Kwa wapenzi wa saa, jina hili lina maana kubwa zaidi ya pesa. Richard Mille anajulikana kwa kutengeneza saa zenye muundo wa kipekee, teknolojia ya hali ya juu, na bei zinazoacha wengi wakishangaa.

Richard Mille Rockstar, ndivyo saa hii inavyoitwa. Na jina hilo si la bahati mbaya.

Ni saa iliyotengenezwa kwa ajili ya watu wenye hadhi ya kipekee, watu walio juu ya mfumo wa kawaida wa maisha, watu ambao majina yao ni alama ya mafanikio.

Ili kuelewa thamani ya saa hii, inabidi uelewe falsafa ya Richard Mille mwenyewe.

Anasema anapotengeneza saa, hatoi tu kifaa cha kuonesha muda, anatengeneza sanaa inayozungumza na nafsi ya aliyenayo.

Ndiyo maana saa zake ni za kipekee, na zinavaliwa na watu wa kipekee kama Jay Z.

Rockstar ni saa ya nadra sana. Duniani zipo mbili tu. Moja ipo kwa Jay Z, na nyingine iko kwa bilionea mmoja wa Asia ambaye jina lake linahifadhiwa kwa usiri mkubwa.

Hili ndilo linawafanya watu wengi waamini kwamba Jay Z si mtu wa kawaida. Wengi wanasema, “Hii ni ishara ya hadhi ya juu, ishara ya kuwa kwenye mzunguko wa watu wenye nguvu duniani.”

Shilingi bilioni 8.5. Hii si bei ya nyumba, wala si bei ya jumba la kifahari. Ni bei ya saa moja tu.
Kwa wapenzi wa saa, jina hili lina maana kubwa zaidi ya pesa. Richard Mille anajulikana kwa kutengeneza saa zenye muundo wa kipekee, teknolojia ya hali ya juu, na bei zinazoacha wengi wakishangaa. Richard Mille Rockstar, ndivyo saa hii inavyoitwa. Na jina hilo si la bahati mbaya. Ni saa iliyotengenezwa kwa ajili ya watu wenye hadhi ya kipekee, watu walio juu ya mfumo wa kawaida wa maisha, watu ambao majina yao ni alama ya mafanikio. Ili kuelewa thamani ya saa hii, inabidi uelewe falsafa ya Richard Mille mwenyewe. Anasema anapotengeneza saa, hatoi tu kifaa cha kuonesha muda, anatengeneza sanaa inayozungumza na nafsi ya aliyenayo. Ndiyo maana saa zake ni za kipekee, na zinavaliwa na watu wa kipekee kama Jay Z. Rockstar ni saa ya nadra sana. Duniani zipo mbili tu. Moja ipo kwa Jay Z, na nyingine iko kwa bilionea mmoja wa Asia ambaye jina lake linahifadhiwa kwa usiri mkubwa. Hili ndilo linawafanya watu wengi waamini kwamba Jay Z si mtu wa kawaida. Wengi wanasema, “Hii ni ishara ya hadhi ya juu, ishara ya kuwa kwenye mzunguko wa watu wenye nguvu duniani.” Shilingi bilioni 8.5. Hii si bei ya nyumba, wala si bei ya jumba la kifahari. Ni bei ya saa moja tu.
0 التعليقات ·0 المشاركات ·189 مشاهدة