Taasisi ya dini ya Kiislamu ya Al-Hikma Foundation imetangaza kuwalipia mahari vijana 200 ambao wapo tayari kuoa.

Akizungumza katika mashindano ya 25 ya kimataifa ya uhifadhi wa Qur'an yaliyofanyika leo Jumapili, Machi 16, 2023, katika Uwanja wa Mkapa na Uhuru, jijini Dar es Salaam, Sheikh Nurdin Kishki, ambaye ni Mwenyekiti wa taasisi hiyo, amesema kuwa mwaka huu Vijana 200 watakaolipiwa mahari 100 watatoka Tanzania , na wengine 100 kutoka Nchini Burundi .

"Kutokana na idadi ya watu wasiokuwa kwenye ndoa, mwaka huu tutaozesha vijana 200. Ndoa 100 zitafungwa Tanzania na 100 nyingine kwa ndugu zetu wa Burundi. Mahari na gharama nyingine za ndoa tutatoa sisi, Al-Hikma Foundation,"

Pia, Sheikh Kishki ameeleza kuwa taasisi hiyo itawalipia gharama za tohara kwa watoto wa kiume 1000 Nchini Tanzania. Amesema mambo hayo yanafanyika kupitia programu maalumu iliyoanzishwa na taasisi hiyo ya kurejesha kwa jamii kupitia mashindano hayo.

Taasisi ya dini ya Kiislamu ya Al-Hikma Foundation imetangaza kuwalipia mahari vijana 200 ambao wapo tayari kuoa. Akizungumza katika mashindano ya 25 ya kimataifa ya uhifadhi wa Qur'an yaliyofanyika leo Jumapili, Machi 16, 2023, katika Uwanja wa Mkapa na Uhuru, jijini Dar es Salaam, Sheikh Nurdin Kishki, ambaye ni Mwenyekiti wa taasisi hiyo, amesema kuwa mwaka huu Vijana 200 watakaolipiwa mahari 100 watatoka Tanzania 🇹🇿, na wengine 100 kutoka Nchini Burundi 🇧🇮. "Kutokana na idadi ya watu wasiokuwa kwenye ndoa, mwaka huu tutaozesha vijana 200. Ndoa 100 zitafungwa Tanzania na 100 nyingine kwa ndugu zetu wa Burundi. Mahari na gharama nyingine za ndoa tutatoa sisi, Al-Hikma Foundation," Pia, Sheikh Kishki ameeleza kuwa taasisi hiyo itawalipia gharama za tohara kwa watoto wa kiume 1000 Nchini Tanzania. Amesema mambo hayo yanafanyika kupitia programu maalumu iliyoanzishwa na taasisi hiyo ya kurejesha kwa jamii kupitia mashindano hayo.
0 Yorumlar ·0 hisse senetleri ·71 Views