BODI YA LIGI SIO CHOMBO HURU KWA MUJIBU WA RAIS WA TFF WALLECE KARIA.

Dhumuni la Baba wa Taifa kupigania uhuru wa Tanganyika ilikuwa kuhitaji Tanganyika kuwa huru ili iweze kujiamulia mambo yake na kujipangia kipi ifanye kwa wakati wowote.

Uhuru ni Jambo la msingi sana kwa binadamu yoyote kwani humsaidia katika kufanya maamuzi yake binafsi.

Kwa mujibu wa kauli za Rais wa TFF Baba Yangu Mzee Wallece Karia ni dhahiri shahiri kuwa bodi ya ligi sio chombo huru.

Wallece Karia akiwa katika mahojiano Wasafi Fm katika kipindi cha “Jana na Leo” Alisema kuwa

“Kuna siku tulipokea Barua kutoka CAF Wakihitaji waamuzi wetu Wawili kwenda kuchezesha michuano ya kimataifa”

“Wakati barua ile imekuja ofisini kuhitaji wale waamuzi kulikuwa na changamoto, Kwani mojawapo ya wale waamuzi ambae ni Ahmed Arajiga alikuwa amefungiwa na kamati ya masaa 72”

“Ilikuwa ngumu sana kwangu, maana CAF wamemtaka mwamuzi alafu huku kwetu kamati imemfungia, lakini nikafanya maamuzi”

“Nilifanya maamuzi nikawaambia hawa waamuzi waruhusiwe waende, Walienda wote wawili lakini bahati mbaya mmoja ndio alifuzu ambae ni Ahmed Arajiga”

“Yalikuwa maamuzi magumu ila sikuwa na namna n Ahmed Arajiga alienda kuwakilisha Tanzania vema sana, Hata mechi aliyochezesha alichezesha vizuri sana”

Kwa maelezo ya Wallece Karia aliingilia maamuzi ya Kamati ya Masaa 72 ambayo ipo chini ya bodi ya ligi. Kumruhusu Mwamuzi aliyefungiwa katika ligi kwenda kuchezesha mechi za kimataifa.
(khalil ufadiga)

BODI YA LIGI SIO CHOMBO HURU KWA MUJIBU WA RAIS WA TFF WALLECE KARIA. Dhumuni la Baba wa Taifa kupigania uhuru wa Tanganyika ilikuwa kuhitaji Tanganyika kuwa huru ili iweze kujiamulia mambo yake na kujipangia kipi ifanye kwa wakati wowote. Uhuru ni Jambo la msingi sana kwa binadamu yoyote kwani humsaidia katika kufanya maamuzi yake binafsi. Kwa mujibu wa kauli za Rais wa TFF Baba Yangu Mzee Wallece Karia ni dhahiri shahiri kuwa bodi ya ligi sio chombo huru. Wallece Karia akiwa katika mahojiano Wasafi Fm katika kipindi cha “Jana na Leo” Alisema kuwa “Kuna siku tulipokea Barua kutoka CAF Wakihitaji waamuzi wetu Wawili kwenda kuchezesha michuano ya kimataifa” “Wakati barua ile imekuja ofisini kuhitaji wale waamuzi kulikuwa na changamoto, Kwani mojawapo ya wale waamuzi ambae ni Ahmed Arajiga alikuwa amefungiwa na kamati ya masaa 72” “Ilikuwa ngumu sana kwangu, maana CAF wamemtaka mwamuzi alafu huku kwetu kamati imemfungia, lakini nikafanya maamuzi” “Nilifanya maamuzi nikawaambia hawa waamuzi waruhusiwe waende, Walienda wote wawili lakini bahati mbaya mmoja ndio alifuzu ambae ni Ahmed Arajiga” “Yalikuwa maamuzi magumu ila sikuwa na namna n Ahmed Arajiga alienda kuwakilisha Tanzania vema sana, Hata mechi aliyochezesha alichezesha vizuri sana” Kwa maelezo ya Wallece Karia aliingilia maamuzi ya Kamati ya Masaa 72 ambayo ipo chini ya bodi ya ligi. Kumruhusu Mwamuzi aliyefungiwa katika ligi kwenda kuchezesha mechi za kimataifa. (khalil ufadiga)
0 التعليقات ·0 المشاركات ·76 مشاهدة