Rais wa Rwanda , Paul Kagame ameweka wazi kuwa hana hofu na vitisho vya vikwazo vinavyotolewa na Mataifa ya Magharibi dhidi ya Nchi yake akisisitiza kuwa Rwanda itachukua hatua zozote zinazohitajika kulinda maslahi yake, akizungumza na Gazeti la Jeune Afrique, Kagame amezungumzia kwa kina mzozo kati ya Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo pamoja na shinikizo kutoka Ulaya na Marekani .

Kagame amesisitiza kuwa hatakubali mashinikizo yanayoelekezwa kwa Rwanda kwa lengo la kuidhoofisha akisema Nchi yake inayo haki ya kujilinda dhidi ya vitisho vyovyote vya nje ambapo Mataifa ya Magharibi yanaishutumu Rwanda kwa kuwaunga mkono kundi la Waasi wa M23 wanaopigana mashariki mwa DR Congo jambo ambalo Rwanda imekanusha mara kadhaa.

Kauli Kagame inakuja wakati mvutano kati ya Rwanda na DR Congo ukiendelea huku mataifa ya Magharibi yakitoa wito wa mazungumzo ya amani lakini licha ya hivyo Rwanda imeendelea kusisitiza kuwa haitakubali kushinikizwa kwa njia yoyote ikibainisha kuwa hatua zake zitalenga kulinda usalama wa Taifa lake kwa gharama yoyote.
(DW Swahili)

Rais wa Rwanda 🇷🇼, Paul Kagame ameweka wazi kuwa hana hofu na vitisho vya vikwazo vinavyotolewa na Mataifa ya Magharibi dhidi ya Nchi yake akisisitiza kuwa Rwanda itachukua hatua zozote zinazohitajika kulinda maslahi yake, akizungumza na Gazeti la Jeune Afrique, Kagame amezungumzia kwa kina mzozo kati ya Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo 🇨🇩 pamoja na shinikizo kutoka Ulaya na Marekani 🇺🇸. Kagame amesisitiza kuwa hatakubali mashinikizo yanayoelekezwa kwa Rwanda kwa lengo la kuidhoofisha akisema Nchi yake inayo haki ya kujilinda dhidi ya vitisho vyovyote vya nje ambapo Mataifa ya Magharibi yanaishutumu Rwanda kwa kuwaunga mkono kundi la Waasi wa M23 wanaopigana mashariki mwa DR Congo jambo ambalo Rwanda imekanusha mara kadhaa. Kauli Kagame inakuja wakati mvutano kati ya Rwanda na DR Congo ukiendelea huku mataifa ya Magharibi yakitoa wito wa mazungumzo ya amani lakini licha ya hivyo Rwanda imeendelea kusisitiza kuwa haitakubali kushinikizwa kwa njia yoyote ikibainisha kuwa hatua zake zitalenga kulinda usalama wa Taifa lake kwa gharama yoyote. (DW Swahili)
Love
1
· 0 Reacties ·0 aandelen ·105 Views