Nikueleze kwa kifupi sana kiini cha mgogoro. Kabla ya mwaka 1991 Ukraine ilikua sehemu ya Urusi kupitia muungano wa kisovieti wa USSR. Baada ya USSR kufa ndipo taifa la Ukraine likazaliwa pamoja na mataifa mengine 14 yaliyokua majimbo ya Urusi.

Lakini usisahau mwaka 1949 umoja wa kujihami wa nchi za magharibi (NATO) ulianzishwa dhidi ya Urusi (USSR). Makubaliano yao ni kwamba ikiwa Urusi itamgusa mmoja wao basi wote watamvamia. Marekani akiwa kinara.

Kuanguka kwa USSR kukafanya mataifa 15 mapya kuzaliwa. Baadhi ya Mataifa hayo yakawa na hofu kuwa Urusi inaweza kurudi kuyakalia kimabavu. Kwahiyo yakaomba kujiunga NATO kwa usalama wao. Estonia, Latvia na Lithuania zikapata uanachana wa NATO chap kwa haraka. Ukraine ilipoomba uanachama Urusi ikakataa, kwa sababu ya strategic position ya Ukraine ambayo inaiweka Urusi hatarini.

Ukraine ilipokosa uanachama NATO ikamua kujilinda kwa kusuka mpango wa nyuklia. Marekani na Urusi zikashtuka. Kwa kutambua hatari ya nyuklia zikamsihi sana Ukraine aachane na mpango huo. Mwaka 1994 ukaandaliwa mkataba uitwao Budapest memorundum, huko Hungary. Mkataba huo ulihusisha nchi 4. Urusi na Ukraine zilisaini kwamba hakuna atakayemvamia mwenzake. Marekani na Uingereza zikasaini kwamba atakayemvamia mwenzake watampiga bila huruma. Pia Marekani na Uingereza zitagharamia fedha na vifaa vyote vya vita. Mkataba ukasainiwa na Ukraine ikasitisha mpango wake wa nyuklia.

Lakini Mwaka 2014 Urusi ikaivamia Ukraine na kuchukua jimbo lake la Crimea kimabavu. Marekani na Uingereza hazikuipiga Urusi kama mkataba wa Budapest unavyosema. Ukraine akalalamika lakini akapuuzwa. Kwenye vita inayoendelea sasa, Urusi ameshajitwalia majimbo manne Donetsk, Luhansk, Zaporizhzhia na Kherson lakini Marekani na Uingereza ziko kimya.

Ukraine inaona imesalitiwa. Mkataba wa Budapest ulikua kiini macho. Laiti Ukraine ingekataa kusaini na kuendelea na mpango wake wa nyuklia, leo Urusi isingethubutu kuigusa. Lakini Waliomdanganya sasa wamemgeuka na wanamfokea. Ukraine ingeyajua maneno ya Mzee Jomo Kenyatta "Learn to fight your own battle" isingeachana na mpango wake wa nyuklia mwaka 1994. Wangejifunza kupigana vita yao wenyewe bila kutegemea mtu.!
(Malisa GJ)

Nikueleze kwa kifupi sana kiini cha mgogoro. Kabla ya mwaka 1991 Ukraine ilikua sehemu ya Urusi kupitia muungano wa kisovieti wa USSR. Baada ya USSR kufa ndipo taifa la Ukraine likazaliwa pamoja na mataifa mengine 14 yaliyokua majimbo ya Urusi. Lakini usisahau mwaka 1949 umoja wa kujihami wa nchi za magharibi (NATO) ulianzishwa dhidi ya Urusi (USSR). Makubaliano yao ni kwamba ikiwa Urusi itamgusa mmoja wao basi wote watamvamia. Marekani akiwa kinara. Kuanguka kwa USSR kukafanya mataifa 15 mapya kuzaliwa. Baadhi ya Mataifa hayo yakawa na hofu kuwa Urusi inaweza kurudi kuyakalia kimabavu. Kwahiyo yakaomba kujiunga NATO kwa usalama wao. Estonia, Latvia na Lithuania zikapata uanachana wa NATO chap kwa haraka. Ukraine ilipoomba uanachama Urusi ikakataa, kwa sababu ya strategic position ya Ukraine ambayo inaiweka Urusi hatarini. Ukraine ilipokosa uanachama NATO ikamua kujilinda kwa kusuka mpango wa nyuklia. Marekani na Urusi zikashtuka. Kwa kutambua hatari ya nyuklia zikamsihi sana Ukraine aachane na mpango huo. Mwaka 1994 ukaandaliwa mkataba uitwao Budapest memorundum, huko Hungary. Mkataba huo ulihusisha nchi 4. Urusi na Ukraine zilisaini kwamba hakuna atakayemvamia mwenzake. Marekani na Uingereza zikasaini kwamba atakayemvamia mwenzake watampiga bila huruma. Pia Marekani na Uingereza zitagharamia fedha na vifaa vyote vya vita. Mkataba ukasainiwa na Ukraine ikasitisha mpango wake wa nyuklia. Lakini Mwaka 2014 Urusi ikaivamia Ukraine na kuchukua jimbo lake la Crimea kimabavu. Marekani na Uingereza hazikuipiga Urusi kama mkataba wa Budapest unavyosema. Ukraine akalalamika lakini akapuuzwa. Kwenye vita inayoendelea sasa, Urusi ameshajitwalia majimbo manne Donetsk, Luhansk, Zaporizhzhia na Kherson lakini Marekani na Uingereza ziko kimya. Ukraine inaona imesalitiwa. Mkataba wa Budapest ulikua kiini macho. Laiti Ukraine ingekataa kusaini na kuendelea na mpango wake wa nyuklia, leo Urusi isingethubutu kuigusa. Lakini Waliomdanganya sasa wamemgeuka na wanamfokea. Ukraine ingeyajua maneno ya Mzee Jomo Kenyatta "Learn to fight your own battle" isingeachana na mpango wake wa nyuklia mwaka 1994. Wangejifunza kupigana vita yao wenyewe bila kutegemea mtu.! (Malisa GJ)
Like
1
· 0 Comments ·0 Shares ·69 Views