Rais wa Marekani , Donald Trump ametoa siri kuwa Ofisi yake imepokea barua kutoka kwa Rais wa Ukraine , Volodymyr Zelensky, ikisema yuko tayari kwa mazungumzo na Russia na kusaini makubaliano ya madini adimu.
“Ukraine iko tayari kukaa kwenye meza ya mazungumzo haraka iwezekanavyo ili kuleta amani ya kudumu. Hakuna anayetaka amani zaidi ya Waukraine,” Trump amesema katika hotuba yake bungeni usiku wa kuamkia leo huku akinukuu barua hiyo.
“Mimi na timu yangu tuko tayari kufanya kazi chini ya uongozi thabiti wa Rais Trump ili kupata amani ya kudumu’,” Trump alinukuu maneno ya Zelenskyy.
“Si hilo lingekuwa jambo zuri?” aliuliza. “Ni wakati wa kukomesha huu upuuzi. Ni wakati wa kusitisha mauaji. Ni wakati wa kumaliza vita hivi visivyo na maana. Ukitaka kumaliza vita, lazima uzungumze na pande zote mbili,” amesema Trump.
Kauli hiyo ya Trump imekuja siku chache baada ya mvutano mkali kati yake na Zelenskyy katika Ofisi ya Oval iliyoko Ikulu ya White House, hali iliyosababisha Marekani kusitisha msaada muhimu wa kijeshi kwa Ukraine.

Rais wa Marekani πΊπΈ, Donald Trump ametoa siri kuwa Ofisi yake imepokea barua kutoka kwa Rais wa Ukraine πΊπ¦, Volodymyr Zelensky, ikisema yuko tayari kwa mazungumzo na Russia π·πΊ na kusaini makubaliano ya madini adimu.
“Ukraine iko tayari kukaa kwenye meza ya mazungumzo haraka iwezekanavyo ili kuleta amani ya kudumu. Hakuna anayetaka amani zaidi ya Waukraine,” Trump amesema katika hotuba yake bungeni usiku wa kuamkia leo huku akinukuu barua hiyo.
“Mimi na timu yangu tuko tayari kufanya kazi chini ya uongozi thabiti wa Rais Trump ili kupata amani ya kudumu’,” Trump alinukuu maneno ya Zelenskyy.
“Si hilo lingekuwa jambo zuri?” aliuliza. “Ni wakati wa kukomesha huu upuuzi. Ni wakati wa kusitisha mauaji. Ni wakati wa kumaliza vita hivi visivyo na maana. Ukitaka kumaliza vita, lazima uzungumze na pande zote mbili,” amesema Trump.
Kauli hiyo ya Trump imekuja siku chache baada ya mvutano mkali kati yake na Zelenskyy katika Ofisi ya Oval iliyoko Ikulu ya White House, hali iliyosababisha Marekani kusitisha msaada muhimu wa kijeshi kwa Ukraine.
0 Comments
Β·0 Shares
Β·18 Views