"Najisikia vibaya namna watu wanavyoniona na kuanza kuniita Yesu, wanafikia hata kutundika picha zangu katika nyumba zao, mimi ni mwigizaji tu, mimi ni mtu" - Jonathan Roumie(50), mwigizaji wa Marekani
Aidha, Jonathan Roumie katika mahojiano amesema maisha yake binafsi alikuwa na hali mbaya kiuchumi hakuwa na uhakika siku inayofuata atakula nini, alikuwa mwigizaji ila kiuchumi alikuwa bado hajafanikiwa. Baada ya mambo kuzidi kuwa magumu siku moja ni kama alikuwa anamuomba Mungu kuhusu hali anayopitia ili mambo yake yakae sawa
Baada ya miezi kama mitatu ndio akapata nafasi ya kuigiza kama Yesu katika series ya "The Chosen" iliyoanza kuoneshwa 2017 ambayo imejipatia umaarufu mkubwa sana hadi sasa imetazamwa na watu zaidi ya milioni 250 na misimu mipya inafuata huku ikipongezwa kwa kinachoonekana kuigizwa
Umaarufu wa uhusika wake kama Yesu umempa umaarufu mkubwa na fursa nyingi ikiwemo katika mikutano na makongamano makubwa ya kidini na app za dini ya kikiristo
Jonathan ambaye ni mkatoliki, alipoulizwa na New York Times, je ni tukio gani gumu analokumbuka ambalo alishakutana nalo baada ya kuigiza kama Yesu, amejibu kwa kusema kuna kipindi alikuwa katika mkutano kwenye uwanja wenye watu takribani 40,000 baadaye alishuka stejini akaenda kwenye chumba fulani uwanjani hapo, mmoja wa walinzi alikuja akamwambia nje kuna mwanamke ana mtoto kwenye kiti cha magurudumu anaomba kusalimiana na wewe
Jonathan alitoka akaonana na mwanamke husika na mwanae ambaye kwa ufupi alieleza jinsi Yesu alivyoponya mtu katika hiyo series ya "The Chosen" na kusema angependa mwanae pia apone yaani akimtaka Jonathan amponye mtoto wake. Ilibidi Jonathan amueleze ukweli kwamba yeye sio mponyaji wala mhubiri bali ni mwigizaji tu.
Jonathan akamueleza wafanye maombi wote ilichukua kama dakika moja, walipomaliza maombi wakafurahi na kushukuru kisha Jonathan akarudi alipokuwa huku akitokwa na machozi akihisi amewaangusha matarajio waliyokuwa nayo kwake ila amesema ni bora waujue ukweli kuwa yeye sio Yesu wala mponyaji bali ni mwigizaji tu
Ukiacha hayo ya uhusika wake wa Yesu na dini, Jonathan Roumie amegusia pia kwamba alishafika Tanzania na Rwanda sababu kuna watoto kadhaa wanaoishi katika mazingira magumu huwa anawasaidia na familia zao
Jonathan Roumie pia ameweka wazi kwamba anatamani watu pia wawe wanamuona katika nyuma ya pazia(behind the scene) anayopitia katika kujiandaa na uigizaji wake kama Yesu ili watu wengine waelewe wajue kumtofautisha katika maisha halisi na kisanaa
KUMBUKA, zipo filamu nyingine miaka ya nyuma kuhusu Yesu zilizohusisha waigizaji wengine kabla ya sasa Jonathan Roumie kupata umaarufu na uhusika wa Yesu katika series maarufu ya "The Chosen"
(Swahili Word)