Nchi za Niger , Burkina Faso na Mali zimetangaza rasmi kujiondoa katika Shirika la Kimataifa la Mataifa yanayozungumza Kifaransa la ‘Francophonie’ (OIF). Uamuzi huo umefanywa na Viongozi wa mataifa hayo yenye Serikali za kijeshi, Niger inaongozwa na Jenerali Abdourahamane Tchiani, Mali inaongozwa na Kanali Assimi Goïta na Burkina Faso inayoongozwa na Kapteni Ibrahim Traoré.

Viongozi hao wamedai OIF na taasisi zingine zilizo chini ya Ufaransa ni ukoloni mamboleo. OIF ni Shirila lililoundwa kwa madhumuni ya kukuza lugha ya Kifaransa na kuimarisha ushirikiano kati ya nchi zinazozungumza Kifaransa.

Gazeti la Le Monde la Nchini Ufaransa limeripoti kuwa taarifa ya pamoja ya Nchi hizo tatu ilisema kwamba OIF imegeuka kuwa ‘chombo cha kisiasa’ kinachoendeshwa na Ufaransa ili kuongeza unyonyaji wa rasilimali za mataifa hayo.

Nchi za Niger πŸ‡³πŸ‡ͺ, Burkina Faso πŸ‡§πŸ‡« na Mali πŸ‡²πŸ‡± zimetangaza rasmi kujiondoa katika Shirika la Kimataifa la Mataifa yanayozungumza Kifaransa la ‘Francophonie’ (OIF). Uamuzi huo umefanywa na Viongozi wa mataifa hayo yenye Serikali za kijeshi, Niger inaongozwa na Jenerali Abdourahamane Tchiani, Mali inaongozwa na Kanali Assimi Goïta na Burkina Faso inayoongozwa na Kapteni Ibrahim Traoré. Viongozi hao wamedai OIF na taasisi zingine zilizo chini ya Ufaransa πŸ‡«πŸ‡· ni ukoloni mamboleo. OIF ni Shirila lililoundwa kwa madhumuni ya kukuza lugha ya Kifaransa na kuimarisha ushirikiano kati ya nchi zinazozungumza Kifaransa. Gazeti la Le Monde la Nchini Ufaransa limeripoti kuwa taarifa ya pamoja ya Nchi hizo tatu ilisema kwamba OIF imegeuka kuwa ‘chombo cha kisiasa’ kinachoendeshwa na Ufaransa ili kuongeza unyonyaji wa rasilimali za mataifa hayo.
0 Commenti Β·0 condivisioni Β·70 Views