu za kijeshi na kiuchumi ili kupata eneo hilo. Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Marco Rubio, alisisitiza mwezi uliopita kwamba ununuzi wa Greenland ni lengo la kweli na "si jambo la kuchekesha."
Love
1
· 0 Commentaires ·0 Parts ·53 Vue