Balozi wa Afrika Kusini Nchini Marekani , Ebrahim Rasool ambaye ametimuliwa na Nchi ya Marekani kutokana na kukosoa sera za Donald Trump, amerejea Afrika Kusini kwa ufakhari mkubwa na kupokewa kwa shangwe na mamia ya Wananchi waliofurika kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Cape Town Nchini Afrika Kusini.

Balozi huyo na mkewe, Rosieda, waliwasili jana katika Uwanda wa Ndege wa Kimataifa wa Cape Town baada ya kusafari kutoka Nchini Marekani kupitia Qatar na wamekaribishwa vyema na kwa shangwe na mamia ya Wafuasi wao. Mapema mwezi huu, Balozi Rasool alitangazwa na Serikali ya Marekani kuwa ni Mtu asiyetakiwa kuweko Nchini humo baada ya kukosoa sera za Donald Trump, hatua ambayo inaonesha wazi jinsi madai ya uhuru wa kusema yasivyothaminiwa Nchini Marekani licha ya majigambo makubwa ya Nchi Marekani ya kupigania haki za Binadamu na demokrasia.

Akiwahutubia mamia ya Mashabiki wake kwenye Uwanja wa Ndege wa Cape Town, Balozi Rasool amesema kwamba ingawa ametakiwa kuondoka huko Marekani lakini jambo hilo limeshindwa kufikia lengo lake kwani Viongozi wa Marekani wanadhani wamemdhalilisha wakati yeye anaona fakhari kwa maneno aliyotoa na Wananchi wa Afrika Kusini nao wanajivunia msimamo huo ndio maana wamejitokea kwa mamia kumpokea kishujaa.

"Unaporejea nyumbani na kupokewa kwa shangwe na umati kama huu wa watu, mtu unaona fakhari na unajivunia msimamo wako." alisema Rasool.

Alipoulizwa iwapo diplomasia imeshindwa, amesema ukweli kwamba matamshi yake yamemfanya Trump na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Marco Rubio kuwa makini na hatua ya Serikali ya Marekani ya kumtangaza kuwa ni Mtu asiyetakiwa nchini humo ni ushahidi kwamba ujumbe wake umefika ngazi za juu kabisa za serikali ya Marekani.

Balozi wa Afrika Kusini 🇿🇦 Nchini Marekani 🇺🇸, Ebrahim Rasool ambaye ametimuliwa na Nchi ya Marekani kutokana na kukosoa sera za Donald Trump, amerejea Afrika Kusini kwa ufakhari mkubwa na kupokewa kwa shangwe na mamia ya Wananchi waliofurika kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Cape Town Nchini Afrika Kusini. Balozi huyo na mkewe, Rosieda, waliwasili jana katika Uwanda wa Ndege wa Kimataifa wa Cape Town baada ya kusafari kutoka Nchini Marekani kupitia Qatar na wamekaribishwa vyema na kwa shangwe na mamia ya Wafuasi wao. Mapema mwezi huu, Balozi Rasool alitangazwa na Serikali ya Marekani kuwa ni Mtu asiyetakiwa kuweko Nchini humo baada ya kukosoa sera za Donald Trump, hatua ambayo inaonesha wazi jinsi madai ya uhuru wa kusema yasivyothaminiwa Nchini Marekani licha ya majigambo makubwa ya Nchi Marekani ya kupigania haki za Binadamu na demokrasia. Akiwahutubia mamia ya Mashabiki wake kwenye Uwanja wa Ndege wa Cape Town, Balozi Rasool amesema kwamba ingawa ametakiwa kuondoka huko Marekani lakini jambo hilo limeshindwa kufikia lengo lake kwani Viongozi wa Marekani wanadhani wamemdhalilisha wakati yeye anaona fakhari kwa maneno aliyotoa na Wananchi wa Afrika Kusini nao wanajivunia msimamo huo ndio maana wamejitokea kwa mamia kumpokea kishujaa. "Unaporejea nyumbani na kupokewa kwa shangwe na umati kama huu wa watu, mtu unaona fakhari na unajivunia msimamo wako." alisema Rasool. Alipoulizwa iwapo diplomasia imeshindwa, amesema ukweli kwamba matamshi yake yamemfanya Trump na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Marco Rubio kuwa makini na hatua ya Serikali ya Marekani ya kumtangaza kuwa ni Mtu asiyetakiwa nchini humo ni ushahidi kwamba ujumbe wake umefika ngazi za juu kabisa za serikali ya Marekani.
Love
Like
3
· 0 Commenti ·0 condivisioni ·156 Views