Jarida la Forbes toleo la mwaka huu wa 2025 limemtaja Manyabiashara wa Tanzania Mohamed Dewjl, kuwa miongoni mwa Watu Matajiri Duniani, akiwa na utajiri wa USD 2.2 bilioni sawa na Shilingi Trilioni 5.7 za Kitanzania. Mo Dewji, anakuwa tajiri namba 12 barani Afrika na namba moja Afrika Mashariki kwa kiwango hicho.

2. Orodha ya mwaka huu inaonyesha utajiri wa Mo
Dewji umeongezeka na kufikia, dola bilioni 2.2 kutoka dola bilioni 1.8 mwaka jana.

3. Orodha ya Forbes ya Matajiri wa Afrika kwa mwaka 2024 ilibainisha kuwa utajiri wa Mo Dewji umeongezeka kutoka dola bilioni 1.5 hadi bilioni 1.8.

4. Licha ya utajiri huo, MO Dewji kupitia kampuni ya Mohamed Entrprises Limited (MeTL) imezalisha ajira 40,000 kwa Watanzania, kupitia biashara 126 zinazofanywa na kampuni hiyo.

5. Lengo la Mo Dewji ni kuongeza ajira hadi kufikia laki moja kwa Watanzania na wana-Afrika Mashariki.

6. Mo Dewji kupitia MoDewjl Foundation, imeshirikiana na Serikali kupitia Wizara ya Maji, kuchimba visima, kukarabati na kutibu maji mkakati uliosaidia Watu zaidi ya 15,000 kupata maji salama ya kunywa.

7. Utajiri wa Mo Dewji haikushia kwenye maji na afya pekee, umekwenda zaidi na kuwekeza katika tasnia ya michezo ambako ni sehemu ya Mmiliki akiwekeza
asilimia 49 kwenye klabu ya Simba SC.

Jarida la Forbes toleo la mwaka huu wa 2025 limemtaja Manyabiashara wa Tanzania Mohamed Dewjl, kuwa miongoni mwa Watu Matajiri Duniani, akiwa na utajiri wa USD 2.2 bilioni sawa na Shilingi Trilioni 5.7 za Kitanzania. Mo Dewji, anakuwa tajiri namba 12 barani Afrika na namba moja Afrika Mashariki kwa kiwango hicho. 2. Orodha ya mwaka huu inaonyesha utajiri wa Mo Dewji umeongezeka na kufikia, dola bilioni 2.2 kutoka dola bilioni 1.8 mwaka jana. 3. Orodha ya Forbes ya Matajiri wa Afrika kwa mwaka 2024 ilibainisha kuwa utajiri wa Mo Dewji umeongezeka kutoka dola bilioni 1.5 hadi bilioni 1.8. 4. Licha ya utajiri huo, MO Dewji kupitia kampuni ya Mohamed Entrprises Limited (MeTL) imezalisha ajira 40,000 kwa Watanzania, kupitia biashara 126 zinazofanywa na kampuni hiyo. 5. Lengo la Mo Dewji ni kuongeza ajira hadi kufikia laki moja kwa Watanzania na wana-Afrika Mashariki. 6. Mo Dewji kupitia MoDewjl Foundation, imeshirikiana na Serikali kupitia Wizara ya Maji, kuchimba visima, kukarabati na kutibu maji mkakati uliosaidia Watu zaidi ya 15,000 kupata maji salama ya kunywa. 7. Utajiri wa Mo Dewji haikushia kwenye maji na afya pekee, umekwenda zaidi na kuwekeza katika tasnia ya michezo ambako ni sehemu ya Mmiliki akiwekeza asilimia 49 kwenye klabu ya Simba SC.
0 Commenti ·0 condivisioni ·159 Views