Jeshi la Nchi ya Uganda limesema limewaua Wapiganaji 242 wa kundi la Waasi Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo linalojulikana kama CODECO baada ya kushambulia kambi ya Jeshi hilo la Uganda mpakani mashariki mwa DR Congo mapema wiki hii ambapo madai yamepingwa na Kundi hilo.
Msemaji wa Jeshi la Uganda, Chris Magezi, amesema mamia ya Wapiganaji wa kundi la CODECO walishambulia kituo cha kijeshi cha Uganda People's Defence Forces (UPDF) katika eneo la Fataki, Mkoani Ituri, siku ya Jumatano na Alhamisi. Jeshi hilo lilijibu mashambulizi hayo mara zote mbili, likiwaangamiza Wapiganaji 31 siku ya kwanza na 211 siku ya pili, Magezi alisema katika chapisho kwenye akaunti yake ya Mtandao wa X Ijumaa usiku na kuongeza kuwa askari mmoja wa UPDF aliuawa na wengine wanne kujeruhiwa.
Msemaji wa CODECO, Basa Zukpa Gerson, alipinga taarifa ya jeshi Jumamosi, akisema kundi hilo lilipoteza wapiganaji wawili tu na kwamba idadi ya vifo vya Wanajeshi wa UPDF ilikuwa juu zaidi. Chanzo kimoja cha Umoja wa Mataifa ambacho hakikutaka kutajwa jina kilisema Waasi 70 na Wanajeshi wa Uganda 12 waliuawa.
Kulikuwa na mapigano zaidi kati ya pande hizo mbili asubuhi ya Jumamosi, alisema Msemaji wa CODECO na kiongozi mmoja wa jamii za kiraia wa eneo hilo. Wapiganaji wa CODECO wanasema lengo lao ni kuwalinda Wakulima wa Lendu dhidi ya Wafungaji wa Hema, ambao kihistoria wamekuwa wakigombana kuhusu ardhi.
Kundi hilo ni moja ya makundi mengi ya Waasi yanayopigania ardhi na rasilimali za madini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ambapo Waasi wa M23 wameongeza mashambulizi mwaka huu na kupata mafanikio makubwa. Uganda ilituma wanajeshi DR Congo mwaka 2021 kusaidia Serikali kupambana na kundi lingine la Waasi, Allied Democratic Forces (ADF), ambalo lina uhusiano na Islamic State na linafanya mashambulizi ya kikatili kwenye baadhi ya Vijiji.

Jeshi la Nchi ya Uganda 馃嚭馃嚞 limesema limewaua Wapiganaji 242 wa kundi la Waasi Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo 馃嚚馃嚛 linalojulikana kama CODECO baada ya kushambulia kambi ya Jeshi hilo la Uganda mpakani mashariki mwa DR Congo mapema wiki hii ambapo madai yamepingwa na Kundi hilo.