"Sijui kama mnaona jinsi Trump na Marekani yake wanavyocheza na Dunia kupitia ugomvi au migogoro ya Dunia ili kuipatia faida Marekani kwa kisingizio cha kutafuta amani huku nyuma ya pazia Marekani ikipata faida kupitia migogoro au vita.

Tazama Makubaliano ya Madini pale Ukraine
Ambapo Marekani watafaidika na Rasilimali za madini za Ukraine, yani ili Marekani waisadie Ukraine ni lazima Ukraine kuipatia madini yake Marekani

Congo nayo inakaribia kusaini mkataba wa kuipatia Marekani madini ili Marekani iipatie ulinzi hapo tunazungumzia rasimali za Congo amabzo zinaenda kutumika kama faida kwa Marekani kisa tu ni ugomvi wa Afrika wenyewe kwa wenyewe na hapo hapo Trump katupiga Bao

Huko Gaza napo mpango wa kuwahamisha wakazi wa Gaza kwa kisingizio cha kuijenga upya Gaza umeiva, Trump haijengi Gaza bure anafahamu fika kuwa chini ya ardhi ya Gaza kuna utajiri mkubwa wa maliasili ya Gesi na mafuta

Huyo ndiye Trump mfanyabiashara kutoka White House ambaye anaenda sambamba na ule msemo unaosema "no free lunch in America" yaani hakuna chakula cha mchana cha bure Marekani, ukiona unapewa cha bure ujue badae utalipia tu!!" - Zungu, Mtangazaji na Mchambuzi wa Siasa.

"Sijui kama mnaona jinsi Trump na Marekani yake wanavyocheza na Dunia kupitia ugomvi au migogoro ya Dunia ili kuipatia faida Marekani kwa kisingizio cha kutafuta amani huku nyuma ya pazia Marekani ikipata faida kupitia migogoro au vita. Tazama Makubaliano ya Madini pale Ukraine Ambapo Marekani watafaidika na Rasilimali za madini za Ukraine, yani ili Marekani waisadie Ukraine ni lazima Ukraine kuipatia madini yake Marekani Congo nayo inakaribia kusaini mkataba wa kuipatia Marekani madini ili Marekani iipatie ulinzi hapo tunazungumzia rasimali za Congo amabzo zinaenda kutumika kama faida kwa Marekani kisa tu ni ugomvi wa Afrika wenyewe kwa wenyewe na hapo hapo Trump katupiga Bao Huko Gaza napo mpango wa kuwahamisha wakazi wa Gaza kwa kisingizio cha kuijenga upya Gaza umeiva, Trump haijengi Gaza bure anafahamu fika kuwa chini ya ardhi ya Gaza kuna utajiri mkubwa wa maliasili ya Gesi na mafuta Huyo ndiye Trump mfanyabiashara kutoka White House ambaye anaenda sambamba na ule msemo unaosema "no free lunch in America" yaani hakuna chakula cha mchana cha bure Marekani, ukiona unapewa cha bure ujue badae utalipia tu!!" - Zungu, Mtangazaji na Mchambuzi wa Siasa.
0 Comments ·0 Shares ·42 Views