"Kupitia kituo cha Wasafi, Kamishna wa mchezo wa Simba na Yanga wa raundi ya kwanza Khalid Bitebo ameomba radhi kuwa aliteleza sio kweli kwamba Yanga walifanya mazoezi ya mwisho kwenye uwanja wa Mkapa kwenye Derby iliyopita, kifupi ameomba radhi kuwa alijichanganya.

Na huo ndio ukweli ulio wazi kuwa kwenye historia ya Derby hakuna aliyewahi kufanya mazoezi siku moja kabla ya mchezo pale hata Mimi siku ya kwanza ya sakata hili niliripoti kuwa Yanga alifanya mazoezi pale ila sio kweli hawakufanya, Simba na Yanga hata mechi yao iwe Mwanza au Kigoma hawafanyi mazoezi kwenye uwanja wa game, inaenda mbali hadi pitch feeling wanakwepa.

Wakongwe wa Simba na Yanga pia wakanikumbusha zamani kwanza walikuwa wote wanapakimbia Dar Es Slaaam sio Mgeni wala Mwenyeji wa mechi, mwingine anaenda Pemba mwingine Morogoro, mara Zanzibar mwingine Pemba, timu zinakutana Mjini Mzizima hapa siku ya mbungi na inapigwa kwelikweli ndio utaratibu wao.

Kwakuwa Kamishna wa mchezo ameomba radhi nadhani ni muhimu ila sio lazima basi na wale waliounga mkono, wakaaminisha Umma kuwa Yanga alifanya mazoezi pale wakaomba radhi pia, ni muhimu ila sio lazima ni katika kuweka kumbukumbu tu sawa, tunakubaliana?" - Farhan JR, Mchambuzi.

"Kupitia kituo cha Wasafi, Kamishna wa mchezo wa Simba na Yanga wa raundi ya kwanza Khalid Bitebo ameomba radhi kuwa aliteleza sio kweli kwamba Yanga walifanya mazoezi ya mwisho kwenye uwanja wa Mkapa kwenye Derby iliyopita, kifupi ameomba radhi kuwa alijichanganya. Na huo ndio ukweli ulio wazi kuwa kwenye historia ya Derby hakuna aliyewahi kufanya mazoezi siku moja kabla ya mchezo pale hata Mimi siku ya kwanza ya sakata hili niliripoti kuwa Yanga alifanya mazoezi pale ila sio kweli hawakufanya, Simba na Yanga hata mechi yao iwe Mwanza au Kigoma hawafanyi mazoezi kwenye uwanja wa game, inaenda mbali hadi pitch feeling wanakwepa. Wakongwe wa Simba na Yanga pia wakanikumbusha zamani kwanza walikuwa wote wanapakimbia Dar Es Slaaam sio Mgeni wala Mwenyeji wa mechi, mwingine anaenda Pemba mwingine Morogoro, mara Zanzibar mwingine Pemba, timu zinakutana Mjini Mzizima hapa siku ya mbungi na inapigwa kwelikweli ndio utaratibu wao. Kwakuwa Kamishna wa mchezo ameomba radhi nadhani ni muhimu ila sio lazima basi na wale waliounga mkono, wakaaminisha Umma kuwa Yanga alifanya mazoezi pale wakaomba radhi pia, ni muhimu ila sio lazima ni katika kuweka kumbukumbu tu sawa, tunakubaliana?" - Farhan JR, Mchambuzi.
Like
1
· 0 التعليقات ·0 المشاركات ·139 مشاهدة