Msemaji wa klabu ya Yanga SC, Ali Kamwe alikamatwa na Jeshi Polisi baada ya mchezo wao dhidi ya klabu ya Tabora United majira ya saa saba na nusu usiku wa kuamkia leo hii. Ali Kamwe alipelekwa kituo kikubwa cha Polisi cha Mkoa na amelala ndani hapo na hadi sasa bado hajaachiwa.

Viongozi wa Yanga SC bado wanaendelea kufanya jitihada za kumtoa Ali Kamwe hapo haijawekwa bayana makosa aliyoyafanya Msemaji huyo. Taarifa iliyopo ni kuwa, inadaiwa Ali Kamwe alitoa kauli isiyokuwa nzuri kipindi anamjibu Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Paul Chacha kabla ya mechi kama sehemu ya utani baada ya Mkuu huyo kutoa ahadi ya Shilingi milioni sitini (60) endapo klabu ya Tabora United ikimfunga Yanga SC ambapo mchezo ulimalizika kwa ushindi wa Yanga SC wa mabao matatu kwa bila (0-3).

Msemaji wa klabu ya Yanga SC, Ali Kamwe alikamatwa na Jeshi Polisi baada ya mchezo wao dhidi ya klabu ya Tabora United majira ya saa saba na nusu usiku wa kuamkia leo hii. Ali Kamwe alipelekwa kituo kikubwa cha Polisi cha Mkoa na amelala ndani hapo na hadi sasa bado hajaachiwa. Viongozi wa Yanga SC bado wanaendelea kufanya jitihada za kumtoa Ali Kamwe hapo haijawekwa bayana makosa aliyoyafanya Msemaji huyo. Taarifa iliyopo ni kuwa, inadaiwa Ali Kamwe alitoa kauli isiyokuwa nzuri kipindi anamjibu Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Paul Chacha kabla ya mechi kama sehemu ya utani baada ya Mkuu huyo kutoa ahadi ya Shilingi milioni sitini (60) endapo klabu ya Tabora United ikimfunga Yanga SC ambapo mchezo ulimalizika kwa ushindi wa Yanga SC wa mabao matatu kwa bila (0-3).
Like
Wow
2
· 0 Commentaires ·0 Parts ·66 Vue