Rais wa Nchi ya Iran , Ayatollah Ali Khamenei, amesema kuwa vitisho vya Nchi ya Marekani dhidi ya Taifa lake havisaidii lolote na havitaleta matokeo yoyote kama Rais Donald Tramp anavyofikiria. Kiongozi huyo amesema hayo baada ya Rais Trump kuonya uwezekano wa hatua za kijeshi kuchukuliwa dhidi ya Iran.

"Wamarekani wanapaswa kuelewa kwamba vitisho havitafanikiwa wanapokabiliana na Iran. Wao (Marekani) na wengine wanapaswa kufahamu kuwa wakifanya lolote baya dhidi ya taifa la Iran, watajibiwa kwa nguvu kubwa." alisema Rais Khemenei

Mnamo Machi 7, Rais Trump alisema kuwa alimwandikia barua Rais Khamenei, akimtaka kuanzisha mazungumzo kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran, huku akionya kuwa kuna uwezekano wa kuchukua hatua za kijeshi iwapo Iran itakataa. Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi, alisema Alhamisi wiki hii kuwa barua hiyo ilikuwa zaidi ya tishio, ingawa pia ilionesha uwezekano wa mazungumzo.

"Tunachunguza kwa kina maudhui ya barua hiyo, na tutajibu rasmi katika siku chache zijazo” alisema Waziri huyo

Kulingana na ripoti ya tovuti ya habari ya Marekani, Axios, ikimnukuu Afisa wa Serikali ya Trump na vyanzo vingine vikisema, barua hiyo inaweka muda wa miezi miwili wa kufikia makubaliano mapya ya nyuklia. Hata hivyo, haijabainishwa ni lini muda huo utaanza au kuisha. Kwa muda mrefu, Rais Khamenei amepuuza wito wa Rais Trump wa mazungumzo ya moja kwa moja, akisema kuwa Rais huyo wa Marekani anajaribu kudanganya ulimwengu kwa kuonesha kuwa Marekani iko tayari kwa mazungumzo huku Iran ikionekana kutotaka kushiriki.

Ikumbukwe kwamba Trump ambaye alianza muhula wake wa pili Januari 2025, amerudisha sera yake ya shinikizo la juu dhidi ya Iran. Wakati wa kipindi chake cha kwanza, Trump aliiondoa Marekani kwenye makubaliano ya kihistoria ya nyuklia ya 2015 kati ya Iran na mataifa yenye nguvu ulimwenguni na akairejeshea Tehran vikwazo vikubwa vya kiuchumi.

Rais wa Nchi ya Iran ๐Ÿ‡ฎ๐Ÿ‡ท, Ayatollah Ali Khamenei, amesema kuwa vitisho vya Nchi ya Marekani ๐Ÿ‡บ๐Ÿ‡ธ dhidi ya Taifa lake havisaidii lolote na havitaleta matokeo yoyote kama Rais Donald Tramp anavyofikiria. Kiongozi huyo amesema hayo baada ya Rais Trump kuonya uwezekano wa hatua za kijeshi kuchukuliwa dhidi ya Iran. "Wamarekani wanapaswa kuelewa kwamba vitisho havitafanikiwa wanapokabiliana na Iran. Wao (Marekani) na wengine wanapaswa kufahamu kuwa wakifanya lolote baya dhidi ya taifa la Iran, watajibiwa kwa nguvu kubwa." alisema Rais Khemenei Mnamo Machi 7, Rais Trump alisema kuwa alimwandikia barua Rais Khamenei, akimtaka kuanzisha mazungumzo kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran, huku akionya kuwa kuna uwezekano wa kuchukua hatua za kijeshi iwapo Iran itakataa. Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi, alisema Alhamisi wiki hii kuwa barua hiyo ilikuwa zaidi ya tishio, ingawa pia ilionesha uwezekano wa mazungumzo. "Tunachunguza kwa kina maudhui ya barua hiyo, na tutajibu rasmi katika siku chache zijazo” alisema Waziri huyo Kulingana na ripoti ya tovuti ya habari ya Marekani, Axios, ikimnukuu Afisa wa Serikali ya Trump na vyanzo vingine vikisema, barua hiyo inaweka muda wa miezi miwili wa kufikia makubaliano mapya ya nyuklia. Hata hivyo, haijabainishwa ni lini muda huo utaanza au kuisha. Kwa muda mrefu, Rais Khamenei amepuuza wito wa Rais Trump wa mazungumzo ya moja kwa moja, akisema kuwa Rais huyo wa Marekani anajaribu kudanganya ulimwengu kwa kuonesha kuwa Marekani iko tayari kwa mazungumzo huku Iran ikionekana kutotaka kushiriki. Ikumbukwe kwamba Trump ambaye alianza muhula wake wa pili Januari 2025, amerudisha sera yake ya shinikizo la juu dhidi ya Iran. Wakati wa kipindi chake cha kwanza, Trump aliiondoa Marekani kwenye makubaliano ya kihistoria ya nyuklia ya 2015 kati ya Iran na mataifa yenye nguvu ulimwenguni na akairejeshea Tehran vikwazo vikubwa vya kiuchumi.
0 Comments ยท0 Shares ยท48 Views