Nchi ya Ufaransa imepinga vikali kauli ya Waziri wa Ulinzi wa Israel , Israel Katz, aliyedokeza uwezekano wa Israel kutwaa baadhi ya maeneo ya Ukanda wa Gaza iwapo Kundi la Hamas haitowaachia huru mateka waliosalia. Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa, Jean-Noel Barrot, amesema kuwa Ufaransa inapinga aina yoyote ya unyakuzi wa ardhi ya Palestina, iwe Gaza au Ukingo wa Magharibi. Kauli hiyo inakuja wakati ambapo Israel imezidisha mashambulizi yake Gaza, hali iliyosababisha maelfu ya wakazi wa maeneo ya Al-Salatin, Al-Karama, na Al-Awda kusini mwa Gaza kuamriwa kuyahama makazi yao kabla ya mashambulizi mapya.
Katika tukio jingine, Jeshi la Israel lilidungua makombora mawili yaliyofyatuliwa na Hamas kuelekea mji wa Ashkelon, ambapo Hamas ilidai kuwa shambulio hilo ni jibu kwa mashambulizi dhidi ya raia wa Gaza. Waziri wa Ulinzi wa Israel ameapa kuendeleza mashambulizi ya angani, majini, na ardhini hadi mateka wote waachiliwe na Hamas ishindwe kabisa.
Hatua hizi za Israel zimezua ukosoaji mkubwa kimataifa. Uturuki imelaani shambulio la Israel dhidi ya hospitali iliyojengwa na nchi hiyo huko Gaza, huku Rais wa Urusi , Vladimir Putin, akielezea kusikitishwa kwake na mashambulizi hayo.

Nchi ya Ufaransa ๐ซ๐ท imepinga vikali kauli ya Waziri wa Ulinzi wa Israel ๐ฎ๐ฑ, Israel Katz, aliyedokeza uwezekano wa Israel kutwaa baadhi ya maeneo ya Ukanda wa Gaza iwapo Kundi la Hamas haitowaachia huru mateka waliosalia. Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa, Jean-Noel Barrot, amesema kuwa Ufaransa inapinga aina yoyote ya unyakuzi wa ardhi ya Palestina, iwe Gaza au Ukingo wa Magharibi. Kauli hiyo inakuja wakati ambapo Israel imezidisha mashambulizi yake Gaza, hali iliyosababisha maelfu ya wakazi wa maeneo ya Al-Salatin, Al-Karama, na Al-Awda kusini mwa Gaza kuamriwa kuyahama makazi yao kabla ya mashambulizi mapya.
Katika tukio jingine, Jeshi la Israel lilidungua makombora mawili yaliyofyatuliwa na Hamas kuelekea mji wa Ashkelon, ambapo Hamas ilidai kuwa shambulio hilo ni jibu kwa mashambulizi dhidi ya raia wa Gaza. Waziri wa Ulinzi wa Israel ameapa kuendeleza mashambulizi ya angani, majini, na ardhini hadi mateka wote waachiliwe na Hamas ishindwe kabisa.
Hatua hizi za Israel zimezua ukosoaji mkubwa kimataifa. Uturuki ๐น๐ท imelaani shambulio la Israel dhidi ya hospitali iliyojengwa na nchi hiyo huko Gaza, huku Rais wa Urusi ๐ท๐บ, Vladimir Putin, akielezea kusikitishwa kwake na mashambulizi hayo.
0 Comments
ยท0 Shares
ยท26 Views