Kwenye barua ambayo Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara (TPLB) imewajibu Yanga yenye kumbukumbu namba TPLB/2024/625 ya Machi 16,2025 imewaambia Yanga hawawezi kupewa alama tatu kutokana na kuwa hakuna KANUNI ya Ligi Kuu inayoamuru jambo hilo ambapo TPLB imewapa sababu takribani 10, nitazielezea kwa uchache.

1. Mchezo ulighairishwa na Bodi majira ya saa8 Mchana ambapo baada ya Bodi huo hapakuwa na Afisa yoyote wa mchezo zaidi ya Watu wa Usalama.

2. Hakuna taratibu zozote za mchezo zilizofanyika uwanjani kwa mujibu wa Kanuni ya 17 ikiwemo timu kukaguliwa na ili timu ipewe alama tatu na mabao matatu ilipaswa ukaguzi kufanyika na Maafisa ww Mchezo.

3. Bodi ilishindwa kuruhusu mchezo uchezwe sio kwasababu Simba ALIGOMEA mechi bali kupitia Kamati ya Masaa 72 ikaamuru kupitia sababu mbalimbali za Kikanuni kughairisha mchezo huo baada ya kupokea pia ripoti mbalimbali kutoka Maafisa wa mchezo huo.

4. Yanga SC wameambiwa kwamba hakuna Kanuni inasema Klabu Mgeni anapaswa kuwataarifu wao kwamba wanakuja kufanya mazoezi, hivyo suala la mawasiliano ni MWONGOZO tu wa Bodi hivyo Simba haikuvunja Kanuni kutowasiliana bali ilivunja MIONGOZO.

5. Yanga SC wamejibiwa kuwa haitowapa alama tatu kwakuwa sababu za kughairisha mchezo zilikuwa ni za kiusalama, ambapo kulikuwa na tuhuma za rushwa, vitisho na kasoro za Kiusalama hivyo ingekuwa ngumu kuruhusu mchezo uendelee ambao ungeleta kasoro, kabla, wakati na baada ya mchezo.

6. Yanga SC wanalaumiwa na Bodi kitendo cha kupeleka timu uwanjani wakati mechi imeshaghairishwa ni kinyume na Kanuni ya 47(18) na imeonesha kupingana na Mamlaka.

7. Kuhusu gharama za mchezo ambazo Yanga wameziingia Bodi inasema itazighulikia Kikanuni.

8. Bodi imewatakia Yanga maandalizi mema ya mchezo ujao wa Derby ambapo watawapangia rasmi tarehe.
Etc.

Kwenye barua ambayo Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara (TPLB) imewajibu Yanga yenye kumbukumbu namba TPLB/2024/625 ya Machi 16,2025 imewaambia Yanga hawawezi kupewa alama tatu kutokana na kuwa hakuna KANUNI ya Ligi Kuu inayoamuru jambo hilo ambapo TPLB imewapa sababu takribani 10, nitazielezea kwa uchache. 1. Mchezo ulighairishwa na Bodi majira ya saa8 Mchana ambapo baada ya Bodi huo hapakuwa na Afisa yoyote wa mchezo zaidi ya Watu wa Usalama. 2. Hakuna taratibu zozote za mchezo zilizofanyika uwanjani kwa mujibu wa Kanuni ya 17 ikiwemo timu kukaguliwa na ili timu ipewe alama tatu na mabao matatu ilipaswa ukaguzi kufanyika na Maafisa ww Mchezo. 3. Bodi ilishindwa kuruhusu mchezo uchezwe sio kwasababu Simba ALIGOMEA mechi bali kupitia Kamati ya Masaa 72 ikaamuru kupitia sababu mbalimbali za Kikanuni kughairisha mchezo huo baada ya kupokea pia ripoti mbalimbali kutoka Maafisa wa mchezo huo. 4. Yanga SC wameambiwa kwamba hakuna Kanuni inasema Klabu Mgeni anapaswa kuwataarifu wao kwamba wanakuja kufanya mazoezi, hivyo suala la mawasiliano ni MWONGOZO tu wa Bodi hivyo Simba haikuvunja Kanuni kutowasiliana bali ilivunja MIONGOZO. 5. Yanga SC wamejibiwa kuwa haitowapa alama tatu kwakuwa sababu za kughairisha mchezo zilikuwa ni za kiusalama, ambapo kulikuwa na tuhuma za rushwa, vitisho na kasoro za Kiusalama hivyo ingekuwa ngumu kuruhusu mchezo uendelee ambao ungeleta kasoro, kabla, wakati na baada ya mchezo. 6. Yanga SC wanalaumiwa na Bodi kitendo cha kupeleka timu uwanjani wakati mechi imeshaghairishwa ni kinyume na Kanuni ya 47(18) na imeonesha kupingana na Mamlaka. 7. Kuhusu gharama za mchezo ambazo Yanga wameziingia Bodi inasema itazighulikia Kikanuni. 8. Bodi imewatakia Yanga maandalizi mema ya mchezo ujao wa Derby ambapo watawapangia rasmi tarehe. Etc.
0 Commentarios ·0 Acciones ·35 Views