Habari iliyobamba kwa sasa kwenye vyombo vya habari ni ndoa ya Stephane Aziz Ki na Hamisa Mobetto, ingawa wapo waliofika mbali na kudai ni kiki tu kwa ajili ya matangazo ya bidhaa fulani na wanatumika tu.

Baada ya vuta nkuvute ya stori hii hatimaye mama yake Hamisa, Shufaa Rutanga amefunga na anathibitisha kuwepo kwa ndoa hiyo na kuhusu posa ya Aziz Ki, amesema hakuna posa yoyote iliyofika kwake kutoka kwa nyota huyo wa kimataifa wa Burkina Faso ingawa amepokea nyingi kutoka kwa wanaume tofauti wanaotaka kumuoa mwanaye.

“Sasa ngoja nikuambie ukweli, maana nilikuwa nashindwa kutoa majibu sahihi kutokana na baadhi ya ya vitu kuhusu ndoa hii vilikuwa havijakamilika, sasa vimekamilika na ndoa ipo. Kiukweli namshukuru Mungu maombi yangu kwa mwanagu yameitika, nilikuwa kila kukicha naomba apate mtu sahihi watakayependana ili aolewe, kuwa kwenye ndoa ni heshima kubwa sana" - Mama Mobetto

Mama Hamisa anasema hekaheka za ndoa hiyo zitaanza Jumamosi Februari 15 na ndiyo siku mahari itatolewa na sherehe itafanyika Februari 19, The Superdome, Masaki, jijini Dar es Salaam.

“Kutoka moyoni nimewapa baraka zote mkwe wangu AziZ Ki na mwanagu Hamisa na upendo mwingi sana kwake Aziz Ki kwa kupenda watoto wa Hamisa. Hiki ndiyo sababu kuu iliyonifanya nimpende zaidi Aziz Ki, maana kwa hali ya sasa hivi upate mwanamume atakayekubali kuoa mwanamke mwenye watoto ni wachache sana ila Aziz Ki ameonyesha upendo wa dhati kwa mwanangu Hamisa, kapenda boga na maua yake.” - Mama Mobetto

Wakati huohuo mmoja wa viongozi wa Yanga, amethibitisha ni kweli wawili hao watafunga ndoa Ijumaa na kwasasa Aziz yupo kwenye maandalizi ya Ndoa ingawa atakuwepo kwenye mchezo wa Ijumaa.
(Mwananchi)

Habari iliyobamba kwa sasa kwenye vyombo vya habari ni ndoa ya Stephane Aziz Ki na Hamisa Mobetto, ingawa wapo waliofika mbali na kudai ni kiki tu kwa ajili ya matangazo ya bidhaa fulani na wanatumika tu. Baada ya vuta nkuvute ya stori hii hatimaye mama yake Hamisa, Shufaa Rutanga amefunga na anathibitisha kuwepo kwa ndoa hiyo na kuhusu posa ya Aziz Ki, amesema hakuna posa yoyote iliyofika kwake kutoka kwa nyota huyo wa kimataifa wa Burkina Faso ingawa amepokea nyingi kutoka kwa wanaume tofauti wanaotaka kumuoa mwanaye. “Sasa ngoja nikuambie ukweli, maana nilikuwa nashindwa kutoa majibu sahihi kutokana na baadhi ya ya vitu kuhusu ndoa hii vilikuwa havijakamilika, sasa vimekamilika na ndoa ipo. Kiukweli namshukuru Mungu maombi yangu kwa mwanagu yameitika, nilikuwa kila kukicha naomba apate mtu sahihi watakayependana ili aolewe, kuwa kwenye ndoa ni heshima kubwa sana" - Mama Mobetto Mama Hamisa anasema hekaheka za ndoa hiyo zitaanza Jumamosi Februari 15 na ndiyo siku mahari itatolewa na sherehe itafanyika Februari 19, The Superdome, Masaki, jijini Dar es Salaam. “Kutoka moyoni nimewapa baraka zote mkwe wangu AziZ Ki na mwanagu Hamisa na upendo mwingi sana kwake Aziz Ki kwa kupenda watoto wa Hamisa. Hiki ndiyo sababu kuu iliyonifanya nimpende zaidi Aziz Ki, maana kwa hali ya sasa hivi upate mwanamume atakayekubali kuoa mwanamke mwenye watoto ni wachache sana ila Aziz Ki ameonyesha upendo wa dhati kwa mwanangu Hamisa, kapenda boga na maua yake.” - Mama Mobetto Wakati huohuo mmoja wa viongozi wa Yanga, amethibitisha ni kweli wawili hao watafunga ndoa Ijumaa na kwasasa Aziz yupo kwenye maandalizi ya Ndoa ingawa atakuwepo kwenye mchezo wa Ijumaa. (Mwananchi)
Like
1
· 0 Yorumlar ·0 hisse senetleri ·52 Views